Chadema waendelea kumng'ang'ania kinana

Chadema waendelea kumng'ang'ania kinana

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA, kwa mara nyingine imezidi kumbana Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ikimtaka mwendesha mashitaka wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumfungulia mashitaka ya kutorosha pembe za ndovu katika mahakama ya Afrika Mashariki.

Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo jana kwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2013/2014, Raya Ibrahim Khamis kwa niaba ya msemaji mkuu Ezekiel Wenje, alitaka Tanzania iombe msaada wa Kenya yenye ubalozi wa Vietnam ili kurahisisha upatikanaji wa ushahidi badala ya kutegemea ubalozi wake ulioko China.

Raya alisema madhumuni ya kumfungulia kesi Kinana yana lengo la kuudhibiti mtandao wa majangili na wafanyabiashara haramu ya pembe za ndovu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Alibainisha kuwa wanataka Kinana afunguliwe kesi kutokana na meli anazosimamia mojawapo ilikamatwa na shehena za pembe za ndovu huko Vietnam mwaka 2009.

Hii ni mara ya pili kwa kambi hiyo kuibua tuhuma hizo dhidi ya Kinana ambapo kwa mara ya kwanza msemaji mkuu wa kambi ya upinzani kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa alihoji jambo hilo na kupata upinzani mkali kutoka kwa wabunge wa CCM.

Raya alisema kuwa biashara haramu ya pembe za ndovu katika ukanda wa Afrika Mashariki inakua kwa kasi jambo linalotishia kutoweka kwa wanyama ndovu ambao ni kivutio kikubwa cha utalii.

Alisema kuwa taarifa katika mtandao wa habari wa "Annamiticus" (ANNAMITICUS :: News & Information About Endangered Species, Wildlife Trade & Wildlife Crime) zinasema kwamba mwaka jana, makontena mawili kutoka Kenya na Tanzania yalikamatwa huko Hong Kong yakiwa yamebeba tani 4 (kilo 4,000) za pembe za ndovu.

"Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kontena lililotoka Tanzania lilikuwa limeandikwa "plastic scrap" ikimaanisha kuwa lilikuwa na vifaa ya plastiki, lakini baada ya kufunguliwa kulikuwa na vipande 972 vya pembe halisi za ndovu zenye uzito wa kilogramu 1,927 pamoja na kilo moja na nusu ya unga wa pembe za ndovu zilizosagwa.

"Kontena lililotoka Kenya lilikuwa limeandikwa "roscoco beans" yaani maharage aina ya roscoco, lakini lilipofunguliwa kulikuwa na vipande 237 vya pembe za ndovu sawa na kilogramu 1,884," alisema.

Alifafanua kuwa kwa mujibu wa taarifa hiyo, wingi wa pembe hizo za ndovu zilizokamatwa, unadhihirisha kwamba tembo 600 kwa uchache waliuawa.

Aliongeza kuwa mwezi uliopita kontena jingine limekamatwa limesheheni pembe za ndovu 113 huko China zenye thamani ya dola za Marekani 400,000 likiwa limeandikwa kwamba limebeba vipuri (spareparts) kutoka Burundi.

"Kwa kuwa Burundi haina bandari, kuna uwezekano mkubwa kwamba kontena hilo lilipitia bandari ya Tanzania, na hivyo kuna uwezekano pia kwamba pembe hizo zinatokana na tembo waliouawa Tanzania," aliongeza.

Alisema kambi hiyo inataka kujua kama Serikali ya Tanzania imefanya mawasiliano na Burundi ili kujua ukweli kuhusu kontena lililosheheni pembe za ndovu lililokamatwa huko China.

Aliongeza kuwa kwa kuzingatia utekelezaji wa mpango mkakati wa amani na usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kubadilishana taarifa za uhalifu na usalama, ni vema serikali ikiwasiliana na wote wanaoweza kukamilisha uchunguzi husika.

Alisema kuwa kuna Watanzania walioshutumiwa na kusutwa kuhusika na mtandao huu wa biashara hii haramu ya pembe za ndovu akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Kinana.

"Kwa kuwa Serikali ya Tanzania inaonekana dhahiri kumtetea na kumlinda mtu huyu kwa kuwa ni kiongozi mkubwa wa chama tawala, kama alivyofanya Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi alipokuwa anatoa mchango wake kwenye bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii Aprili 30 mwaka huu.

