Gilbert A Massawe
JF-Expert Member
- May 14, 2015
- 5,922
- 4,716
Wanataka uhuru wa kuranda randa mtaani
Hebu wekeni wazi hapa. Kama vyama vya upinzani nchini,na katika afya ya demokrasia,mnahitaji uhuru gani?
Wahusika,ingawa hawajanituma,wapo hewani kufuatilia mtakacho ili mpewe hata kama kitakawia kidogo. Tajeni uhuru muutakao ndani na nje ya Bunge.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Geita)
Mzee tupatupa kama uko Geita hebu ulizia issue ya Mawazo kama hujaonyeshwa wahusika mtaani wakila bata na wengine wakizunguka na Ma-Prado- viongozi wa chama chako pendwa.
Uliza kwa siri hapo kwenye ofisi zenu za chama karibu na choo cha Max. Watakwambia!
Her!! Wee jamaa simu umenunua nyingine au, maana ile si wamefunga?Hebu wekeni wazi hapa. Kama vyama vya upinzani nchini,na katika afya ya demokrasia,mnahitaji uhuru gani?
Wahusika,ingawa hawajanituma,wapo hewani kufuatilia mtakacho ili mpewe hata kama kitakawia kidogo. Tajeni uhuru muutakao ndani na nje ya Bunge.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Geita)
Mzee Tupatupa, tunadai haki ya kufanya shughuli za kisiasa kwa uhuru.
Haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na kujadiliana na wananchi juu ya changamoto zinazotukabili kama jamii.
Haki ya kutoa maoni bila kubugudhiwa. (Freedom of expression);tutoe maoni yetu juu ya budget ya serikali, tuongelee kashfa ya Lugumi, tujadili escrow, uuzwaji wa nyumba za serikali, mikataba ya UDA. n.k
Tunahitaji mshindi wa uchaguzi atokane na kura za wananchi na sio tume.
Tunahitaji mipaka ya mihimili mitatu ya serikali iwepo na ionekane na bunge liache kugeuzwa kikao cha chama kama ilivyo sasa.
Tunahitaji ushindi wa Maalim Zanzibar utambuliwe.
Tunahitaji tume huru ya uchaguzi.
Tunahitaji ukomo wa figisufigisu kwa mameya wetu na halmashauri zilizo chini yetu.
Tunahitaji mauaji ,mateso na udhalilishaji kisiasa uliokwisha fanyika utambuliwe kitaifa na wahusika wachukuliwe hatua.
Tunahitaji bunge live..
Mzee tupatupa, nikiendelea ni litania ila kimsingi CCM imetuchosha ipumzike.
#I HATE MAGUFULI