Mkuu nashukuru hili umeliona kutoka angle nyingine .CCM kwa hulka yake ime declare an all out war against wananchi wasioipenda kwa kutumia silaha yoyote ile na zozote zile na moja wapo katika silaha hiyo ni vulnerable Dr. Slaa. He will soon wake up out of his slumber and slowly realize kwamba Watanzania wa sasa si wale wa 2010, this is a completely new breed. Bila kujua Dr. Slaa anaijeruhi CCM kuliko Lowassa or UKAWA for that matter, mark my words.
JokaKuu, za miaka mkuu!..I took the worst case scenario kwamba Lowassa siyo Ukawa.
..lakini baada ya kutafakari, hata katika mazingira ambayo Lowassa siyo ukawa, bado nimeangukia kwenye kwenye scenario namba 1.
..I like ur strategy ya kutokuweka "mayai yote ktk kikapu kimoja." It is something I have toyed with for some time. lakini ktk kampeni hizi, CCM inaendelea kufanya mambo yanayozidi kunitibua, na ndiyo maana nimeshawishika kuwapumzisha kila mahali.
..Tangu Magufuli aanze kufanya kampeni kwa nia ya kupotosha waziwazi, nimepoteza hata ile heshima ndogo niliyokuwa nayo kwake. Hivi kweli miaka 20 aliyokaa serikalini, na exposure aliyoipata, hafahamu tofauti ya kilichotokea Libya, Iraq, Zaire, na hiki kinachoendelea hapa Tanzania?
NB:
..unaweza kutuletea uzi wa hii theory yako ya kutokuweka mayai yote ktk kikapu kimoja.
..choice ya kwanza itakuwa ni Lowassa Raisi, Waziri Mkuu toka CCM, chama cha kikuu cha upinzani CDM/UKAWA.
..choice ya pili itakuwa ni Raisi Magufuli, Waziri Mkuu toka CDM/UKAWA, chama kikuu cha upinzani CCM.
..choice ya tatu ni Raisi na waziri mkuu kutoka chama kimoja, lakini chama tawala kina very slim majority.
cc Rev. Kishoka, Zakumi, Nguruvi3, NasDaz
Hili la kuweka mayai yote kapu moja linaweza kutokea.
Huko nyuma katika mijadala tuliwahi kuzungumza na JokaKuu . Tulisema hivi
Plan ya UKAWA , Plan A1 kushinda dola na bunge, Plan A2 kushinda kimoja kati ya dola au Bunge.
Hakuna Plan A na B
Kwa hali iliyopo inaonekana linawezekana kwasababu hizi
UKAWA wanaweza kushinda Bunge na Serikali
CCM wanaweza kushinda bunge na Serikali
Kwa bahati mbaya UKAWA wameacha jukumu la kuwa ‘power broker'
Ukitazama kwa jicho pevu attention yao imeondoka katika suala la bunge
Kwahiyo wameamua kucheza karata moja kubwa! Ni hatari isiyoonekana lakini ipo
Kwa maana kuwa meli ikizama izame na mzigo
Hii kasi ya kujiadhirisha mbele ya kadamnasi inamfuta kabisa kutoka kuwa mtu mahiri na mwenye busara.
Inaelekea baada ya Serena, kafuata interview ya Tido na sasa Star TV kujitetea mno na kuendelea kutoa hoja ambayo ni kutwanga ngumi kwenye maji.
Lakini pia hii ni mbinu ya kuondoa wanahabari kufuatilia kampeni za Ukawa. Propaganda za CCM ni distortation na mis-information.
Dr. Slaa anajitangaza kana kwamba kaonewa haki ya kuwa mgombea wa Chadema/Ukawa (his tone and choice of words says it in plain english despite his continuous refusal kuwa hautaki Uraisi) hivyo anatafuta sympathy ya wananchi ambao wanahamasishwa kuanza maandamano ya kumuaga na yeye eti anaanza kampeni ya kuaga wananchi kutembelea mikoa.
Go figure mtu anayedai kuwa na roho safi kabisa!
Hivi ni akina nani wanaunda 'Genge' la Lowassa?...
Kuna yeyote anaweza kunisaidia kuwataja kwa majina?...
Pia si vibaya mkuu wangu ukaanza na hao aliowaacha CCM...
NasDaz ahlan wasahalan!!JokaKuu, za miaka mkuu!
