Sumasuma
JF-Expert Member
- Jun 23, 2011
- 342
- 110
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vifendo vya fujo vilivyodaiwa kufanywa na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Februari 7, mwaka huu wakati wakirudi kutoka kwenye mikutano yao ya kampeni katika Shehia ya Mgeni Haji.
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Bw. Hamad Mussa Yussuf aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.
Alisema, wapo baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi ambao wamekuwa wakifanya fujo dhidi ya chama hicho wakati wakurudi kwenye mikutano ya kampeni.
Alisema, tukio hilo limetokea wakiwa wanarudi kwenye kampeni ndipo msafara wa gari lao liliposhambuliwa kwa mawe na kupasuliwa kioo cha mbele katika gari lao la matangazo pamoja na kuwatolea matusi viongozi wao wa tawi la Kiboje Manzese.
"Vitendo hivi vinafanywa kwa makusudi na wafuasi wa vyama vya upinzani kwa maelekezo ya viongozi wao na vina lengo la kuleta vurugu na fujo katika uchaguzi wa Jimbo hili la Uzini,"alisema
Alisema, hawataweza kuvumilia vitendo vyovyote vya 'kihuni' na fujo vitavyoendelea kufanywa na vyama vyovyote vya kisiasa dhidi yao.
Bw.Hamad alisema, taarifa za matukio yote hayo tayari wameyaripoti kwenye vyombo husika pamoja na kwa msimamizi wa uchaguzi jimboni humo katika Wilaya ya Kati na kwa Kamanda wa polisi.
Alisema, wanatarajia hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika pamoja na viongozi wao wote, hata hivyo alidai pindi madai yao hayo yatapopuuzwa na kutochukuliwa hatua yoyote hawataweza kuvumilia.
"Tuna imani na Tume ya Uchaguzi pamoja na Jeshi la Polisi, lakini wataposhindwa kuwachukulia hatua inayofaa kwa haya hatuwezi kukaa kimya," alidai.
Hata hivyo alitoa mwito kwa wanachama wao wawe watulivu katika kipindi hiki cha kampeni ili siku ya uchaguzi waweze kushiriki kuchagua Mwakilishi wanayemtaka bila vitisho na fujo ya aina yoyote.:A S 465: