CHADEMA: Tutashinda tena Sombetini

CHADEMA: Tutashinda tena Sombetini

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Posts
1,237
Reaction score
1,828
Ndugu zetu Arusha leo Feb 8 tunaenda kuhitimisha kampeni za udiwani wa kata ya Sombetini zilizoanza Jan 16.Hitimisho la kampeni hizi ambazo sisi CHADEMA tutahitimisha katika viwanja vya Ngusero,tunahitimisha kampeni wakati wanachama wetu 9 wakiwa wamejeruhiwa kwa mapanga na green guard.

Jumamosi ya leo inatukumbusha Tarehe 15.06.2013 viwanja vya Soweto wakati wa hitimisho la Kampeni za kata nne,pale watawala walipouwa raia wasiokuwa na hatia kwa bomu.Lilikuwa tukio ovu kabisa katika historia ya mageuzi ya nchi yetu,ulikuwa ukiukwaji mkubwa sana dhidi ya utu na haki ya kuishi ya binadamu.Hata hivyo hatutokata tama wala kurudi nyuma dhidi ya wakandamizaji, wanyonyaji, wakiukaji wa haki za binadamu.Hata hivyo umma wa Arusha ukadhihirisha kuwa haukubaliani na mauaji haya na hivyo tukashinda kata zote nne.

Tunahitimisha kampeni zetu tukiwa wajasiri sana,tukiwa na uhakika wa ushindi wa 95%,ushindi ambao utakuwa kwa heshima ya wale waliouwawa katika harakati za mabadiliko ya Taifa letu.

Tunawashukuru sana Sombetini kwa kutuunga mkono,tutalinda kura zetu kwa gharama yoyote

A man who won't die for something is not fit to live.
 
Kwani hiyo kata ili kuwa ina ongozwa na diwani wa chama gani kabla ya uchaguzi huu wa pili?.
 
Ni aibu kubwa CCM kutumia majambazi kujeruhi watu huyo Mjusi ni Jambazi mkuwa anafahamika na watu wote hapa Arusha kama muuaji inakuwaje CCM kumtumia katika matukio ya uchaguzi?

KANU ilitengeneza Mungiki na hatimaye UHURU KENYATA anayo mashtaka ya kujibu kutokana na hivyo vikundi vya wauaji alivyo kuwa anavitumia. Hakuna sababu ya kutumia wauaji katika siasa tumieni nguvu ya hoja na tekelezeni yale ambayo mliahidi katika ilani ya uchaguzi.

Arusha CCM haina chake hiyo inatokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi watu wamewadharau.
 
Mr Nanyaro ni vizuri kwetu kwa habari hiyo kila la heri mzee lakini hapo kwenye tarehe ni 2013 na si 2014
 
15.06.2014 Bado hatufika mkuu huenda 2013. Ila naamini ushindi Daima. Nilikuwa natamni ile ya Bukoba tuwapige 5-0. Mungu awajalie majeruhi afya njema.
 
Tunawaamini makamanda wa Arusha, ushindi ni wenu, cha msingi wekeni ulinzi mkali, msiwaamini hao polisi hata kidogo, Mungu awatangulie.
 
Nanyaro ongea kwa kujiamini, ushundi kwa Chadema ni mpango mzima. Niko na watu 30 wa kuoifa jura kwa Chadema bado yangu na nke wangu. Ccm ni laana
 
wauza maziwa bwana?? baada ya vurugu kushindikana sasa hivi mnajipa matumaini ya kushinda, subiri box la kura liseme
 
Chadema Arusha ushindi ni kama mtu kujitongozea mkeo vile. Hahahahaha!!!
 
Kila rakheri Arusha, makamanda mlinde kura!
 
CCM wasahau Arusha!!!pamoja na kugawa fedha na kuwrubuni vijana eti wajiunge kwenye vikundi ili wawezeshwe!!lakini hamna kitu wataambulia!!!Kula ccm kulala Chadema!!!CHADEMA DAIMA
 
Back
Top Bottom