Nikirudi kwenye mnakasha, kwanza siungi mkono kauli ya kwamba EL ataleta mabadiliko... kama lengo ni kuitoa CCM, sawa lakini kwamba eti kuleta mabadiliko; sioni ni namna gani mabadiliko hayo yanaweza kuletwa na mtu kama EL unless kama tunaota ndoto za mchana kwamba EL akiingia madarakani, ataharakisha mchakato wa katiba mpya (mchakato mwingine) na kuleta katiba inayopunguza nguvu za rais... sioni uwezekano huo na kama hakuna, sitarajii mabadiliko yoyote, labda mabadiliko ya kuileta Tanganyika!
MABADILIKO TOWARDS TANGANYIKA! Hapa EL ameshafahamu kwamba Watanzania ni rahisi kuwateka akili! Narudia, EL hana ubavu wa ku-engineer mabadiliko ya katiba itakayojali maslahi mapana ya wananchi na kupunguza nguvu dola! Ili kuwateka zaidi CHADEMA na CUF, sana sana ninachoona anaweza kufanya ni ku-revive tu Rasimu ya Katiba Ya Jaji Warioba na kurudisha suala la serikali tatu ambalo sichelei kulisema hata kidogo kwamba ndio pekee ambalo linaimarisha ushirikiano huu wa UKAWA, husani kati ya CHADEMA na CUF... huku CHADEMA wanataka Tanganyika yao, na kule CUF wanataka Zanzibar yao yenye mamlaka kamili!
Kwangu mimi, Lipumba anaaminika maradufu kumlinganisha na Maalim Seif! Sioni makubaliano ya msingi kati ya Maalim Seif na Mbowe zaidi ya ikiwa CUF wataiunga mkono CHADEMA na EL, basi EL akiingia madarakani, waiachie Zanzibar mamlaka kamili... sioni lingine zaidi ya hili na katika hili, Maalim Seif yupo tayari kwa lolote!
Hili likifanyika, wote tutapiga vigelegele kwamba tayari tumepata mabadiliko as if rushwa, ufisadi, ukosefu wa uwajibikaji, ukiukwaji wa haki za raia na mambo mengine yote ya hovyo yanatokea kv hatuna Tanganyika!
Mkuu GLAxyS3Mkuu,
Nukta yangu ya msingi katika bandiko langu kwa JokaKuu ni kuwa, hizo plan A1, plan A2 zote ziko kwenye interest UKAWA. Swali ni kuwa what is best for Tanzania. Kwa maoni yangu ni kuwa UKAWA hii ya Lowasa haiwezi kuleta yale mabadiliko yaliyo kwenye fikra za mtanzania wa kawaida (najua utakuwa na opionion yako kwenye hili).
Swali ni je, kutokana na tuliyojifunza katika miaka 10 iliyopita kwenye accountable government. Is it in the best interest ya Mtanzania kuweka mayai yake yote kwenye kapu moja?
Najua inawezekana niko nje kidogo ya mjadala wa Dr. Slaa unaoendelea sasa hivi ila nadhani kwenye hoja kuu ya original bandiko nadhani bado niko. Naomba radhi kama sipo.
Nguruvi3, ni kweli nilisema nitarudi na mathalani nimepata ka muda kidogo naomba nianze kwa kuwapa changamoto kidogo wachangiaji wanaofuatilia kwa haya maswali;Mkuu GLAxyS3
Upo katika mada kabisa. Ukisoma kwa ukaribu bandiko na kule tulikolitoa suala lamabadiliko ni muhimu sana.
Na hapo wengi tumetofautiana sana
Kwa mfano, sisi wengine tunaamini mbadiliko yaliyotoka katika wanachama waliojenga vyamavya upinzani wenyewe ni real and sustainable.
Huu ndio msingi wa kusema upo uwezekano wa Plan A1 na A2 kupitia wanachama waliopigania mabadiliko ya dhati
Kwa upande mwingine, watu kama JokaKuu Alinda @Ma3 wanasema, nilazima kukata kichwa cha joka kwanza, ili kupata nafasi ya kuhangaika na mijusi au vinyoka mbele ya safari (chase thefox to the bush first..)
Ni wazi tunataka mabadiliko, sote tunataka hili dudu lililodumu miaka 50 sisi tukidumaa
liondoke. Hilo ndilo linasukuma watu wengi kukubali chochote ilimradi tu kuiondoa CCM.