"Na kwa kuwa tembo wengi wa Afrika Mashariki wanazidi kupotea kila siku kutokana na biashara hii haramu ya pembe za ndovu, jambo ambalo linaikosesha Jumuiya ya Afrika Mashariki mapato yatokanayo na utalii na hivyo kuiweka hatarini sekta ya utalii ya Afrika Mashariki, watu hawa lazima washtakiwe," alisema.

Raya pia aligusia uhuru wa habari kwa nchi wanachama huku akinukuu taarifa ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ya Mei 20 mwaka huu ambayo ilisema kuwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameamuru kufungiwa kwa gazeti la kila siku la nchi hiyo la "The Daily Monitor", na gazeti lingine la "Red Pepper".

Hatua hiyo ni kutokana na kuchapisha habari iliyofichua njama za Rais Museveni za kumuandaa mtoto wake, Muhoozi Kainerugaba ambaye ni brigedia wa jeshi kuwa rais wa nchi hiyo baada ya yeye kuondoka madarakani.

Hata hivyo, baada ya kuhitimisha hotuba yake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi aliomba mwongozo wa kiti akitaka wapinzani wakemewe kwa kukiuka kanuni na kutaja majina ya viongozi wakuu wa nchi kwa dhihaka.

"Mimi sitaki kuzungumzia suala la Kinana maana hizo ni porojo wacha waendelee, lakini nazungumzia ukiukwaji wa makusudi wa kanuni na kumtaja Rais Museveni kwa mambo ambayo eti msemaji ameyasikia kwenye redio pamoja na lile la Kinana japo tumeishajibu, lakini wanaendelea kujifurahisha.

Naomba ukemee jambo hili," alisema.

Hata hivyo, baada ya Lukuvi kuketi, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika naye aliomba mwongozo akitumia kanuni inayomruhusu mbunge kunukuu taarifa kwenye vyombo vya habari akisema kuwa Raya alikuwa sahihi.

Sitta amkingia kifua

Akijibu hoja hiyo wakati wa majumuisho, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta aliwataka CHADEMA wamuache Kinana afanye siasa na majibu watayaona mwaka 2015.

Sitta alisema CHADEMA imekuwa ikitumia nguvu kulazimisha hoja zao na inaonekana Kinana ndiye anayewakera kwa kuwa hatoki midomoni mwao.
"Kila siku Kinana…Kinana…jamani hebu acheni kumhusisha na biashara haramu ya pembe za ndovu," alisema.

 
CHADEMA ni bora iwaambie wananchi kwamba wao ni watchdog wa serikali kuliko kuendelea kuwalaghai wananchi kwamba CHADEMA ni chama cha Siasa.
 
CHADEMA haiwezi kuwaambia wananchi sera zake kwasababu CHADEMA wameshajua kuichukua hii nchi ni ndoto ya mchana ndiyo maana CHADEMA wameamua kubaki kutunga kashfa za uongo na kuwa watchdog wa serikali.
 
chadema ni bora iwaambie wananchi kwamba wao ni watchdog wa serikali kuliko kuendelea kuwalaghai wananchi kwamba chadema ni chama cha siasa.

kivipi funguka
 
Ukiwa ndani ya Mfumo mchafu[Corrupt System] kama wa CCM ni vigumu kuwa msafi.Sitta ni mchafu tangu zamani.Kuna Waungwana wanaomfahamu Sitta kiundani waliwahi kujiuliza alipata wapi ujasiri wa kumwita mwenzie[Lowassa] fisadi wakati yeye mwenyewe ni fisadi mkubwa.Si ajabu anamtetea fisadi mwenzao.Sitta is an epitome of hypocritical politicians this once was a great nation is full of.He was against FISADIs before he is for them?
 
unafikiri kwa nini wananchi wanajichukulia sheria mikononi nsasa hivi kuliko zamani?
huyu kinana si wakumwachia,tembo 700 kila siku ni wengi sana.
mi nashauri chadema si kumng'ang'ania tu bali ni kumbinya korodani kabisa.
 
sita aliingiza richmond nchini wakati akiongoza kituo cha uwekezaji kabla hajamwachia ole naiko akishirikiana na rosta,lowasa na kikwete na baada ya dili lake la kuwa wazziri mkuu kutekwa na boyz 2 men ndo akakurupuka na bunge kufichua dili lao.
akae kimya hana usafi wowote.
 
