CHADEMA vs Mitandao ya Jamii

Nimekuwa nikitafakari kwa muda mrefu sana kuhusu Posts na Comments ninazokutana nazo kwenye mitandao ya jamii, zinahusiana na siasa za Tanzania. Mitandao hiyo ni kama hii Jf, twitter, facebook, blogs nk; wengi wanaotoa comments inaonekana kuwa kama si washabiki basi ni wanachama wa CHADEMA. Hii dalili nzuri kwa chama hiki pendwa kwani watumiaji wengi wa hii mitandao ni wasomi na/au vijana ambao wanao uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko.

Ukweli huu unadhihirika pale anapokuwa anatoa Topic/Thread mwanachama au mshabiki wa CCM; hiyo topic ikiwa imelalia upande wa CCM, wengi wanaochangia wanam-oppose vikali sana. Sasa ambacho najiuliza ni kuwa hizi ni dalili gani kwa Chadema? Kuna mchango gani mitandao hii ilionayo katika kukua kwa Chama cha siasa? Wasomi wengi (ambao ndo wanaitumia sana mitandao hii), wameichoka CCM? Kifo cha ccm? Au humu wengi ni wahuni, kama wanavyojitetea ccm?
Nawasilisha!

I think ur right
 
Kuna wengine hatuna msimamo na chama chochote, tunakata issues tu.
 
Kiongozi humu hamna wahuni bali kuna Vikosi kazi vyenye kuchambua mchele na chunya (great thinkers)!
 
Nimekuwa nikitafakari kwa muda mrefu sana kuhusu Posts na Comments ninazokutana nazo kwenye mitandao ya jamii, zinahusiana na siasa za Tanzania. Mitandao hiyo ni kama hii Jf, twitter, facebook, blogs nk; wengi wanaotoa comments inaonekana kuwa kama si washabiki basi ni wanachama wa CHADEMA. Hii dalili nzuri kwa chama hiki pendwa kwani watumiaji wengi wa hii mitandao ni wasomi na/au vijana ambao wanao uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko.

Ukweli huu unadhihirika pale anapokuwa anatoa Topic/Thread mwanachama au mshabiki wa CCM; hiyo topic ikiwa imelalia upande wa CCM, wengi wanaochangia wanam-oppose vikali sana. Sasa ambacho najiuliza ni kuwa hizi ni dalili gani kwa Chadema? Kuna mchango gani mitandao hii ilionayo katika kukua kwa Chama cha siasa? Wasomi wengi (ambao ndo wanaitumia sana mitandao hii), wameichoka CCM? Kifo cha ccm? Au humu wengi ni wahuni, kama wanavyojitetea ccm?
Nawasilisha!

Karibu jamii forum
 
Nimependa jinsi watu wanavyozidi kuchangia mada hii. Nimeshaanza kupata majibu, na kikubwa nilichokigundua ni humu kuna watu wa aina mbili; waliotayari kuelewa na kuchangia mada positively, hawa ndio tunaowataka na wanauwezo wa hata kukiimarisha chama hata mtaani (nje ya mitandao). Lakini kundi la pili ni lile ambalo likotayari kwa ubishi usio na maana yoyote. Mfano, mtu anaona neno 'WAHUNI' anaanza kukuambia tuombe radhi eti wameitwa wahuni, wakati angesoma between the lines kwa lengo la kuelewa hata asingepata hiyo shida. But all in all my thread aimed at provoking and/or finding out the reality of wha is happening in these social networks in relation to the changes happening in the country. Still, your ideas are needed, and are very potential to ensure the real meaning of change we are proclaiming!
 
ccm kama chama kwa kiasi kikubwa wametoka kwenye misingi ya chama chenyewe na kuwa cha cha wenye pesa au mamlaka inayo pitiliza. kuna wakati wao hudhani wako juu ya sheria na wanaweza kufanya chochote ili mradi kinawapendeza wao.KIBURI CHA MADARAKA.Hawawajali tena masikini wa nchi hii na hivyo kujenga chuki isiyo na kifani.
Akitokea mwana ccm anaye wajali walala hoi utashangaa watanzania hawahawa wanampenda na kumshabikia sana mfano DEO FILIKUNJOMBE,MAGUFULI,PRO SOSPETER MHONGO nk wanaishi na kutenda kama wananchi wanavyo wategemea.
 
