vipik2
JF-Expert Member
- Nov 24, 2011
- 2,853
- 2,270
Inaonyesha jinsi ambavyo waTZ elimu imeshuka. Mnatoa kashfa na kejeli za nini? CDM kwa kufuata katiba na sheria za nchi kama watapata mgombea mzuri aingie kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi. Kidemokrasia wakiona labda mgombeaji wa CUF anafaa wanaweza kujiondoa huko mbele ya safari ili upinzani ushinde. Lengo ni kupata viongozi wenye uwezo wa kuiongoza hii nchi kikatiba na kisheria kwani kwa sasa kwa mwananchi wa kawaida tunaona mambo hayaendi sawa sawa hasa upande wa elimu na afya.
Mtu yeyote anayshabikia ukabila na udini hana nafasi katika taifa hili kwani sisi tu wamoja na taifa hili sio la kidini wala kikabila ni letu sote.
CDM pamoja na wapinzani au Wakiungana na chama chochote basi Chalinze wanaweza shinda kwa kishindo, hii ni kutokana na Ramani ya jimbo la Chalinze ina population kubwa pembezoni mwa barabara ya Morogoro road ambako pia watu wamechanganyika bila kujali udini eg Chalinze penyewe, Vigwaza Ubena Zomozi, Mbala, Magindu etc, ukabila na ukwere ukwere kidogo ni tatizo kule Msata, Lugoba, Msoga, Wami, Madesa.. etc kwani hao wanajali ukabila sana na ndio hako ka group kadogo ambako mara ya mwisho 2010 walionekana wakiwa na gari mbili tatu hivi asubuhi wakienda Ikulu kushuhudia na kuona ------ mwenzao akiapishwa kamwe sikuona mkwavi katika kundi hilo,...
CHANGAMOTO KUBWA NINAYOIONA KUKWAMISHA CDM NI UMASKINI WA WATU WA CHALINZE WAKATI YULE BWANA MDOGO ANAZO ZA KUTOSHA KUTOKANA NA BIASHAARA ZAKE HALALI NA ZISIZO HALALI