Dr Matola PhD
Platinum Member
- Oct 18, 2010
- 61,429
- 108,583
mbona heading na habari haviendani? kwa nini usingeandika ukawa wapiga gori la kisigino?
Muungano wa kinafki sana huu
Ongea taratibu usimsababishie Wassira na Mwigulu kupata SHINIKIZO LA DAMU.
Huu Muungano wa mabua kwenye Bajaji ya barafu hauwezi kupita kwenye Moto mkali.
Natarajia mipasho na anguko lao hivi punde....puuu!
Hoja ya ukanda, udini na ukabila zapeperuka. Sasa naona wameanza ya kitoto ya ugaidi leo. Imejibiwa kitaalam hapa jf ikaonekana ya kitoto kabisa. Nape atapata shinikizo, nimemsikia akiulizwa swali wapo fm, jamaa amechanganyikiwa kabisa anasema " mkiona Ukawa wapigeni mawe" mwandishi akabaki kucheka! aaaah aaah aaaah aaah!!!!
ishu itakuwa kwenye nafasi ya kugombea urais mwakani... Lipumba vs padri slaa.... Je, cuf watakubali mgombea wao wa urais awe padri?..je, chadema watakubali mgombea wao wa urais awe muislamu? Ukawa itasambaratika mapema sana?
Huu Muungano wa mabua kwenye Bajaji ya barafu hauwezi kupita kwenye Moto mkali.
Natarajia mipasho na anguko lao hivi punde....puuu!
Mleta mada ni kama hauna uzoefu na siasa za Tanzania... hii si mara ya kwanza upinzani kutangaza kuungana! Assume leo hii Jimbo la Temeke linakuwa wazi, ambako CUF na CHADEMA wote wana nguvu za kutosha... hapatatokea kati yao wa kumwachia mwenzako... kila mmoja atataka ku-test zari! Lakini ikitokea jimbo X huko ZNZ lipo wazi, CHADEMA watajifanya kuwaunga mkono CUF coz' wanafahamu wao hawana chao visiwani... na ikiwa Jimbo linabaki wazi say, Arusha, CUF watajifanya kuwaunga mkono CHADEMA coz' wanafahamu CUF Arusha hawana chao... hamna kitu hapo!
Kuhusu influence ya CHADEMA... watu wengi kama sio wote wanapiga hesabu zao vibaya... wengi wanaamini umoja wa UKAWA utainufaisha CHADEMA lakini msingi, watakaofaidika na UKAWA ni CUF na NCCR! CUF anazo nguvu za kutosha kule ZNZ, hususani Pemba... kule Pemba walianza kuikataa ASP, wakaja kuikataa CCM... si rahisi hata kidogo ama kwa CHADEMA au NCCR kupata nguvu kule Pemba/ZNZ hata kama UKAWA wanapiga kambi ZNZ/Pemba mwaka mzima... wapemba huwaambiwi kitu Kuna wakati NCCR waliwahi kuifitini CUF kule Pemba, walichoambulia ni aibu pamoja na kupeleka mabati ya msaada ktk harakati zao za kutaka kuungwa mkono na Wapemba!!
Kwa upande mwingine, movement za UKAWA huku bara zitasaidia sana kuifufua CUF na NCCR! Ingawaje CUF imejisimika zaidi ZNZ lakini huku Bara, angalau mikoa ya Pwani walikuwa na ushawishi ambao ulianza kupungua... UKAWA itawa-boost... na hili ndivyo kwa NCCR! Tukija upande wa CHADEMA, tayari walishakuwa na ufuasi wa kutosha huku bara lakini hapa kati kati CHADEMA wamewazingua wengi! Wapo waliokuwa mashabiki wa CHADEMA lakini wakaamua kukaa pembeni baada ya kuona migogoro isiyoisha ya uongozi! Hawa ni wale ambao hawaamini katika CCM lakini kwavile chama pekee walichokuwa wanakitegemea (CHADEMA) kiliwazingua, wakaamua kukaa kando! UKAWA, itawazindua tena watu hawa... na kv hawana tena imani na CHADEMA, si ajabu wengi wakakimbilia nccr au hata CUF! Trust me, ingawaje watu wanadhani CUF wanacheza ngoma wasiyoijua, lakini ni CHADEMA ndio wanacheza ngoma wasioijua!
c.c:JokaKuu, Yericko Nyerere
Ongea taratibu usimsababishie Wassira na Mwigulu kupata SHINIKIZO LA DAMU.
Dawa ya kusambaratisha ukawa ipo jikoni. Unadhani sisiemu itakaa kumya? Itacheza karata zote kuhakikisha wanasambaratika!Biblia inasema " nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu" . UKAWA OYEEEEE!, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Nahis kama natamani hivi kutaka kukuunga mkono kwa 100%... ila kama ndivyo maoni yako ndo haya kwanini uliacha kuniunga mkono wakati napigia upatu suala la what's so called "Good Governance" ambayo ingawaje ni mfumo wenye jina tamu na la kuvutia lakini kimsingi ni mfumo unaotumika kama kichaka cha mafisadi na viongozi wazembe... mfumo unaoshadidia utawala wa sheria, yaani utawala wa sheria utoke kwa mafisadi na wazembe... what a ----! Nasi kama mazuzu tumekuwa tukishadadia kwa mbwembwe na vifijo bila kujiuliza ni kwanini leo viongozi wa Afrika ambao kwa miongo kadhaa wamekuwa wakipinga mifumo inayoletwa na watu wa magharibi, hivi sasa viongozi wetu wanaunga mkono mfumo wa utawala bora walioletewa na hao hao watu wa magharibi... hatutaki kujiuliza, WHY? Kumbe jibu ni simple, wanaushabikia mfumo huu coz' kichaka cha uovu wao... huwezi kuwafanya chochote coz' ni mfumo unaozingatia utawala wa sheria... whereas, a person atabaki mtuhumiwa hadi ithibitike beyond reasonable doubt kwamba ametenda kosa analotuhumiwa! Kama si utawala wa kijeshi kama unavyopendekeza basi tu-replace Approved Dictatorship Governance with Good Governance!..kwanza, sitaki kabisa kuisikia CCM.
..pili, baada ya kusikia toka kwa waziri Lukuvi kwamba gharama za kumtumza Raisi ni sawa na bajeti ya mikoa mitano, nikaona suluhisho hapa ni kutawaliwa kijeshi tu.
..hii nchi imeoza tunapaswa kuanza upya. bora waje hao maafande wasafishe uoza huu kabla ya kuruhusu tena siasa za vyama nchi hii.
..kwa hiyo mimi nimeshatoka ktk siasa zenu za vyama.
Muungano wa kinafki sana huu