Chadema wachapana makonde Mwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wachapana makonde Mwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Sep 24, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Chadema wachapana makonde Mwanza

  Jumatatu, Septemba 24, 2012 05:47

  Na John Maduhu, Mwanza


  *Vurugu kubwa zaibuka, mkutano wavunjika
  *
  Mbunge Kiwia ajificha chini ya meza kujinusuru

  KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Ilemela jana kilivunjika, baada ya kutokea vurugu kubwa, zilizosababisha wajumbe kutwangana makonde.

  Kikao hicho kilikuwa kikifanyika katika Hoteli ya Ladson iliyopo Bwiru, kwa ajili ya kupitisha majina ya wagombea wa nafasi ya meya na naibu meya wa Manispaa ya Ilemela,

  Hata hivyo askari polisi walifanikiwa kuwasili mapema hotelini hapo na kuwatawanya wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na vijana wa chama hicho, waliokuwa wamevamia kikao hicho.

  Vurugu hizo zilizodumu kwa saa moja na kusababisha kizaazaa hicho, zilizuka baada ya uongozi wa Kamati ya Utendaji wa chama hicho Wilaya ya Ilemela, kukaidi amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.

  Mahakama hiyo ilikuwa imezuia kufukuzwa uanachama wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kitangiri, Henry Matata, hadi pale kesi ya msingi itakapomalizika.

  Mahakama hiyo pia iliamuru diwani huyo aendelee kuwania nafasi ya umeya wa Ilemela, ambapo kamati hiyo ilizuia jina la Matata lisiwemo katika majina ya watu wanaogombea nafasi ya umeya.

  Dalili za kuvurugika kwa hali ya amani ilionekana tangu mapema, baada ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ilemela (OCD), Debora Magiligimba, kuwasili katika hoteli hiyo akiwa katika gari lililokuwa limebeba askari polisi.

  Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Yunusu Chilongozi, alisema kikao hicho hakitambui amri hiyo ya mahakama, hivyo hakukuwa na haja ya kumruhusu Matata kuwa miongoni mwa wagombea.

  Pamoja na juhudi za polisi kuwataka viongozi hao kuheshimu amri ya mahakama, viongozi hao walizidi kukaidi, ndipo OCD na askari wake walipoamua kuondoka katika eneo hilo na kuwaacha wanachama pamoja na viongozi wakiendelea kuvutana.

  Muda mfupi baada ya askari kuondoka, kundi kubwa la vijana wa Chadema lilivamia katika ukumbi huo na kuanza kutembeza kichapo kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji, hali iliyosababisha vurugu kubwa.

  Makundi hayo ya vijana ni miongoni mwa wafuasi wa chama hicho wanaopinga kitendo cha diwani huyo na mwenzake wa Kata ya Igoma kuvuliwa uanachama.

  Katika vurugu hizo, Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia (Chadema), aliyekuwa miongoni mwa wajumbe hao, aliamua kujificha chini ya meza kama njia ya kujinusuru.

  Wakati Kiwia akiingia uvunguni mwa meza kujinusuru, baadhi ya wajumbe walikimbia huku na kule na wengine waliamua kujificha chooni, ili kujinusuru.

  Kutokana na vurugu hizo, uongozi wa hoteli hiyo uliamua kupiga simu polisi ambapo kikosi cha polisi wenye silaha na zana nyingine walifika na kuwatawanya vijana hao.

  Akizungumza na Mtanzania baada ya vurugu hiyo, Chilongozi alizidi kusisitiza msimamo wa kamati yake kwamba, hapakuwa na sababu za kuahirisha kikao hicho.

  Chilongozi alifafanua zaidi na kusema kuwa kamati yake iliamua kumzuia Matata kutokana na maelekezo yaliyotolewa na viongozi wa juu kutoka makao makuu ya chama.

  Akizungumza na waandishi wa habari Matata alisema kuwa, kamati hiyo imeonyesha dharau kubwa kwa mahakama na kusema kuwa, wajumbe hao wanapaswa kuchukuliwa hatua ili iwe fundisho.

