Nimekuwa nikitafakari kwa muda mrefu sana kuhusu Posts na Comments ninazokutana nazo kwenye mitandao ya jamii, zinahusiana na siasa za Tanzania. Mitandao hiyo ni kama hii Jf, twitter, facebook, blogs nk; wengi wanaotoa comments inaonekana kuwa kama si washabiki basi ni wanachama wa CHADEMA. Hii dalili nzuri kwa chama hiki pendwa kwani watumiaji wengi wa hii mitandao ni wasomi na/au vijana ambao wanao uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko.
Ukweli huu unadhihirika pale anapokuwa anatoa Topic/Thread mwanachama au mshabiki wa CCM; hiyo topic ikiwa imelalia upande wa CCM, wengi wanaochangia wanam-oppose vikali sana. Sasa ambacho najiuliza ni kuwa hizi ni dalili gani kwa Chadema? Kuna mchango gani mitandao hii ilionayo katika kukua kwa Chama cha siasa? Wasomi wengi (ambao ndo wanaitumia sana mitandao hii), wameichoka CCM? Kifo cha ccm? Au humu wengi ni wahuni, kama wanavyojitetea ccm?
Nawasilisha!
Hali hii imesababishwa na mambo mengi, lakini sababu kubwa ni sisiem yenyewe kupitia serikali. TANZANIA ya sasa si ile ya MWALIMU, ni nyingine kabisa. CCM wanataka na wanafanya kila mbinu ili TZ iendelee kuwa ile2 ya ENZI za SUPER MWALIMU. CCM wanaamini njia pekee ya kuendelea na TZ ya MWL ni kubana vyombo vya habari: magazeti, tv, radio nk. WANANCHI wamewagomea, ambapo kwa msaada wa sasa wa TEKINOHAMA, wananchi wameanzisha njia mbadala za kupata habari wanazozitaka: mitandao ya kijamii.
CCM wanataka vyombo vyote vya habari viandike au vitangaze habari za KIKWETE au NNAPE ( yaani watu wao) amesema ..., amekemea ..., ameahidi (kujenga bara2 ya MAKUTANO, BUTIAMA, SERENGETI, MTO WA MBU, bila kutaja litaanza kujengwa lini, fedha zitatoka wapi nk) ...., nk. WANANCHI kwa sasa hawataki habari hizo za upande mmoja, wao wanataka mjadala, na pale mjadala unapokosekana, wanahama. MFANO mzuri ni TBC ya TIDO vs ya sasa, na bunge la SITTA lililokuwa na mijadala moto2 vs la MAKINDA lililofunga waheshimiwa midomo: watu hawaangalii tena.
KWA MAONI yangu utaratibu huu ulioanzishwa na CCM, unaiua nchi. KWA SABABU katika democrasia ya vyama vingi siku zote na popote pale dunia kunakuwa na pande mbili: a = b; "
a" ni chama kilichomadarakani na wakereketwa wake, hapa TZ ni CCM, na "
b" ni vyama pinzani na watu wengine wote wenye mawazo mbadala kwa watawala. UKIONDOA "
a" kwenye mlinganyo huu, basi hakuna mlinganyo tena, bali "
b" pekee. CCM imejiondoa yenyewe kwenye mlinganyo huu (kwa sababu hawataki mijadala, wanataka kile wanachopelekea walaji yaani wasikilizaji wao kipokelewe bila mjadala wowote wala kupingwa kwa namna yoyote ile), kwa hiyo hakuna mlinganyo tena. HALI hii imesababisha wananchi ambao wanataka mijadala kuhama vyombo vya habari vilivyozoeleka kama redio na televisheni kwenda kwenye mitandao ya kijamii kujadili kinachoendelea kwenye jamii. NA kwa kuwa huko nako CCM haipo, basi habari zinazoandikwa ni za upande mmoja kama ambavyo umetaja kwenye posting yako.
SASA hii hali ni hatari sana kwa uhai wa nchi kwani, japo inasaidia maslahi ya muda mfupi ya CCM - kusogeza mbele kidoogo muda wa kukaa madarakani. HALI HII, KAMA nchi wananchi tunakosa nafasi ya kujadili, kuchambua, kutafakari, kuchuja na kutenganisha uongo na ukweli kati ya sera za chama kimoja dhidi ya kingine - tunabaki kujadili chama kimoja tu, na hivyo maana ya vyama vingi inakuwa imepotea. Hali hii inaisadia CCM kwa wao kusema na kisha kuondoka, wanakuja tena kipindi kingine wanasema kitu kile2 na kisha kuondoka; na kwa sbb hakuna mtu wa kuwauliza "mbona kipindi kile mlisema hay2?" wanachaguliwa ...