CHADEMA ni bora iwaambie wananchi kwamba wao ni watchdog wa serikali kuliko kuendelea kuwalaghai wananchi kwamba CHADEMA ni chama cha Siasa.

by vertue of being chama cha upinzani outomaticaly unakuwa ni watchdog wa chama tawala.ndiyo maana nalengo hasa la mfumo huu wa multparty.check and ballance.bilashaka hata ccm yenu italazimika kufanya hivyo kuanzia 2015.hapo upo ndg sumu?
 
CHADEMA haiwezi kuwaambia wananchi sera zake kwasababu CHADEMA wameshajua kuichukua hii nchi ni ndoto ya mchana ndiyo maana CHADEMA wameamua kubaki kutunga kashfa za uongo na kuwa watchdog wa serikali.
sera ni kitu gani wewe sum,u,ccm wamekaa na sera zao mnazoziita nzuri kwa miaka 50 nsa nchi ikiteketea na umasikini ukishika hatamu.
hatuhitaji sera wala ilani tunataka rasilimali za nchi zionekane zinawainua wanachi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
huo ujinga wako peleka lumumba mkafarijiane nao ila mjue siku yaja isiyo na jina.
 
unafikiri kwa nini wananchi wanajichukulia sheria mikononi nsasa hivi kuliko zamani?
huyu kinana si wakumwachia,tembo 700 kila siku ni wengi sana.
mi nashauri chadema si kumng'ang'ania tu bali ni kumbinya korodani kabisa.

Tembo 700 kwa siku?? Sasa vizazi vijavyo si watakua wanasikia kama hadithi tu na hao tembo si watakuwa wanawaona kwenye picha tu? Huyu mtu alitakiwa kunyongwa hadharani kabisa!
 
CHADEMA ni bora iwaambie wananchi kwamba wao ni watchdog wa serikali kuliko kuendelea kuwalaghai wananchi kwamba CHADEMA ni chama cha Siasa.

Wewe umwambie mkeo kuwa ni mwanaume sio kumlaghai mkeo kuwa wewe kama baba ndie mlinzi mkuu wa nyumba...!!

Kitu gani hicho? Gamba!
 
Kung'ang'aniwa kwenye sehemu hii ya hotuba.

8.0 BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA NDOVU AFRIKA YA MASHARIKI

Mheshimiwa Spika, biashara haramu ya pembe za ndovu katika ukanda wa Afrika ya Mashariki inakuwa kwa kasi sana jambo ambalo linatishia kutoweka kabisa kwa wanyama hao ambao ni kivutio kikubwa cha utalii. Taarifa katika mtandao wa habari wa “Annamiticus” (www.annamiticus.com) zinasema kwamba mwaka jana 2012, makontena mawili kutoka Kenya na Tanzania yalikamatwa huko HongKong yakiwa yamebeba tani 4 (Kilo 4,000) za pembe za ndovu.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa hiyo, kontena lililotoka Tanzani lilikuwa limeandikwa “plastic scrap” ikimaanisha kuwa lilikuwa na vifaa ya plastiki lakini baada ya kufunguliwa kulikuwa na vipande 972 vya pembe halisi za ndovu zenye uzito wa kilogramu 1,927 pamoja na kilo moja na nusu ya unga wa pembe za ndovu zilizosagwa. Kontena lililotoka Kenya lilikuwa limeandikwa “roscoco beans” yaani maharage aina ya roscoco, lakini lilipofunguliwa kulikuwa na vipande 237 vya pembe za ndovu sawa na kilogramu 1,884.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa hiyo, wingi wa pembe hizi za ndovu zilizokamatwa, unadhihirisha kwamba tembo 600 kwa uchache waliuwawa.

