CHADEMA, Walimu mburuzeni kortini Mwigulu Nchemba

 
Hakuna haja ya kwenda mahakamani maana kupata haki kunahitaji muujiza. Labda aje mtume na maswahaba wake!!?
Nawashauri waalimu wafanye maamuzi magumu. Wagome kufanya kazi za uchaguzi tena kwa kuanzia waanzd na uchaguzi wa madiwani Arusha! Halafu wawaadabishe ccm kwa kuipigia debe cdm na kwenda kuipigia kura. Huyo Mchamba Miguu atawaomba radhi mwenyewe!
Kuhusu cdm, hakuna haja ya kumshtaki huyo jamaa. Hana lolote kwa cdm. Kama kuna anayebisha basi amshauri aje Ar kuwanadi madiwani. Igunga ametokea kwenyf chaki alafu mnampa sifa za kijinga. Maambieni wavue gamba lingine wauone moto!
Kwangu mimi huyo jamaa hastahili sifa. Amepeleka green guide wamekwenda kuteka na kunyanyasa watu akasingizia ni Mungiki na Makomandoo wa cdm, amesababisha watu wameogopa kwenda kupiga kura. Wamemtumia dc kupata kura za waislamu, leo tumsifu kwa lipi? Amebahatika tu kwa kuwa Igunga hawajaamka vya kutosha. Hapo ndio mwisho. Wavue gamba lingine waone.
Uvccm walikuwa jana Arusha. Ungewaona ungefikiri ni chama cha updp! Aibu tupu!?
 

What? anataka kuja mwanza? jijini au kijiji kinachoitwa mwanza ya madaso kilichopo wilayani bukombe mkoani shinyanga?kama ni mwanza jijini mshauri mapema asitie mguu wake, aibu aliyoipata bosi wake nape kule serengeti hapa mwanza itakuwa mara tirion kadhaa, kama anakuja kufanya vikao vyao vya ndani kama alivyo fanya nape hapa juzi kati is fine, ila asithubutu kulitenga pale uwanja wa furahisha au popote pale jijini mwanza, atakachokiambulia wewe mwenyewe utashuhudia, mwanza magamba hawana chao mkuu na wala hakuna matumaini ya kuwa nacho cku zijazo.
 

Nimeipenda avatar yako.
Teh teh Teh
 
Huyo Mwigulu inafaa akatafutiwa namnaya kuzima porojo zake!!!!!! Ila hapa ATown sijui ila macharii hawadanganyiki, tena achunge sana watamtoa baruu!!!!!!!!
 
Hilo swala likipelekwa mahakamani watakaoumia ni walimu waliowagawia watu karatasi zimetikiwa kashindye na hawa watu walikamatwa na msimamizi mmoja alitolewa igurubi, kama swala ni hilo tuwe makini mimi sijipendekezi bali nasema kama nilivyosema mwanzo hata ukarudia mara mia na uka bold kama mwigulu sivyo alivyo haisaidii. Sisi tuko Igunga swala la kufumaniwa niliwambia halituongezei kura kwani halina ukweli na hata mazingira hayaoneshi uking'ang'ania chupi chupi unajiridhisha mwenyewe tu
 
Ni kweli salimia, mwigulu ameinyima ushindi cdm. Kajama kalibadilisha watu na kalitumia mbinu zote, hakajulikani kasukuma si kasukuma, kanyiramba si kanyaturu yaani balaa tu. Huyu jamaa anayesema mwanza hapati mtu labda hamjui mwigulu, ni kosa kubwa kumsikiliza mwigulu, na hilo ndio kosa walilofanya igunga. Angalia mpaka diwani aliamua kubwaga manyanga urugha kule iramba akaenda slaa na zito lakini walipoongea watu wakasema hawajamfikia mwigulu hata nusu ya hotuba. Ngoja aje mwanza then uwasikilize watu kishatoka mkutanoni
 
Akipewa jukumu la A town kazi itakwepo kwa cdm, tena kata nne tu. Yaani huyo jamaa kuna kata moja nyandukwa au nyandekwa walimuzomea nusura wampige cdm wala hakuwakimbia alichofanya wote waliokuwa wakali akakutana nao usiku kesho yake wote wlivaa kijani na pale ccm ikashinda. Kwa kuwa yuopo subirin mtamwona
 

wambie magamba wenzako upuuzi huo!yani unachosema hakina uhusiano na mada!mpe nanihii yako ili ainanihii...mlizoea walimu kuwaibieni kura sasa hivi walimu hawagangi njaa wanataka ukombozi wa kweli!
 

Akiripoti kutoka MAGAMBA ni yule yule GAMBA WA MAGAMBA...!
 
Mwigulu hana hatari yoyote kwa Chadema wala hakuna anatishika nae labda tu nikukumbushe mwigulu huyu anaishi ndani ya zizi kubwa la mafisadi na hivyo nae ni fisadi tena hana nguvu unazomsifia nazo,mwanza anakokwenda unavyosema kumbuka mwanza ni jiji la chadema,mwambie aende haraka na tunakuomba uende nae wewe mopao mokonzi unaemsifia na kutaka kututisha,kwani humu uswahili kuna watu wangapi wanajua kutusi na kuongea vichekesho kiasi kwamba watu wakiwa kwenye kahawa huendelea kumnunulia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…