CHADEMA tusilalamike matokeo ya Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA tusilalamike matokeo ya Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Ringo Edmund, Mar 5, 2012.

 1. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  WADAU HABARI ZA MCHANA.
  NIMEKUWA NIKIFUATILIA BAADHI YA CHAGUZI NDOGO TANZANIA NILICHOGUNDUA NI KUWA KWA MFUMO ULIOPO CCM ITAKUWA IKITANGAZWA MSHINDI KILA UCHAGUZI WAUTAKAO(SI KUSHINDA)

  igunga chadema ilishinda ila ccm ikatangazwa.
  uzini raza alishinda(si ccm)

  chadema kila siku wanafanya mambo kama hawaijui ccm,uchaguzi wa igunga walitumia turufu yacuf hapo arumeru lazima watakuja na mbinu mpya ya wizi.
  kumbuka majimbo waliyoshinda chadema 2010 ni kwa sababu ccm walilala wakidhani watanzania ni wale wale na kuelekeza nguvu kwenye urais.

  chadema walitakiwa kufungua kesi ya kikatiba ili watanzania waliofikisha miaka 18 toka daftari lilipofanyiwa marekebisho waingizwe kwenye daftari.
  wazee akili zao zinahitaji msaada,bibi zetu bado wanaichagua ccm na ccm wanalijua hilo.

  chadema hata impeleke obama kuwa kampeni manager wasishangae ccm ikatangazwa mshindi,chadema kupata idadi kubwa ya kura sina hofu nalo ila kutangazwa mshindi ni kitu nyingine.

  nitakuwa arumeru kwa ajili ya kampeni za chadema ila viongozi wangu tutafute namna ya kupigana na adui.:A S new:
   
 2. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kweli Mkuu...
  Mbinu pekee ni
  1. Kulinda kura
  2. Nguvu ya umma ya kutosha

  (miujiza ya Arusha mjini)

  saiv hatuwezi kurudisha mda nyuma!
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwa pamoja tutashinda.....tuunganishe nguvu kulikomboe jimbo la Arumeru Mashariki
  ....Tuwetayari kutoa michango ya hali na mali
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wewe unaota au umeamua kuwatukana Mbowe na SLAA kuwa hawana akili mpaka wakubali matokeo. Acha kutapatapa wewe CCM ni Noma, wananchi wanaikubali sana , tunadanganyana tu humu JF kwa vile tunasogeza muda ufike wa kutoka kIbaruani. Kumpgia kura mtu kama sugu, Lema ,Mdee , Wenje na wengine mpaka uwe mwendawazimu na inahitaji moyo. Machizi yale ndiyo maana wananchi wenye akili zao watakushangaa kuhusu ushindi wa CCM katika chaguzi mbalimbali. Halafu umesema vizuri sana ila kinyume, unajua majimbo ya Nyamagana, Mbeya Mjini, Kawe, Mbulu,Arusha mjini na mengine mengi lilishinda jina la Chama ila siyo watu.
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kama Arusha tuliweza kwanini siyo Arumeru ....mimi ninaimani kabisa tutaweza kuwa bana tofauti na ilivyo kuwa kule Igunga...Babu na Bibi zetu tuendelee kuwa elimisha.......
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Safari hii kazi munayo Arusha-Arumeru siyo Igunga kura tutazilinda kwa gharama yoyote......
   
 7. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Mbwa koko kila siku unaweza ukampiga mawe mateke nk, atakimbia na makelele, lakini ukizidi sana kumuonea mpaka nyumbani kwake, bado unampiga tu, ndugu yangu! Akikugeukia ni afadhali ushambuliwe na mbwa wa polisi! "Huwezi kuwafanya watu wote wajinga siku zote" (Abraham Lincoln) na Waswahili tunasema " hakuna refu lisilo na ncha!"
   
 8. Rabi wa Leo

  Rabi wa Leo Senior Member

  #8
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa anawatusi waziwazi watanzania na wapiga kura wa Mbeya,mwanza,kawe,arusha,iringa n.k kwa kuwa wametumia vema haki yao kikatiba kuchagua watu makini...Anaenda mbali zaidi kwa kuwavunjia heshima na utu waheshimiwa sana akina Sugu,Mdee,wenje n.k..Lakini nimwambie tu ukweli kua,ama atake,ama asitake,kuifananisha chadema na ccm ni sawa na kufananisha kifo na usingizi..CCM kina hali mbaya zaidi ya inavyoonekana..ccm kimeoza kiasi kwamba makada wamekalia matusi na vijembe kwa Chadema..CCM INAKUFA KIFO CHA ASILI...KINAKWENDA KUPUMZIKA NA WAASISI WAKE..kimeishiwa sera,hakina dira,kimepungukiwa watendaji makini,kimekosa nguvu,kina uhaba wa busara,kimechoshwa na upinzani,kina utajiri wa majungu,vijembe,vitisho na fujo,na zaidi ya yote,KIMEJAALIWA MAKADA HOHEHAHE WASIOJUA KUKITETEA BALI KUWATUSI WATANZANIA BILA HAYA WALA WOGA...Nawapa pole wapiga kura na wanachama wa chadema kwa matusi hayo.,nina imani viongozi makini wa chadema wataendelea kuuthibitishia umma kuwa walichaguliwa kwa umakini na wananchi hawakufanya kosa..
   
 9. p

  politiki JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Ringo, you are bettter than this!!
  Unajua vyema kuwa mahakama za Tanzania zinaendeshwa kisiasa mfano mzuri kesi ya mgombea binafsi ambayo jawabu lake lilikuwa wazi lakini unajua nini kilitokea. kesi ya kupinga matokeo ya Ubungo kati ya mnyika na mzee keenja ilichukua miaka mitano mpaka uchaguzi mwingine ukafika. Angalia hivi sasa kesi nyingi za uchaguzi zinazoendeshwa na za kutoka majimbo ya upinzani, kesi za wapinzani dhidi ya CCM zinahalishwa kisa hakuna pesa za kuendesha kesi. umeona JK anachokifanya kuwapa uanasheria mkuu na uenyekiti wa tume ya uchaguzi majaji ?? unafikiri lengo lake nini?? Hii ni rushwa ya kiana kwa majaji wote kuwa ukitubeba nawe tutakufanyia kama tulivyomfanyia huyu mwenzako. ni kama vile mwananchi wa kawaida anavyoonga pesa ili baadaye apewe anachokitaka lakini CCM inahonga vyeo kwa ajili ya ku buy favor on future issues. mfumo wetu umezichafua mahakama kutoka kwenye chombo huru cha kutoa haki na kuwa chombo cha watu wanaosubiria fadhila za wanasiasa kubadilisha maisha yao kwahiyo mpaka siku huo mlango utakapofungwa bila hivyo usitegemee majaji hawa wataisurubu serikali kwani wote wanasubiria kuwa m-kiti wa tume wanna be, mwanasheria mkuu wanna be na kadhalika.
  nawaunga mkono makamanda wote waliosema issue ya kulinda kura ndio eneo pekee la kufa nao wakikushinda hapo huko kwingine usitegemee kitu kwani wana control nako. nguvu zetu ni kwenye kampeni na kuhesabu kura ndio nguvu zetu zinapoishia kwahiyo tutumie nafasi hiyo vizuri badala ya kukimbilia mahakamani kufungua kesi ya kikatiba ambayo huenda ikasikilizwa 2014.
   
 10. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Pls Pls! Kauli mbiu ya Arumeru iwe ni kulinda kura! at all cost!
   
 11. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Hata Igunga Chadema ilifanya remarkable job bana,hatutakiwi kujibeza
   
Loading...