Ccm aka choo cha makuti bado wapo kwenye analogia chadema tupo kwenye digtali,,chama cha kishamba na kipumbavu kama ccm hakuna msomi na kijana mimi anayeweza kukishabikia labda hawe na mtindio wa ubongo kama mwigulu na nape
 
Mhimili mkubwa wa Chama cha Siasa ni lile kundi la kati; yaani watu wasio maskini wala matajiri sana. Katika Marxism, watu wa kati hupambana ili wasirudi kwenye umaskini wa kupindukia, wakati huo wakipigana wawafikie matajiri huko juu.

Matajiri kwa upande wao, huwekeza kulinda utawala uliopo madarakani ili kujihakikishia ulinzi wa mali zao.

Maskini au kapuku, yeye ni mtu wa kuyumbishwa tu, maana mwenye njaa kali hana maamuzi.

Nionavyo, kundi la "mitandao", ni kundi muhimu katika kukieneza chama. Ni kundi lisiloyumbishwa; ni kundi la wasomi; ni kundi lenye "wivu" wa kufika kileleni; ni kundi litakalokiondoa CCM.

Jiulize, kwa nini katika Jiji la Dsm CHADEMA kilishinda KAWE na UBUNGO na si ILALA au KINONDONI?
 
hapo kwenye red...nina shaka na elimu yako...hv ni nani mwenye upeo asiyejua madudu ya ccm....i ll never like ccm!

mimi ndio kabisa nina shaka na elimu yako yaani umeshindwa kutambua typing error!.... i will never like chadema
 
Nimekuwa nikitafakari kwa muda mrefu sana kuhusu Posts na Comments ninazokutana nazo kwenye mitandao ya jamii, zinahusiana na siasa za Tanzania. Mitandao hiyo ni kama hii Jf, twitter, facebook, blogs nk; wengi wanaotoa comments inaonekana kuwa kama si washabiki basi ni wanachama wa CHADEMA. Hii dalili nzuri kwa chama hiki pendwa kwani watumiaji wengi wa hii mitandao ni wasomi na/au vijana ambao wanao uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko.

Ukweli huu unadhihirika pale anapokuwa anatoa Topic/Thread mwanachama au mshabiki wa CCM; hiyo topic ikiwa imelalia upande wa CCM, wengi wanaochangia wanam-oppose vikali sana. Sasa ambacho najiuliza ni kuwa hizi ni dalili gani kwa Chadema? Kuna mchango gani mitandao hii ilionayo katika kukua kwa Chama cha siasa? Wasomi wengi (ambao ndo wanaitumia sana mitandao hii), wameichoka CCM? Kifo cha ccm? Au humu wengi ni wahuni, kama wanavyojitetea ccm?
Nawasilisha!

Hali hii imesababishwa na mambo mengi, lakini sababu kubwa ni sisiem yenyewe kupitia serikali. TANZANIA ya sasa si ile ya MWALIMU, ni nyingine kabisa. CCM wanataka na wanafanya kila mbinu ili TZ iendelee kuwa ile2 ya ENZI za SUPER MWALIMU. CCM wanaamini njia pekee ya kuendelea na TZ ya MWL ni kubana vyombo vya habari: magazeti, tv, radio nk. WANANCHI wamewagomea, ambapo kwa msaada wa sasa wa TEKINOHAMA, wananchi wameanzisha njia mbadala za kupata habari wanazozitaka: mitandao ya kijamii.

