CHADEMA wamjia juu JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wamjia juu JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Mar 6, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshambulia Rais Jakaya Kikwete kikimtuhumu kushindwa kuisimamia serikali yake na hivyo kulifanya taifa kuwa katika hali tete inayohatarisha amani ya nchi. CHADEMA pia imemshutumu Rais Kikwete pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, kwa madai ya kutumia vibaya rasilimali za nchi kwa kuendesha shughuli zisizokuwa za kiserikali hususan za Chama cha Mapinduzi. CHADEMA katika taarifa yake nzito kwa vyombo vya habari jana, imesema kuwa Rais Kikwete ameshindwa kabisa kushughulikia udhaifu wa kiutendaji ndani ya serikali yake, jambo ambalo limesababisha kukosekana kwa utawala wa kisheria.

  Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, iliyoketi juzi jijini Arusha, imesema kuwa ni wazi kuwa vyombo vya serikali, likiwemo baraza la mawaziri, vimedhihirisha kukosa uwezo, umakini na uwajibikaji katika masuala mazito ya uendeshaji wa nchi, hali ambayo ni hatari kwa uhai wa taifa.
  Chama hicho kikuu cha upinzani kimesema kuongezeka kwa migogoro ya kijamii kuhusu ardhi na madai ya madaktari, wanafunzi, walimu na makundi mengine ya kijamii, kunatishia ustawi wa nchi, huku serikali ikiendelea kushughulikia matokeo badala ya vyanzo vya migogoro. "Serikali haielekei kuchukua hatua za haraka kunusuru uchumi wa nchi, kuongeza uzalishaji na ajira na kudhibiti mfumko wa bei na ongezeko la gharama za maisha kwa wananchi hali ambayo ni kinyume na ahadi ya CCM na Rais Kikwete ya maisha bora kwa kila Mtanzania na ni tishio kwa usalama wa nchi.

  "Hatua kamili hazijachukuliwa na serikali na CCM kuhusu kuwawajibisha watuhumiwa mbalimbali wa ufisadi na kushughulikia udhaifu wa kiutendaji katika serikali na chama tawala pamoja na kutetereka kwa utawala wa sheria," imesema sehemu ya taarifa ya CHADEMA.
  Ili kuinusuru nchi, chama hicho pinzani kimemtaka Kikwete kuziba ombwe la uongozi lililopo na kufanya mabadiliko ya msingi na ya haraka ndani ya serikali katika kipindi hiki.

  Aidha Kamati Kuu imeielekeza kambi rasmi ya upinzani inayoongozwa na CHADEMA kuisimamia kwa karibu serikali kupitia mkutano wa saba wa Bunge unaotarajiwa kuanza Aprili 10 na kuwasilisha taarifa kwenye mkutano ujao wa Baraza Kuu la chama kwa ajili ya hatua zaidi iwapo mabadiliko ya msingi hayatafanyika kwa njia za kawaida za kibunge na kiserikali.


  Kuhusiana na tuhuma za matumizi mabaya ya rasilimali za serikali, CHADEMA imelaani vikali hatua ya Rais Kikwete na Makamu wake, Dk. Bilal, kutumia mali za serikali kinyume na utaratibu.

  Kikifafanua, chama hicho, kimesema kuwa Rais, makamu wake na baadhi ya viongozi wakuu wa serikali wamekuwa wakitumia rasilimali za umma kufanya kazi za kisiasa za Chama cha Mapinduzi.

  "Kamati Kuu imeamua kukemea tabia inayoanza kushamiri ya viongozi wakuu wa serikali, wakiwemo Rais na Makamu wa Rais, kuchanganya shughuli za kiserikali na kazi za kisiasa za Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kutumia rasilimali za umma," kimesema chama hicho.
   
 2. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli CDM wanajitahidi sana na haya matamko yao. Lakini mbona kama hayabadilishi utendaji wa hii serikali? Nadhani kuna haja ya kwenda mbele zaidi ya matamko na kuchukua hatua. Serikali wameshajua kile ambacho CDM inakiogopa na ndio maana wanaendelea na huu utamaduni wao. Kuna msemo unasema, "you can discover what your enemy fears most by observing the means he uses to frighten you" by Eric Hoffer.
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tupe source ya taarifa yako usitoe tamko wewe kama ulivyofikiria kichwani mwako. Mbona yote uliyoyasema hapo yanasababishwa na CHADEMA wenyewe kama migomo si wao ndo washawishi wakubwa? Maisha magumu wao ni chanzo kama wanaweza kwenda kuwachangisha wananchi fedha za kampeni wakati wanapewa ruzuku si kuwanyang'anya hata kidogo walichonacho na hivyo kufanya maisha yazidi kuwa magumu.
   
 4. k

  kastarehe JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ee Mola tusaidie watu kama hawa wawe waelewa!! Hivi kweli kuna mwenye akili timamu atakayepingana na ujumbe huo au wewe ni TISS!!!?
   
Loading...