Mheshimiwa Spika, mwezi uliopita kontena lingine limekamatwa lililosheheni pembe za ndovu 113 huko China zenye thamani ya Dola za Kimarekani 400,000. Kontena hili liliandikwa kwamba limebeba vipuri (spareparts) toka Burundi .
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Burundi haina bandari, kuna uwezekano mkubwa kwamba kontena hilo lilipitia bandari ya Tanzania, na hivyo kuna uwezekano pia kwamba pembe hizo zinatokana na tembo waliouwawa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kujua kama Serikali ya Tanzania imefanya mawasiliano na Serikali ya Burundi ili kujua ukweli kuhusu kontena lililosheheni pembe za ndovu lililokamatwa huko China. Hii ni kwa kuzingatia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Amani na Usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (The Strategy for Regional Peace and Security) wa kubadilishana taarifa za uhalifu na usalama.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kuna watanzania walioshutumiwa na kusutwa kuhusika na mtandao huu wa biashara hii haramu ya pembe za ndovu akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Abdulrahman Kinana, na kwa kuwa Serikali ya Tanzania inaonekana dhahiri kumtetea na kumlinda mtu huyu kwa kuwa ni kiongozi mkubwa wa chama tawala, kama alivyofanya waziri wa mambo ya ndani Mhe. Emmanuel Nchimbi alipokuwa anatoa mchango wake kwenye bajeti ya wizara ya maliasili na utalii mnamo tarehe 30.04.2013, na kwa kuwa tembo wengi wa Afrika Mashariki wanazidi kupotea kila siku kutokana na biashara hii haramu ya pembe za ndovu jambo ambalo linaikosesha Jumuiya ya Afrika Mashariki mapato yatokanayo na utalii na hivyo kuiweka hatarini sekta ya utalii ya Afrika Mashariki.
Na kwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi alipokuwa anachangia hotuba ya Maliasili na utalii na kwa mujibu wa kumbukumbu rasmi za Bunge (Hansard) alisema kuwa kesi Na.3 na 4 ya mwaka 2009 kuhusu pembe za ndovu na meli iliyokamatwa Vietnam iliyokuwa mahakama ya Kisutu ilifutwa kutokana na Tanzania kutokuwa na mkataba wa kubadilishana wahalifu na Vietnam na hivyo kukosekana kwa ushahidi Mahakamani, (hansard ya tarehe 30.04.2013, uk.141) .

Hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inamtaka Mwendesha Mashtaka wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumfungulia mashtaka ndugu Abdulrahman Kinana katika mahakama ya Afrika Mashariki kwa madhumuni ya kuubaini na kuudhibiti mtandao wa majangili na wafanya biashara haramu ya pembe za ndovu katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki kutokana na Meli anazosimamia kama wakala wa meli mojawapo kukamatwa na shehena za pembe za ndovu huko Vietnam mwaka 2009.

Aidha, tunaitaka serikali iombe msaada kutoka nchi mwanachama ya Kenya ambayo ina ubalozi wa Vietnam ili kurahisisha upatikanaji wa ushahidi badala ya kutegemea ubalozi wetu ulioko China kama ilivyosemwa na hivyo kesi hii iweze kuendelea ili wahujumu hawa wa uchumi na washirika wao waweze kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria.
 
Kitu kimoja Mahakama ya Afrika Mashariki haina waendesha mashitaka. Ikiwa CHADEMA wanafikiri kuna ushaidi wa kutosha kumhusu Bw. Kinana wao kwa kutumia wanasheria wana ruhusa kupeleka mashitaka kwenye mahakama hiyo. Treaty ya Afrika Mashariki inaruhusu hili. Nilifikiria Mh Sitta hangejibu hivi kinyume chake akapiga siasa za kuwaponda CHADEMA!
 
Hivi kwanini wabunge wa Ccm wabamtetea sana Kinana badala ya kuomba ushahidi kwa wanaomuandama Kinana wao???? Au ni kwa vile wanajua ukweli wa hizi shutuma????
 
Siku ya hotuba ya wizara ya wanawake na watoto.watakuja na hotuba yenye heading.:
WIZARA YA WANAWAKE NA WATOTO NA BIASHARA HARAMU YA VIPUSA.
Halafu wanaendelea na hadithi ileile.
Si wafungue kesi kama wana ushahidi.
 
Sita mnafiki kama Kinana wanamwonea mbona tembo wanaisha na meli zake ndio zinakamatwa
 
Back
Top Bottom