Kuna mambo mawili kutokana na hali hiyo
Immediate measure ambazo ni hizi tunazoona za kukukmbatiakila kitu
Sustainable measure ambazo kwa sasa wengine hawaoni kamani kipaumbele na wewe unasomeka kuwa pro
Katika hili kuna wale wanaosema ujio wa Lowassa utasaidiakatika harakati za kupambana na tembo sitting room.
Wapo wanaosema kuna tatizo na ujio kwasababu hakukuwa na maadalizi na political base ipo paralysed muda ukiwa hautoi nafasi ku recuperate from the drastic changes
Pengine Mag3 atakaporudi ataweza kutusaidia kupambanua kamaujio wa Lowassa ambao ni immediate measure unaweza kuwa msaada na kwamba ni asset na denominator
Kwa upande mwingine GalaxyS3 utusaidie kama tunaweza kuwa na sustainable changes tembo akiwa amejaa sitting room , if not, how long we've to wait
Sasa umeeliza what is best kwa mwananchi. Tunaweza kusemathe best thing ni CCM kuondoka madarakani.
Rearrangement of the system siyo task ngumu kama kuiondoa CCM.
Namwananchi atakuwa bora bila CCM hata kama mbadala utakuwa mbovu
Mkuu JokaKuu, Ahlan bīkNasDaz ahlan wasahalan!!
..nafurahi kusikia toka kwako baada ya kimya kirefu.
..bila kuleta mabadiliko EL atapoteza support ya political base iliyomuingiza ikulu.
..sitegemei kama Lowassa atakuwa mjinga kiasi kwamba afanye mambo ambayo yatawatibua UKAWA. Unless ana mipango ya kurudi CCM.
..zaidi kama wananchi wakiweza kuiondoa CCM ujue kwamba EL atakuwa ana-deal na MAZOEA MAPYA. Itakuwa vigumu sana kwa mtawala[chama/raisi/wabunge] yeyote yule kuendelea kukaa madarakani bila kutekeleza matakwa ya wapiga kura waliomuingiza madarakani.
NB:
..mimi nataka ile IMANI kwamba ukipitishwa na CCM wewe moja kwa moja ni Raisi wa Tanzania ifutike ktk vichwa vya wa-Tanzania.
..pia napenda kusiwe na chama chenye 66% ya kupitisha miswada na sheria ktk bunge la muungano.
Mosi, kwa suala la kutompokea EL, sina sababu ya kumung'unya maneno kusema kwamba endapo UKAWA wasingempokea EL ingekuwa wamefanya kosa kubwa sana la kisiasa kwa sababu, pamoja na yote yanayosemwa, bado ukweli unabaki pale pale kwamba EL ni tishio kwa CCM.Na katika msingi huo huo naomba niulize swali muhimu kwa wakati huu nalo ni je hali ingekuwaje ndani ya UKAWA kama Lowassa asingepokelewa na kuteuliwa kuwa mgombea wa Uraisi? Hapa maswali mengine ya nyongeza yanayofuatia hilo ni je hali ingekuwaje kama, kwa mfano, Prof, Lipumba wa CUF ndiye angeteuliwa? Na je Dr. Slaa wa Chadema ? Na mwisho je Dr. George Kahangwa wa NCCR Mageuzi?
NasDaz, tofauti kubwa kati ya mimi na wewe ni moja tu; wakati unaamini kwamba wapo binadamu who are born destined to be evil mimi, on the other hand, sikubaliani na falsafa hiyo. Mimi naamini kwamba hakuna kitu kama hicho na badala yake ni mazingira tunayokulia na jamii tunayoishi kama sehemu yake is what shapes our destiny. Mdahalo wa kama yawezekana binadamu akazaliwa akiwa muovu umefanyika kwa karne nyingi na matokeo yake kwa ufupi ni kwamba siku zote wanaosema hapana wameshinda.
NasDaz, humans are just born, humans are nor Evil nor Good. Humans are just human, and the only reason for them to become Evil, is if the environment they are surrounded by, encourages bad behaviors. Humans when they are born don't have a sense of what is going on, so how could we tell if they are born Evil? They don't even have any memory. Everything comes into their life as the grow older.
Kinachonishangaza katika huu mjadala ni namna tulivyo tayari kuwagawa viongozi wetu katika makundi mawili, wale ambao tunaweza kuyafumbia macho makosa yao na wale ambao hatuko tayari kuwapa nafasi hata wakitubu. Mimi sikumtaka Lowassa katika mazingira ya awali alokuwemo na hivyo hivyo nilikuwa upande wa Dr. Slaa katika mazingira alokuwemo awali lakini sasa nimebadilisha msimamo.
