Chadema waishiwa sera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema waishiwa sera

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tata mura, Oct 11, 2012.

 1. t

  tata mura JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 27, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndungu wana Jr. nashangazwa sana na sera ya Chadema na mwendelezo wake hadi sasa wamepoteza mwelekeo. Awali ya yote huwa nawambia Chama hiki kipo after maslahi ya wachache, baada ya kugunduwa Ndg; Godbless Lema ameshindwa kwenye kesi aliyokata rufaa sasa mawazo yao yote yamehamia Arusha. Jiulize ni kwa nini ARUSHA na si kwingineko? sababu kubwa Arusha watalii wanaingia wengi hivyo kipato kipo, pamoja na wavuta ............... wa machimbo wapo kwa wingi. Mbona Tanga baada ya kutishwa na kijana wa Makamba wamekuwa kimya au hawakusikia alicho sema?

  Nauliza tu hivi vyama vingine havina mpango wa Uchaguzi ndani ya vyama vyao? kwani kila kukicha CCM imekuwa hivi !!!!!!!!!, au ndo kusema waliopo hakuna wakuwatoa?

  Cha ajabu sana Chadema wamefuata nyayo ya CCM kwa kutumia mtandao wa sms kutumia watu ujumbe hata wasiowahusu.(( Nanukuu ujumbe niliotumiwa hivi punde; HATARI! Angalia, watoto wa vigogo waliopita UVCCM ngazi ya taifa DICKSON MEMBE, FRED LOWASA, RIDHIWANI KIKWETE, ASHURA HUSSEIN MWINYI, BENY SAMWEL SITA, DEBORA MWANDOSYA, IREN PINDA, FELSTER NDUGAI, CHRISTOFER NDEJEMBI, SHARIFER BILALY, HAWA KIGODA, JUDITH MUKAMA NA JALOME MSEKWA. Nchi hii imekwisha. Inatia hasira, wacha watoto wa maskini tupambane kupitia mlango mwingine ''CHADEMA'' ili kutete maskini wenzetu, wazazi na watoto zetu! Vita Hii Inaanza Sasa! Upatapo meseji hii , tuma kwa WAZALENDO wenzako 5 )) Mwisho wa kunukuu.

  Je CHADEMA kuna ngugu wa viongozi wangapi hadi sasa au ndo huwa sielewi tena ngazi kubwa kabisa? Mfano Dr. Slaa Mkewe mtelekezwa ni Mb wa kuteuliwa, ambapo mteuaji mkubwa ni Dr. Slaa mwenyewe, Wakili maarufu wa kuongea sana na Mwanasheria Mkuu mtarajiwa Dada yake naye ni Mb wa kuteuliwa. Wapo wengi sana lakini vyanini wakati wote wanashibisha matumbo yao kwa kutumia udhaifu huu wa kuto kufikilia mbali, na kutegemea mawazo dhaifu kama haya.

  Chadema kimekuwa kinavuta watu kwa nguvu kuingia kwenye Chama, bila kujua madhara yake makubwa ya baadae, Mfano Kiongo anasimama anasema VUA GAMBA VAA GWANDA. Fikilia huyu unayemvuta aliko sasa unamponda je akija huku utamwosha na Omo ili atakate ama atakuja kuendeleza ufisadi?


  Nawasilisha TUUNGANE KUJENGA NCHI SIYO KUBOMOA
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Bora kutokuwa na sera kuliko kuwa na sera za kuwaibia na kuwatia umasikini wananchi, kuwauwa wananchi wasio hatia, sera ya omba omba nchi za nje wakati tumejaliwa na rasilimali kibao, na sera ya kuhonga wakati wa uchaguzi.

  Kwa kweli ni bora kutokuwa na sera kuliko kuwa na sera za namna hiyo, zinazoashiria vita vya wenyewe kwa wenyewe.
   
 3. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,771
  Likes Received: 8,038
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unataka Mwana Mtoka Pabaya nikusaidiaje?

  Mi naona povu tu. Hivi msg zooote unazopokea nyingine za sex, nyingine vichekesho n.k zinajulikana huwa zimetungwa na nani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Waache magamba hayo -- yanaweweseka kwa kitu kinachoendelea sasa hivi nchi nzima kiitwacho M4C a.k.a. 'TWANGA KOTE KOTE.' Wana woga mkubwa wa chaguzi ndogo zijazo, za madiwani na ubunge wa sumbawanga na Igunga.
   
 5. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sasa mikutano yao yote vikapu ndo vingi kuliko watu na Lema ndo mfuatiliaji wa hivyo vikapu mpaka anakosa muda wa kuwahutubia wananchi chezea chd wewe.
   
 6. m

  malaka JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Vipi kale kaujumbe kenu ka CDM ni chama cha fujo hukuwahi kukapata nini?
   
 7. y

  yaya JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, nasikitika kupoteza muda wangu kusoma kitu kisicho na mpangilio kama hiki.
  Ulichokiandika (ambacho kwa hakika hakina utafiti wowote), kilitakiwa kuandikwa na mtoto nadhani wa darasa la tano ambaye anaanza kufunzwa namna ya kuandika insha.

