CHADEMA wagundua mtambo wa kuingiliana kwa mawasiliano

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Chama-cha-Demokrasia-na-Maendeleo-Chadema-founder-Edwin-Mtei.jpg


Saturday, July 21, 2012 1:52 PM
CHAMA CHA DEMOKRASIA na Maendeleo (Chadema), kimedai kugundua mtambo unachochea uvunjifu wa amani unaotumika kupitia mawasiliano ya simu za mkononi ambao unamilikiwa na mtoto wa kigogo wa CCM
Hayo yalisemwa jana mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA, Mabere Marando

Marando aliviambia vyombo vya habari kuwa, mtambo huo unafanya kuingiliana kwa mawasiliano ya simu ambapo anayekupigia si mlengwa

Alifafanua kuwa, mtambo huo una uwezo wa kufanya kupigiwa simu au kupokea ujumbe mfupi wa maneno na namba ambayo unaifahamu ambapo aliyetuma ama kupiga simu si mtu ambaye unamfahamu mwenye namba hiyo

Marando alisema mitambo hiyo ya inayomilikiwa na mtoto mmoja wa kigogo ambaye hajamtaja jina alisema aliinunua nchini Israeli ambapo kuna kampuni mbili alizozitaja kwa majina ya Nice System na Verinty System, ambazo zimefanikiwa kutengeneza mitambo yenye uwezo wa kuingilia kwa mawasiliano kati ya mtu na mtu kwa umbali wa kilometa tano

Alisema mitambo hiyo ndiyo ilitumiwa kusambaza ujumbe mfupi wa vitisho kwenye simu ya mbunge wa Iramba Magharibi, Mh.Mwigulu Nchemba.

Alifafanua mfumo uliotumika kuingiliana unaitwa sms proofing, na kwamba inaweza kutumiwa na idara za kiusalama kwa sababu maalum tu.

Pia alisema chama hicho kilisikitishwa na taarifa walizozipata kuwa mwanasheria mkuu wa serikali Jaji George Werema kuwaagiza watumishi wa ofisi yake kuandaa mashtaka kwa ajili ya tukio hilo la kuwahusisha wabunge wa CHADEMA na meseji hizo badala ya kushughulika na watu walioingilia mawasiliano yao.

Wiki iliyopita mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu, alisimama bungeni na kuomba mwongozo wa Spika akidai kuwa amepokea ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA, akitishiwa kuuawa.
 
inashangaza sana kwani mpaka sasa hivi tcra wameshindwa kununua mtambo ambao utaonyesha idadi ya simu na sms zinazotumika na makampuni ya simu ili waweze kukusanya kodi inayostahili badala yake tunasikia taarifa juu ya mtambo wa kuingilia mawasiliano tcra mnafanya nini?
 
Back
Top Bottom