CCM wanataka vyombo vyote vya habari viandike au vitangaze habari za KIKWETE au NNAPE ( yaani watu wao) amesema ..., amekemea ..., ameahidi (kujenga bara2 ya MAKUTANO, BUTIAMA, SERENGETI, MTO WA MBU, bila kutaja litaanza kujengwa lini, fedha zitatoka wapi nk) ...., nk. WANANCHI kwa sasa hawataki habari hizo za upande mmoja, wao wanataka mjadala, na pale mjadala unapokosekana, wanahama. MFANO mzuri ni TBC ya TIDO vs ya sasa, na bunge la SITTA lililokuwa na mijadala moto2 vs la MAKINDA lililofunga waheshimiwa midomo: watu hawaangalii tena.

KWA MAONI yangu utaratibu huu ulioanzishwa na CCM, unaiua nchi. KWA SABABU katika democrasia ya vyama vingi siku zote na popote pale dunia kunakuwa na pande mbili: a = b; "a" ni chama kilichomadarakani na wakereketwa wake, hapa TZ ni CCM, na "b" ni vyama pinzani na watu wengine wote wenye mawazo mbadala kwa watawala. UKIONDOA "a" kwenye mlinganyo huu, basi hakuna mlinganyo tena, bali "b" pekee. CCM imejiondoa yenyewe kwenye mlinganyo huu (kwa sababu hawataki mijadala, wanataka kile wanachopelekea walaji yaani wasikilizaji wao kipokelewe bila mjadala wowote wala kupingwa kwa namna yoyote ile), kwa hiyo hakuna mlinganyo tena. HALI hii imesababisha wananchi ambao wanataka mijadala kuhama vyombo vya habari vilivyozoeleka kama redio na televisheni kwenda kwenye mitandao ya kijamii kujadili kinachoendelea kwenye jamii. NA kwa kuwa huko nako CCM haipo, basi habari zinazoandikwa ni za upande mmoja kama ambavyo umetaja kwenye posting yako.

SASA hii hali ni hatari sana kwa uhai wa nchi kwani, japo inasaidia maslahi ya muda mfupi ya CCM - kusogeza mbele kidoogo muda wa kukaa madarakani. HALI HII, KAMA nchi wananchi tunakosa nafasi ya kujadili, kuchambua, kutafakari, kuchuja na kutenganisha uongo na ukweli kati ya sera za chama kimoja dhidi ya kingine - tunabaki kujadili chama kimoja tu, na hivyo maana ya vyama vingi inakuwa imepotea. Hali hii inaisadia CCM kwa wao kusema na kisha kuondoka, wanakuja tena kipindi kingine wanasema kitu kile2 na kisha kuondoka; na kwa sbb hakuna mtu wa kuwauliza "mbona kipindi kile mlisema hay2?" wanachaguliwa ...
 
Mimi ni mwana CCM damu na nikijana. Na tupo kama 20 hivi kazini kwetu wote ni wanaccm sijui mnaongelea wasomi wapi.
Maana msomi halisi mwenye fikra pevu hawezi kuwa mwana CDM hata siku moja.
 
Mimi jana nilipoona server ya JF imeenda down nikajua Kafumu kavuliwa ubunge kwani nilijua server imezidiwa traffic ya pongezi na updates.
 
Watanzania tuna Hulka za KupiGa mdomo pasi Matendo...tufanye Changes za kweli zinatufikisha. Tunapotaka sio tunakimbia kwa kuogopa Mabomu na Askari siku ya Kupiga Kura ...
 
Mimi ni mwana CCM damu na nikijana. Na tupo kama 20 hivi kazini kwetu wote ni wanaccm sijui mnaongelea wasomi wapi. Maana msomi halisi mwenye fikra pevu hawezi kuwa mwana CDM hata siku moja.
unaweza kuwa kijana lakiki akili za kizee
 
unaweza kuwa kijana lakiki akili za kizee
Sio kila mtu anawaza unavyo waza wewe na si kila mtu anapenda unacho penda wewe. Na usidhani kuwa wewe unaakili sawa sawa. Pale ulipo tu umeonesha kutokuwa na akili kamili. Your Intelligent but your not Wise
 
Back
Top Bottom