  Kwa hakika hakikutakiwa kwa mpangilio huu, kuandikwa na mtu ambaye anajiita au angependa kujumuishwa katika kundi la GTs.
  Najua utachukia lakini ndio ukweli halisi, pole sana.
   
 8. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huajongea kitu bali utumbo mtupu. Kama siyo CCM basi una akili mbovu kama wao. Lau ungenyimazia au huo muda ukautumia kujifunza kufikiri badala ya kujipayukia mwanangu. Ni vizuri kuficha ujuha wako.
   
 9. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wewe naona shule yako ina mashaka, naona haujui maana ya neno sera(policies) umeshindwa kuonesha hao chadema wameishiwaje na hizo unazoziita sera, na kuhusu hiyo msg una uhakika kwamba ni chadema ndiyo wamezituma? mbona siyo CUF, NCCR AU ADC au ccm wenyewe? kajipange mkuu acha kukurupuka, yaani mkisikia CDM tu basi mnaporomosha matusi, kazi mnayo
   
 10. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  matatizo ya ku2mia masaburi kufikiri!
   
 11. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ccm at work, binafsi cjaona point zaidi ya mbwembwe na majigambo tu!
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Kumbe umeshajua hukumu ya Lema!

  Thibitisha huo ujumbe umetumwa na cdm!
   
 13. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  1. Aliyeishiwa ni wewe na hiyo CCM yako
   
 14. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Kama Chadema wameishiwa sera nilisafiri kutoka Arusha mpaka Dodoma bendera za Ccm unaweza pita mkoa mzima ujaona bendera ya Ccm chezea Chadema zippo kila mahali
   
 15. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
   
 16. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wana JF,
  Chadema wanapaswa kufahamu kuwa siasa ipo na itaendelea kuwepo lakini kinachohitajika ni kuindesha kwa ustaarabu na amani na katika maeneo stahiki.

  Chadema mnawasumbuwa wakazi wa Arusha na siasa zenu watu wanashindwa kufanya kazi zao kila siku maandamano yasiyoisha na mikutano ya Lema, Chadema ebu acheni ulimbukeni wa kisiasa, vitendo vyenu vya kukusanyika ovyo na kusukuma gari la Lema kuzunguka mji mzima kuwatia hofu wananchi pamoja na wageni (Watalii) na wewekezaji pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo wa Jila la Arusha.

  Mji wa Arusha saizi umedumaa kibiashara watu wanaukimbia wanaogopa fujo za Chadema, katika hali ya kawaida Chadema wameudumaza mji wa Arusha
   
 17. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  ??????????????????????
   
 18. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Vipi mkeo hapati wateja?Wewe vipi ulitaka wateja?Nenda zanzibar kuna biashara nzuri sana wewe na mkeo mtapata wateja wengi sana...Masaburi yanawashawasha?Nenda zenji kawashwewashwe..wakunekune
   
 20. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Niliandika haya nitapigwa madongo

  Kurekebishana: Lema badilika
  Mimi ni kijana ambaye kwa sasa nina makazi nje ya nchi lakini ni kijana niliyekulia Arusha. Nilipoenda Arusha mwezi wa tatu kuna vitu ambavyo sijafurahia. Kwanza ni kile kitendo cha Lema kuwaambia watu sokoni wafanye wanachotaka na hivyo kufanya watu kuanza kuuza vitu barabarani bila utaratibu wa mji.

  Pamoja na kuwa na demokrasia haina maana watu wa mipango ya mji wapuuzwe ni lazima kuwe na utaratibu wa kufanya biashara na kufungua vigenge. Vilevile kuhusu sehemu nyingine za maandeleo kama sehemu za kujenga masoko ya kisasa na miji ya kisasa. Ni kweli kwamba kama mbunge Lema anatakiwa kuhakikisha hakuna kufukuzwa watu kwenye maeneo lakini ni lazima vilevile Lema ahakikishe ujenzi na maendeleo ya mji wa kitalii Arusha unafanyika.

  Malalamiko ya wananchi ni muhimu lakini huwezi kufurahisha kila mtu mmoja mmoja utakiwa uangalie Project na manufaa ya Arusha kwa ujumla. Vilevile Lema unatakiwa ujihusishe zaidi kwenye kutangaza Arusha nje ya nchi, kwenye balozi, na kufanya kazi na wizara ya utalii maana wana zile contact za groups za kifaifa za wageni lakini sijawahi kukusikia unafanya chochote. Kwenye Meeting ya Diaspora ya Marekani na uingereza ungekuja kutangaza Arusha maana wewe ni mbunge wa mji ambao unategemea utalii lakini sijakuona mwaka jana pale Virginia ingawa kulikuwa na watu wengi wa kampuni ya utalii.

  Sijawahi kusikia Lema unafanya mkutano na wafanyabishara wote wa Utalii na biashara nyinginge Arusha na kuwauliza shida zao ni zipi Arusha ni mji wa biashara hivyo huwezi kuongelea chadema pekee.

  Pamoja na ukweli kwamba umefanya kazi nzuri ya kueneza chama Arusha ni wakati wa kuongea biashara na kusaidia kuleta maendeleo Arusha. ​
   
Loading...