afsa
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 1,986
- 1,592
Katika kura za maoni zinazoendelea CHADEMA Wataweka wagombea katika kata ambayo hawajawahi kufika kufanya mkutano wowote wa kisiasa. Baada ya vijana kwa wazee kuchoshwa na mwenendo wa CCM wameamua kuweka wagombea wao kupitia CHADEMA na kupata ufuasi mkubwa hapa katani kwetu. Walianza kama utani, hatimae wakafaulu kuweka wagombea wanaopendekezwa. Kata yetu INA vijiji 2 wameweka wenyeviti wa vijiji vyote viwili huku wakijidai kuwa siku ya kupiga kura kufikia SAA 5 asubuhi watakuwa wameshinda vijiji vyote. Hii kata ina vitongoji 19 wameweka wanaopendekezwa vitongoji vyote na wajumbe wa serikali ya kijiji wote. Wakati 2009 CHADEMA hawakuweka mgombea yeyote CCM waliweka mgombea wao kila kijiji na kila kitongoji, mwaka huu imekua tofauti kwani CCM imeshindwa kuweka wagombea katika vitongoji 3. Wana Jf kuelekea uchaguzi huu wa serikali za mitaa kila mwana Jf atuwekee hapa mtaa/kijiji ni jinsi gani UKAWA na CCM wameweka wawakilishi wao kila mtaa/kitongoji/kijiji