Ilongailunga
JF-Expert Member
- Jan 18, 2012
- 1,388
- 896
Kama CHADEMA inataka kuwa sawa na CUF na ijaribu kumkaribisha EL ambaye amejaa tuhuma kila kona ya vyombo vya habari na midomoni mwa watz, CHADEMA itajiua yenyewe na kama mpango ndo hou wa kuanza kubeep tension ya wapenzi wa CDM hapa sio.
Hapa ndipo Chadema wataanza kukoroga RASMI, hafai hata kugombea ubalozi wa Nyumba kumi kumi chadema, anaweza waibia wananchi Mahindi yao, mwizi ni mwizi tu.
Kwanza kabisa naomba niwarejeshe kwenye kaulimbiu ya JF, inasema, "The Home of Great Thinkers". Ukweli niliougundua ni kwamba tuna wana JF wengi sana humu ambao si great thinkers. Naomba nizungumzie mambo mawili tu:
Kwanza tunachofanya humu ndani ni kisa tulichosimuliwa zamani kwamba baba mmoja alikutwa na mkewe akinoa panga. Mke akamuuliza unanoa panga la nini, yeye akajibu hivi: "Ninanoa hili panga ili nikafyeke shamba halafu nilime pamba nikivuna na kuiuza nitanunua ng'ombe wawili: mweusi na mweupe. Yule mweusi hata wewe unaweza kumkamua lakini mweupe nitakuwa namkamua mimi tu". Mke akasema haiwezekani mweuupe umkamue peke yako. Hata mimi nitakuwa namkamua. Mme akasema haiwezekani umkamue ng'ombe wangu. Wakabishana mpaka wakapigana. Ndicho ninachokiona humu ndani. Watu wanatoa macho kiasi kwamba baadhi wangekuwa karibu yule aliyemtukana eti Tuntemeke Mwigamba aondoke atuachie chama, labda angeweza hata kumpiga. Tunatoleana macho utadhani Lowassa katangaza kuingia CDM na sasa tunabishana ama tumpokee ama tuache. Kumbe inawezekana jamaa hana hata mpango huo!
Jambo la pili naomba tusome tena hii nukuu hapa kama Mwandishi wa gazeti alivyomnukuu Mwigamba:
"Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama,"
Kama mmesoma hayo maneno ya Mwigamba between lines, hamna sababu ya kumshambulia kiasi hicho. Hajasema kwamba leo hii inaweza kutokea tu EL akaja akaomba kuingia CDM na yeye kama mwenyekiti wa mkoa akampokea. Amesema lazima aeleze sababu za kufanya hivyo na akatumia neno la wingi "na sisi" ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama. Maneno yake yanaonyesha collective responsibility kwamba watakuwa jopo la viongozi. Watamuuliza kwamba unataka kuja CHADEMA lakini una tuhuma hizi na hizi. Wakiridhika na maelezo yake ndo wataamua kama viongozi si yeye kama mwenyekiti wa mkoa. Naomba niwaulize swali mnaotumia msuli mkubwa kupinga EL kuja CDM kwa vyovyote vile. Hivi akija na uthibitisho kwamba madudu yote yamefanywa na Mkapa na Kikwete. Yeye kafanywa mbuzi wa kafara kwa ajili ya kuiokoa serikali isidondoke kama alivyofanyiwa gavana wa zamani wa benki kuu Daudi Ballali, hivi akaja na ushahidi wa kile alichokitamka Mwakyembe kwamba kuna vitu walificha ili serikali isidondoke na vitu hivyo kumbe EL akafanikiwa kuonyesha kwamba ni ushahidi kwamba ufisadi wote wa Richmond ni wa JK na si wa kwake Lowassa. Hivi akija akakiri na kutubu kwa kuonyesha ushahidi wa baadhi ya vitu alivyovifanya kwa kulazimishwa na system kwa ajili ya chama na akavijutia na kuviungama na kuwaomba radhi wananchi, akasema ametoa maisha yake kama serikali itamuua kama ilivyommaliza Ballali yuko tayari ili mradi ukweli wote uwe hadharani, hivi mtakataa kumpokea awe mwanachama wa CHADEMA. Try to use your bongos badala ya kutumia misuli kupinga kila kitu kwa ushabiki.
uttoh hivi gamba ni Lowassa? au gamba ni system? kama gamba ni Lowassa then Lowassa akitoka CCM wote mimi na wewe turudi CCM is that Ok? Lowassa katoka madarakani tangu 2008 je ufisadi umeisha serikalini? Je, haya mdudu yanayopigiwa kelele bungeni leo yamesababishwa na Lowassa?Feedback, mda huu tupo kikazi zaidi,kuliondoa GAMBA CCM, na sio KULIVUA, maana lote ni GAMBA! sidhani kama tuna mda kweli wa kulijadili ni jinsi GANI lilikuwa GAMBA KAKA? ila kama walipenda GAMBA nisikukatishe tamaa, endelea nalo
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Arusha, Samson Mwigamba, amesema kuwa yeye yuko tayari kumpokea hata Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, endapo ataamua kufanya uamuzi wa kubadilika na kujiunga na CHADEMA.
Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama, alisema.
Source: Tanzania Daima
My take: Nimeanza kuamini kuwa inawezekana kabisa Lowassa anaandaliwa mazingira ya kusafishwa.

