CHADEMA: Ubunge jimbo la Chalinze

CHADEMA: Ubunge jimbo la Chalinze

Chadema Diaspora

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2010
Posts
480
Reaction score
644
CHADEMA JIMBO LA CHALINZE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

6 MACHI, 2014

Chama cha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Chalinze kimeanza mchakato wa ndani wa kupata mgombea ubunge kwa ajili ya uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Aprili, mwaka huu, ambapo fomu za uteuzi zimeanza kutolewa kwenye Ofisi Jimbo, kuanzia tarehe 4 Machi na mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu hizo itakuwa tarehe 7 Machi 2014, saa 10.00, jioni.

Kura za maoni ndani ya chama, zitafanyika tarehe 8 Machi katika Mji wa Chalinze na kufuatiwa na kikao cha kamati ya utendaji ya jimbo ili kufanya uteuzi wa awali kwa mujibu wa Katiba ya chama na hatimaye kikao cha Kamati Kuu kufanya uteuzi wa mwisho ili kupata mgombea atakayeshindana na wagombea wa vyama vingine.

Mpaka sasa wagombea waliochukua fomu kwenye ofisi ya jimbo ni watatu (3) na wagombea wengine watatu (3) wamechukulia fomu Ofisi za Makao Makuu ya Chama, Dar es Salaam, hivyo hadi sasa idadi ya wagombea waliotambuliwa rasmi ni sita.

Tunatumia nafasi hii kuujulisha umma wa Watanzania, hususan wanachama wa CHADEMA, kuwa fomu za kuwania uteuzi wa ndani zinaendelea kupatikana sehemu tatu, Makao Makuu ya Chama, Ofisi ya Jimbo la Chalinze na kwenye tovuti ya chama Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo – Chadema

Imetolewa Machi 5, 2014
Iddi Omary Ucheche
Katibu wa CHADEMA, Jimbo la Chalinze
0756 639014

Ahsante MPIGANAJI,Arusha tupo nanyi.

Chadema na wakwere/waislam wa chalinze wapi na wapi?
Mngelikua na akili ya mbali hiyo pesa inayoenda kwenye kampeini za chalinze mngeipeleka kwenye mradi wowote wa wabunge wenu walau hata jimbo moja au msaada kwenye kituo cha kulelea watoto yatima ili kumnusuru mbunge huyo na kimbuga kinachowanyemelea kwa kupoteza majimbo kibao 2015 kuliko kuifanyia kampeini.....

Hiyo nafasi cuf inawafaa sana lakini sio chadema....
Siasa za kibongo huitaji akili nyingi kuzichambua hasa linapokuja suala la udini/ukabila/ukanda...

Cuf kamata fulsa twende zetu.
 
Vipi twaweza kuwafahamu hao waliojitokeza?kila la heri makamanda.
 
Chadema na wakwere/waislam wa chalinze wapi na wapi?
Mngelikua na akili ya mbali hiyo pesa inayoenda kwenye kampeini za chalinze mngeipeleka kwenye mradi wowote wa wabunge wenu walau hata jimbo moja au msaada kwenye kituo cha kulelea watoto yatima ili kumnusuru mbunge huyo na kimbuga kinachowanyemelea kwa kupoteza majimbo kibao 2015 kuliko kuifanyia kampeini.....

Hiyo nafasi cuf inawafaa sana lakini sio chadema....
Siasa za kibongo huitaji akili nyingi kuzichambua hasa linapokuja suala la udini/ukabila/ukanda...

Cuf kamata fulsa twende zetu.

Ni dhahiri kuwa wewe ni mmoja wa wale wasiopenda kuiona CDM ikiendelea na harakati za kumkomboa Mtanzania.
 
Tunawaombea kwa Mungu mmpate jasiri atakaye mnyang'anya mwana wa mfalme Juha fimbo na hivyo kumwonesha mfalme kuwa hatufurahii jinsi anavyowalinda wauza sembe,jamaa wa EPA na hawa wawindaji wa mjini,ambao hawaui sungura wala digidigi ila tembo na faru
 
Chadema na wakwere/waislam wa chalinze wapi na wapi?
Mngelikua na akili ya mbali hiyo pesa inayoenda kwenye kampeini za chalinze mngeipeleka kwenye mradi wowote wa wabunge wenu walau hata jimbo moja au msaada kwenye kituo cha kulelea watoto yatima ili kumnusuru mbunge huyo na kimbuga kinachowanyemelea kwa kupoteza majimbo kibao 2015 kuliko kuifanyia kampeini.....

Hiyo nafasi cuf inawafaa sana lakini sio chadema....
Siasa za kibongo huitaji akili nyingi kuzichambua hasa linapokuja suala la udini/ukabila/ukanda...

Cuf kamata fulsa twende zetu.

hatukumuogopa baba yake mzazi mwaka 2010 mpaka akafikia kutumia kete ya udini kuwagawa watu kwahiyo mwanae ni mwepesi kwani hana record yeyote ya utumishi wa umma zaidi ya kutumia jina a baba kutafutia ubunge.
 
Jiandaeni kwa kipigo kingine chadema kwisha habari yao wamepotezwa na ACT.
 
Hao waliochukulia Makao Makuu wajulikane mapema. Yasije yakatokea ya Kalenga ambapo Tendega alichukulia fomu makao makuu lakini akashindwa kupata kura za kutosha matokeo yake Makao Makuu hao hao wakabadilisha Matokeo
 
Jiandaeni kwa kipigo kingine chadema kwisha habari yao wamepotezwa na ACT.

hvi ile mimba yako imefikie miezi mingapi au imepitiliza nenda clinic haraka itabdi ujifungue kwa operation, hzi chuki zko cyo bure ni dalili unataka kuzaa tena mtt wakoa atakuwa ni wakike
 
Chadema na wakwere/waislam wa chalinze wapi na wapi?
Mngelikua na akili ya mbali hiyo pesa inayoenda kwenye kampeini za chalinze mngeipeleka kwenye mradi wowote wa wabunge wenu walau hata jimbo moja au msaada kwenye kituo cha kulelea watoto yatima ili kumnusuru mbunge huyo na kimbuga kinachowanyemelea kwa kupoteza majimbo kibao 2015 kuliko kuifanyia kampeini.....

Hiyo nafasi cuf inawafaa sana lakini sio chadema....
Siasa za kibongo huitaji akili nyingi kuzichambua hasa linapokuja suala la udini/ukabila/ukanda...

Cuf kamata fulsa twende zetu.

Uijui chalinze ,dini kuna wakristo na waislamu idadi sawa .kabila wakwere .maasai,wakwavi,ect .ondoa hii hoja yako ya ukabila na udini .,na watanzania wote wakulaani kwa kutuletea ubaguzi kwenye karne hii .
 
Back
Top Bottom