I believe that neither of these two guys was born evil but that it is the environment that influenced what they turned out to be each in his own way. With the wind of change now blowing, Dr. Slaa apparently appears decided to build a wall to stop it while Lowassa has decided to build a windwill to utilize it...guys, to exist is to change, to change is to mature, to mature is to go on creating oneself endlessly.
Kila kitu kinachosemwa kuhusu namna Lowassa atakavyondesha serikali akiwa Raisi kinasukumwa na hisia na kwa bahati mbaya hisia hizo zinaongozwa na vitu vitatu; chuki, mashaka na woga. Ni kweli yawezekana wapo wengi wasio na imani na lengo la Lowassa tofauti na mimi niliye tayari kumpa faida ya shaka kama nilivyo tayari kumpa faida ya shaka mtu yeyote atakayeunga mkono mabadiliko.
Faida ya kuingia timu mpya katika utawala wa nchi hii ni nyingi lakini kubwa kuliko zote ni ustaarabu wa kupokezana kijiti. Aina hii ya ustaarabu hujenga uvumilivu ndani ya jamii na kupunguza hofu na mashaka inayoandamana na kiu ya mabadiliko. Tukifanikiwa katika hili tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana katika kujenga utawala unaowajibika na kuondoa kabisa ulaghai na kiburi katika kuwatumikia wananchi.
Lakini, si Dk Slaa alikuwa CCM. Yeye liwezajekubadilikaMag3;
Ni kiongozi gani ambaye ametubu na watu wakaendelea kumsakama na makosa yake? Dr. Slaa hajafanya kosa lolote. Lowassa hajasema chochote kile kuhusu shutuma zinazotolewa dhidi yake.
Ninapobeba mabox tunashushulisha na mambo ya management. Utafiti wa studies nyingi katika management zinaonyesha kuwa maendeleo ya mtu binafsi, taasisi, au ya jamii mara nyingi hayashuki kutoka mbinguni. Ni matokeo ya watu yaliyopangwa (deliberate actions).
Deliberately, you decided to venture in maths, computers and electronics. Deliberately, Lowassa decided to accumulate wealth. Na tunapojikita katika deliberate actions zinazobadilisha maisha yetu tunajenga characters ambazo ni vigumu sana kwa sisi wenyewe kuzifuta.
Ni vigumu kwako kubadilisha characters ambazo zimekufikisha ulipo. Vilevile ni vigumu kwa Lowassa kubadilisha characters zilipomfikisha alipo. Kitendo cha Lowassa kujiunga na CDM sio ufunio aliuona Paulo ambao ulimfanya kuacha kuwatesa wafuasi ya Yesu na baadaye kujiunga nao. Hivyo usitegemea kuwa atabadilika.
Lakini, si Dk Slaa alikuwa CCM. Yeye liwezajekubadilika
Wengi tu walikuwa CCM wamebadilika
Usisahau mwananchi aliyeipigia CCM kura miaka 50 anaweza kupigia upinzani. Je, hajabadilika!
Kwa hoja yako hii, watakaobadilisha Tanzania lazimawatoke nje ya nchi kama si mbinuni
Senti sumuni tu
..Dr.Slaa sasa hivi yuko karibu na Dr.Mwakyembe na Mwigulu Nchemba.
..kwa mtizamo wangu Dr anapaswa kuwa makini sana na hawa marafiki zake wapya.
cc Rev. Kishoka, Nguruvi3, Alinda, ZeMarcopolo
Mag3;
Lowassa hajasema chochote kile kuhusu shutuma zinazotolewa dhidi yake.
Kwa mujibu wa Tundu Lisu, Lowasa alijieleza mbele ya kamati kuu kuhusiana na tuhuma zinazomkabili hususan Richmond ambapo alimtaja mhusika mkuu. Ukiondoa Dr Slaa hatujasikia mjumbe mwingine yoyote wa kamati kuu alieonyesha kutoridhika na maelezo ya Lowasa.
Bado swali la msingi linabaki kwa Dr Slaa kwamba pingamizi lake kwa Lowasa linatokana na tuhuma za ufisadi au kutotimiza "masharti" ikiwemo kuingia na wabunge na wenyeviti wa CCM wa mikoa?