Mkuu Nikupateje,
Kwanza niseme tu kwanza mie ndg yako huwa nafurahi sana kila nipatapo fursa ya kujadili na mtu makini wa aina ya mtu kama wewe,Pongezi kwako mkuu.
Mkuu kwanza nikubaliane kabisa na ushauri wako ambao umenipa kwani una maslahi mapana ktk taifa lolote lenye kupenda kuona demokrasia huru na ya haki,Japo mada kuu niliyokiichangia ililenga Jimbo la Nachingwea lkn si dhambi mapungufu yaliyoonekana yakafanyiwa kazi kwa maslahi ya taifa lote kwa ujumla.Ni ukweli usiopingika kuwa mapungufu yote haya yanayolalamikiwa leo katika nyanja karibu zote! CCM yenyewe na serikali inayoiongoza wanayajua!,Chakujiuliza hapa ni kwanini yapo? Kwanini yanaendelea kuwepo? Na kwa manufaa ya nani?.Binafsi nasikitika sana ninaposikia msomi anapokubali kumezeshwa ujinga na yeye bila kuhoji anatamka neno "SERIKALI YA CCM" badala ya neno "SERIKALI INAYOONGOZWA NA CCM"! Kwa uelewa wangu mimi serikali si mali ya chama cha siasa ktk nchi yoyote ya demokrasia huru na ya haki,Na tukiweza kutofautisha maneno haya mawili itakuwa tumepiga hatu kubwa sana ktk taifa.Kiongozi aliye kwa ajili ya kuongoza hawezi kukulazimisha kukuongoza bali Mtawala aliye kwa lengo la kukutawala lazima hata kama hautaki atakulazimisha kukutawala! Hivyo uongozi unahitaji hekima,busara na maono kwa maslahi ya wanaongozwa,Wakati utawala unahitaji nguvu nyingi na maono binafsi kwa maslahi binafsi ya watawala.Unategemea nini kutoka kwa mtu wa ccm ambaye tayari anasema waziwazi serikali ni yake!? Yani kapewa ridhaa ya kuiongoza yeye keshajimilikisha!.Na ndio maana leo ukisimama na kumkosoa kiongozi wa serikali au kumuomba ufafanuzi kuhusu jambo fulani mtu wa ccm anakujia juu,Usishangae ukaenda kuhuliza swali ofc ya serikali(wizarani) Dar lkn majibu ukayapata toka kwa msemaji wa ccm baada ya kumalizika kikao cha lumumba Dodoma.Nirejee kuhusu matokeo yatangazwe kwenye vituo vya kupigia kura moja kwa moja,Kwa hili sidhani kama itakuwa rahisi kukubalika kwa wanaojiita wenye serikali na ndio maana matokeo haya ubambikwa jina "MATOKEO YA AWALI YASIYO RASMI".Labda tusubir maamuzi magumu ya kwenye katiba kama tunavyosimuliwa na tume.NB;Nachingwea ya leo sio ya 1995,Elimu ya urahia imetuingia vizur mnoooo.Naishia hapa ili nijiandae kesho naenda kuchukua malipo ya korosho ya stakabadhi gharani,Maana nasikia wametuletea walahu sh.400 badala ya sh.600 tuliyokiwadai kwa kilo 1! lkn Mungu yupo tutavumilia 2015 si mbali wanakusini tutaionyesha kwa kuikumbusha ccm kuwa huku ndiko mkoloni alinyooshea mikono.