CHADEMA Wajisahihishe ili washinde Arumeru Mashariki.

mwankuga

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
334
120
[h=6]CHADEMA WAJISAHIHISHE.

Ni vita tena kati ya CHADEMA na CCM.Safari hii ni uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Arumeru Mashariki.Ni vita kati ya Siyoi Sumari (CCM) na Joshua Nassari (CDM).Ni vita kati ya vijana.Ni vita kati ya status quo na mabadiliko (changes).

Kama ingekuwa matakwa yangu,ningependa kijana na rafiki yangu Joshua Nassari ashinde.Sababu ni moja tu.Ni kijana nayependa mabadiliko.Ni kijana Mwanaharakati wa kweli mwenye kudhubutu.Namfahamu vizuri Nassari.Tumekuwa wote pale UDSM kwa miaka 3.Lakini kwa bahati mbaya sana,huyu Siyoi Sumari simfahamu.Lakini chama chake nakifahamu vyema.

Kwa rekodi nilizonazo,CHADEMA wamewahi kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge,jimbo la Tarime (2008).Na chaguzi zote CHADEMA wanaonyesha ushindani mkubwa sana.CHADEMA wamekuwa wakifanya makosa ambayo yamekuwa yakiwagharimu sana.Kama makosa haya watayasahihisha basi ni dhahiri kwamba Arumeru Mashariki watashinda.Makosa hayo ni kama ifuatavyo;

(a) Kutoanzisha matawi ya wanachama huko vijijini.
Hapa hakuna ubishi kwamba CCM inashinda chaguzi nyingi kwa sababu ya watu waishio vijijini ambako ndiko kuna wapiga kura wengi.Najua kuna baadhi ya maeneo ya vijijini ambako Chadema wapo,lakini kwa kiasi kikubwa Chadema kimekuwa cha watu wa mjini.Ni vema CHADEMA kikajiimarisha zaidi vijijini.

(b) Kusubiri Uchaguzi.
Uchaguzi mmoja unapoisha,huandaa uchaguzi mwingine.Chama lazima kiwe kinafanya maandalizi kwa kutoa elimu ya uraia,kueleza itikati na falsafa ya chama kwa wananchi.Harakati hizo zinategemea sana,uimara wa chama katika ngazi ya kijiji,kata,wilaya,na mkoa.Wananchi wa Tanzania wanahitaji kukumbushwa mara kwa mara.

(c) Usimamizi wa Upigaji wa Kura.
Kwa muda mrefu sana kumekuwepo na tuhuma kwamba CCM wanaiba kura.Na mara kadhaa baada ya kushindwa uchaguzi madai yanakuwa ni uchakachuzi wa kura.Ifike mahala kama ni kweli CCM wanaiba kura,CHADEMA na vyama vingine vya siasa kulipatia ufumbuzi suala hilo.

(d) Uwepo wa Mawakala.
Mawakala ndio hushuhudia zoezi la kuhesabu kura,hivyo ukiwaweka mawakala "njaa" ujue umeliwa.Kwa kuwa MAWAKALA wa vyama vya upinzani wanategemea sana upenzi wao wa chama na mabadiliko,ni vema zoezi la kuwapata mawakala likafanyika wa umakini mkubwa sana.Kwanza mawakala sharti watoke eneo husika,lakini ikishindikana kabisa basi vetting ya nguvu/makini ifanyike.

(e) Mamluki katika Chama.
Kati ya hatari ya vyama vya upinzani ni watu mamluki.Vyama vya upinzani visiwe jalala la watu wanaosaka madaraka kwa nguzu zote.Kuna wale wanaohama kutoka vyama vingine au CCM na kuhamia CHADMEA,hawa lazima waangaliwe kwa jicho la pekee sana.Mfano,ni mgombea mmoja aliyeshindwa kwenye kura za maoni CCM huko Arumeru Mashariki,akakimbilia CHADEMA na akachukua fomu ya kugombea ubunge kupitia CHADEMA.Huyu ni mroho wa madaraka na sidhani kama anamini itikati na falsafa ya CDM.

(f) Uhamasishaji wananchi kujitokeza kupiga kura.
Moja kati ya vitu ambavyo vinawanyima ushindi CDM ni wananchi wachache kujitokeza kupiga kura hasa vijana.Wakati wa kampeni watu wengi sana hujazana kwenye mikutano ya CDM ,lakini mwisho wa siku wengi hawajitokezi kupiga kura.Pamoja na kampeni za majukwani,ni vema CHADEMA ikashuka chini na kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu ili waweze kujitokeza kupiga kura.Vijana ambao wanaonekana wanapenda sana mabadiliko,basi waelimishwe umuhimu wa kupiga kura.

(g) Kulinda kura.
CCM ni chama kizoefu sana katika kufanya rafu katika uchaguzi.CHADEMA bila kulifanyia kazi suala hili,wanaweza kutoka kapa tena huko Arumeru Masharik.Demokrasia ni gharama sana,CHADEMA na watanzania wote lazima wakubali gharama hizo.Katika uchaguzi mkuu uliopita,wabunge wa CHADEMA walishinda kwa sababu ya nguvu ya umma.Wananchi waliamua kulinda kura kwa gharama yoyote.Mfano ni Mbeya Mjini,Mbozi Magharibi,Ilemela,Nyamagana,Arusha Mjini,Iringa Mjini n.k.
[/h]
 
CHADEMA WAJISAHIHISHE.

(h) CDM waanze kuiba kura kama CCM
 
jana tu walionekana kupwaya,hotuba zao hazna mashiko,huyo nasari ndo bado kabsa kwnye kujieleza,kaz kwl kwl,yan cdm bwana..........!
 
Nashauri pia kuweka nguvu zaidi kwa wanawake na wazee. Aidha mkakati maalum uwekwe kuwatumia vijana wa kiume kuwashawishi wake , wapenzi na dada zao kukiunga mkono na kukichagua cdm. Wanawake ni mtaji mkubwa!
 
Back
Top Bottom