  "Amri ya mahakama haiwezi kuvunjwa na wahuni wachache kwa manufaa yao, nitapigania haki yangu hadi pale kitakapoeleweka, siwezi kukaa kimya," alisema Matata.

  SOURCE; MTANZANIA YA LEO

   
 2. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Na bado! it is just a beginig,to show their true colour!
   
 3. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,400
  Likes Received: 10,518
  Trophy Points: 280
  Hawa ndio tuwape nchi yetu si itakuwa hatari.
   
 4. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Hii habari imekaa kishabiki sana, hata muandishi hakutulia kabisa
   
 5. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kumbe source ni gazeti la Bashe!!!
   
 6. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  sasa nchi untaka apewe nini?

   
 7. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo nchi ibaki kwa "wanaoongoza" kwa bastola? Nyie subirini mziki wenu 2015, mtajua nani atakae kabidhiwa nchi, hata kama ni kwa mtindo wa Ivory Coast! Nyie kura hampati hata kwa dawa.
   
 8. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wachangiaji umewasoma?
   
 9. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Umeonaee! iko siku wakiwa madarakani,utasikia prezidaa kazichapa na pm wake! hawafaiiii!
   
 10. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,400
  Likes Received: 10,518
  Trophy Points: 280
  Tena hawa jamaa lazima tuwe makini sana inawezakuwa ni wakimbizi kwa sababu mambo ya kupigana pigana sisi hatuna.
   
 11. Opinionated

  Opinionated Senior Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ngoja niwambie ukweli kwa wale wanaofikiri hizi fujo zililetwa na wanachama halali wanaoipenda chama chao. Ukweli wa mambo ni Matata alitafuta vijana wakwenda kufanya fujo. Usiku wa kuamkia tukio hilo Matata alisikika katika katika hoteli moja ijulikanayo kama Hotel Kingdom ambako alikuwa akinya na watu kadha pamoja na Katibu wa CCM wilaya ya Ilemela na Jamaa mwingine wa CCM. Matata alisikika akipanga jinsi ya kupata watu wakwenda kufanya fujo kesho yake.

  Huyu jamaa(matata) ni jangili wa siku nyingi hapa mwanza na anafahamika. Pia anashirikiana na CCM kutaka kuivuruga Chadema.
   
 12. t

  thatha JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  mkuu do u trust the source???

  is there any relation with your comment???
   
 13. t

  thatha JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  usifiche ugonjwa ww,kifo kitakuumbua siku moja.kinachotakiwa hapa ni kutatua mgogoro/tatizo sio kutumia mabavu au kutumia lugha ya kujihami kama ya kwako hapa
   
 14. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hawa wachagiaji wako ofisi moja pale Lumumba. Gazeti la Mtanzania ni gazeti mkakati la CCM
   
 15. t

  thatha JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu umefuatilia ,hakuna mambo ya ukabila na udini huko? sababu za kuchapana ni nini?
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Teh teh teh, kwani hawa wachangiaji ndo wamewaambia CDM wachapane?
   
 17. t

  thatha JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Tabia ya mtu haitibiwa bali ugonjwa ndo unatibiwa-maneno ya babu yangu. Hawa jamaa wa CDM unavyoona wanajibu utumbo hivyo ndivyo walivyokuwanzia wapambe,,wanachama na hata viongozi, sasa wataachaje kuchapana?
   
 18. t

  thatha JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Wangezuia magazeti yasiandike kuliko kushambulia wachangiaji humu utafikiri ndo waliwaambia CDM wachapane.
   
 19. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  unajuaje kama hao waliovamia walitumwa kuvuruga kikao? Naona sasa ccm kinaingilia vikao vya ndani baada ya kushindwa mikutano ya hadhara
   
 20. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  baada ya poliSISIM kuondoka likaingia kundi kubwa la vijana kufanya fujo.CHANGANYA NA ZA KWAKO
   
Loading...