swala la utajiri hata mbowe,mtei,ndesa ambao ni mizizi ya cdm ni matajiri wakubwa pia, kwa hiyo utajiri sio kigezo
Thanks Maskini MkulimaKwanza kabisa naomba niwarejeshe kwenye kaulimbiu ya JF, inasema, "The Home of Great Thinkers". Ukweli niliougundua ni kwamba tuna wana JF wengi sana humu ambao si great thinkers. Naomba nizungumzie mambo mawili tu:
Kwanza tunachofanya humu ndani ni kisa tulichosimuliwa zamani kwamba baba mmoja alikutwa na mkewe akinoa panga. Mke akamuuliza unanoa panga la nini, yeye akajibu hivi: "Ninanoa hili panga ili nikafyeke shamba halafu nilime pamba nikivuna na kuiuza nitanunua ng'ombe wawili: mweusi na mweupe. Yule mweusi hata wewe unaweza kumkamua lakini mweupe nitakuwa namkamua mimi tu". Mke akasema haiwezekani mweuupe umkamue peke yako. Hata mimi nitakuwa namkamua. Mme akasema haiwezekani umkamue ng'ombe wangu. Wakabishana mpaka wakapigana. Ndicho ninachokiona humu ndani. Watu wanatoa macho kiasi kwamba baadhi wangekuwa karibu yule aliyemtukana eti Tuntemeke Mwigamba aondoke atuachie chama, labda angeweza hata kumpiga. Tunatoleana macho utadhani Lowassa katangaza kuingia CDM na sasa tunabishana ama tumpokee ama tuache. Kumbe inawezekana jamaa hana hata mpango huo!
Jambo la pili naomba tusome tena hii nukuu hapa kama Mwandishi wa gazeti alivyomnukuu Mwigamba:
Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama,
Kama mmesoma hayo maneno ya Mwigamba between lines, hamna sababu ya kumshambulia kiasi hicho. Hajasema kwamba leo hii inaweza kutokea tu EL akaja akaomba kuingia CDM na yeye kama mwenyekiti wa mkoa akampokea. Amesema lazima aeleze sababu za kufanya hivyo na akatumia neno la wingi "na sisi" ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama. Maneno yake yanaonyesha collective responsibility kwamba watakuwa jopo la viongozi. Watamuuliza kwamba unataka kuja CHADEMA lakini una tuhuma hizi na hizi. Wakiridhika na maelezo yake ndo wataamua kama viongozi si yeye kama mwenyekiti wa mkoa. Naomba niwaulize swali mnaotumia msuli mkubwa kupinga EL kuja CDM kwa vyovyote vile. Hivi akija na uthibitisho kwamba madudu yote yamefanywa na Mkapa na Kikwete. Yeye kafanywa mbuzi wa kafara kwa ajili ya kuiokoa serikali isidondoke kama alivyofanyiwa gavana wa zamani wa benki kuu Daudi Ballali, hivi akaja na ushahidi wa kile alichokitamka Mwakyembe kwamba kuna vitu walificha ili serikali isidondoke na vitu hivyo kumbe EL akafanikiwa kuonyesha kwamba ni ushahidi kwamba ufisadi wote wa Richmond ni wa JK na si wa kwake Lowassa. Hivi akija akakiri na kutubu kwa kuonyesha ushahidi wa baadhi ya vitu alivyovifanya kwa kulazimishwa na system kwa ajili ya chama na akavijutia na kuviungama na kuwaomba radhi wananchi, akasema ametoa maisha yake kama serikali itamuua kama ilivyommaliza Ballali yuko tayari ili mradi ukweli wote uwe hadharani, hivi mtakataa kumpokea awe mwanachama wa CHADEMA. Try to use your bongos badala ya kutumia misuli kupinga kila kitu kwa ushabiki.
Hapa ndipo Chadema wataanza kukoroga RASMI, hafai hata kugombea ubalozi wa Nyumba kumi kumi chadema, anaweza waibia wananchi Mahindi yao, mwizi ni mwizi tu.
Lowassa akitubu madhambi yake tumkaribishe chadema, kwani binadamu hasamehewi?
Sidhani Lowasa kama ni mchafu sana kiasi hicho kama tunavyotaka kuaminishwa, kwangu mimi kosa kubwa la Lowasa ambalo namhukumu nalo, ni kwakuwa alishiriki kwa kiasi kikubwa katika mipango ya kumweka Kikwete madarakani na huku akichafua wengine kupitia mtandao wao walioubuni enzi hizo, na Sitta akiwemo. Kuhusu suala la Richmond, jamani ifike mahali sasa na EL naye aseme hadharani Richmond alihusika vipi. M/kiti wa kikao cha baraza la Mawaziri ni Rais, sasa kuendelea kukaa kimya kwa EL ndiyo ataendelea kujichimbia kaburi. Ok ametubu kama Mwigamba alivyosema na viongozi wakapima akaja CDM na akawa mwanachama wa kawaida, je akataliwe? na wote mnaomhukumu kiasi hicho kila mtu ajitazame ni msafi kiasi gani. Kwetu sisi wakristo Biblia inatuambia kuwa hata yule mwana mpotevu baada ya kutapanya mali za baba yake, akagundua kosa, akajuta, akarudi kwa baba yake, je baba yake si alimpokea?
Viongozi wa CHADEMA kama mnataka KUZOMEWA NA KUPIGWA MAWE kila mtakapoonekana, mkarisheni Lowasa!! Watanzania wengi tutajua hata nyinyi ni wachumia tumbo!! Na kama mna mpango wa kumkaribisha Lowasa tafadhali tuambieni mapema tujue mbinu mbadala na mturudishie vijimiamia vyetu maana pesa ya Mungu haichangamani na pesa ya shetani kamwe!!!