Elections 2010 Chadema wababe HAI, kwa kura moja toka CCM!!

Wa Kwilondo

JF-Expert Member
Sep 15, 2007
1,081
312
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi na kufanikiwa kuongoza Halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.
Diwani wa Kata ya Machame Kaskazini, Clement Kwayu, ndiye alishinda nafasi ya mwenyekiti wa halmashauri hiyo. Hai ni Halmashauri ya sita kuongozwa na CHADEMA nyingine ni Kigoma Ujiji, Mwanza, Musoma Mjini, Karatu, Moshi Mjini.
Kabla ya jana, uchaguzi huo ulishindikana na kuahirishwa mara mbili, baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Melkizedeck Humbe, kukataa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, aliyeruhusu wabunge wawili wa Viti Maalumu mkoani Kilimanjaro kupitia CHADEMA, Lucy Owenya na Grace Kiwelu, kuwa ni wajumbe halali wa baraza hilo.
Kwayu alipata kura 12 dhidi ya mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ally Mwanga, aliyepata kura 10. Nafasi ya makamu mwenyekiti haikupata mshindi, kwani walifungana kwa kura, hata baada ya kurudiwa.
Baraza la Madiwani wa wilaya hiyo, lilikubaliana na kauli moja kuwa waliokuwa wakigombea nafasi hiyo waongoze kwa kuachiana.
Atakayeanza kuongoza kwenye nafasi ya makamu mwenyekiti katika mwaka wa kwanza ni Diwani wa Kata ya Weruweru, Adris Mandrai (CCM). Baadaye atafuata Diwani wa Kata ya Masama Kati, Deogratius Kimaro (CHADEMA).
Hata hivyo, matokeo hayo yameibua mtafaruku ndani ya CCM baada ya viongozi wa chama hicho kudai kuwa kuna diwani wao mmoja ambaye amewasaliti na wanamjua. Walidai watamfukuza kwenye chama.
Kila chama kilikuwa na wajumbe 11, hali iliyokuwa inaviweka katika wakati mgumu wa kupata mshindi.
Awali, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa kikao hicho, aliwataka watendaji wa serikali kujifunza taratibu za uongozi.
Alisema kuwa kitendo cha watendaji kukaidi maelekezo ya Mwanasheria Mkuu ni ushahidi kwamba watendaji hao hawajui taratibu za uendeshaji wa shughuli za kila siku ndani ya serikali yao.


Source: Tanzania daima:A S thumbs_up:
 
Mungu awabariki nyie mliofumbua macho na kuwakataa wauaji. Chadema mtafuteni huyu mwanamapinduzi toka cccm aliyewapa ushindi na mkae nae aachane na hao mabedui na wauaji
 
Kwani huyo mwana CCM aliyeipigia kura CDM amefuata sera au chama? Kuna haja gani ya wagombea kujieleza kama wasikilizaji wana jibu la nani apewe kura?
 
safi sana
kumbe kunawatu ndani ssm wasiokubaliana na mambo yanavyoenda?
kweli nimekubali na huu msemo 'usituone wavumilivu ukafikiri hatusikii maumivu'
 
Tuseme ukweli wana ccm wanapata maumivu ya maisha na wamechoka nayo!wanachoogopa ni kupoteza walau kile kimkate chao cha ubabaishaji.
 
Kuchaguliwa kwa kiongozi kwa wanaojua maana ya uongozi hakuangalii chama wanaangalia uwezo wa mtu hasa kulingana na sera zake. Na ndicho kilichotokea Hai.
 
Umeashum Madiwani woote wa CHADEMA wameipigia chadema na kapatikana mmoja toka CCM. Je hujui kwamba kuna uwezekano madiwani 10 wa Chadema wameipigia CCM na diwani mmoja tuu wa Chadema ndo kaipigia Chadema na madiwani woote kumi na moja wa CCM wameipigia Chadema hivyo kura zao zoote 10 zimetoka Chadema. Hivyo hata CCM waache kutafuta msaliti maana yawezekana Chadema inawasaliti zaidi ya mmoja na CCM inawasaliti hata zaidi ya mmoja. Najaribu kufikiria kisayansi zaidi
 
Kweli tunahitaji ufanisi na si jina au mbwebwe za mtu. Utendaji na uwajibikaji ndio tija kwa taifa. Tanzania inahitaji watu wazalendo na wachapa kazi sio wanaosinzia hata mcha na mwisho wa siku wanakinga sahani kupata msosi tema kushinda watendaji wenyewe.:love:
 
safari bado ndefu, yaani halmashauri sita tu tanzania nzima ndio zimeenda cdm


Ukilinganisha na kipindi cha nyuma, mimi naona ni hatua nzuri kuwa na hizo sita. mimi bado naamini kuwa zitaongezeka maana pia Arusha itakuwa chini ya CHADEMA.
 
Back
Top Bottom