Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Ni bahati mbaya sana viongozi na wafuasi wa CHADEMA na upinzani kwa ujumla tunaonekana kunasa katika mtego huu wa CCM wenye lengo la kutuvuruga, kutogombanisha na zaidi kutufanya tutumie muda mwingi kujadili agenda na propaganda zinazobuliwa na CCM badala ya sisi kama upinzani kuibua madhaifu ya serikali hii ya CCM.
Tunachopaswa kutambua ni kuwa,hawa mabwana kwa sasa wameshagundua udhaifu wetu wa kujadili zaidi agenda ya hamahama wanayoiibua kila kukicha badala ya kutumia muda wetu kuibua na kujadili mambo mengi ambayo awamu hii imeshindwa kuyatekeleza pamoja na makosa waliyoyafanya.
Ndungu zangu,hata Lowassa kukubaliwa kwenda Ikulu kipind hiki inawezekana ni sehemu ya mkakati huu au muendelezo wa huu mkakati wa wao ku-set agenda na sisi tukabaki tunatumia muda mwingi kujadili agenda hizo badala ya kuwaeleza wananchi ni jinsi gani utawala huu unavyofeli katika mambo kadha wa kadha.
Je,leo hii Sumaye alielalamika kunyang'anywa mashamba yake akiitwa Ikulu kujadili kuhusu mashamba hayo unadhani atakataa?
Je,akiitwa Ikulu na kupewa habari za matumaini na kisha nae akasifia huu utawala,tutaanza tena kujadili mazunguzo ya Sumaye na Mkulu?Ita
kuwa ni akili tukaanza tena kuparuana kisa Sumaye kasifia huu utawala?
Viongozi wa CHADEMA na mashabiki wa upinzani ni bora tukapuuza hizi habari za hamahama au sijui nani kaenda Ikulu na badala yake tujikite kueleza mapungufu ya hii serikali na zaidi tupaze sauti kutetea wananchi.
Tutambue hii hamahama na watu kwenda Ikulu havitaisha leo wala kesho bali ni mambo yatakayokuwa yanafanywa kimkakati ili kututoa kwenye reli maana kama ni wa kuhama bado wako wengi na mkakati huu unaweza kuendelea mpaka 2020.
Ingekuwa ni busara na jambo la kimkakati kama leo mbunge au diwani wa CHADEMA anatangaza kujiuzulu na kuhamia CCM,kesho Tundu Lissu anakuja na barua au waraka kutoka Uturuki akielezea mkakati au mpango wa CHADEMA kwenda mahakani kufungua kesi kupinga makato ya asilimia 15 kwa ajili ya Bodi ya Mikopo.
Wakati wao wanatangaza kumpokea kiongozo kutoka upinzani,waziri kivuli wa utumishi anapanga kukutana na waandishi wa habari kueleza ni jinsi gani serikali hii imeshindwa kuboresha masilahi ya watumishi wa umma pamoja na kushindwa kulipa malimbikizo yao.
Wakati Mkulu anaibua kashifa mpya ya ufisadi,kiongozi wa kambi rasimi ya upinzani na mwenyekiti wa chama anaita waandishi na kueleza mlolongo wa kashifa na tuhuma kibao ambazo mpaka sasa hakuna mtuhumiwa hata mmoja alieshitakiwa mahakamani.
Si hivyo tu,wakati wao wanaendelea kujisifu kuongeza mapato,waziri kivuli wa elimu anaita waandishi wa habari na kuwaeleza idadi ya wanafunzi waliokosa mikipo au kupewa mikopo kiduchu pamoja na vigezo vipya vinavyowabana wanafunzi wengi kupata mikopo.
Badala ya kukaa na kujadili hamahama,CHADEMA kama chama huu ni wakati wa kutoa awareness kwa umma juu ya mapungufu yaliyoko katika mswaada unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni kuhusu kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii.
Wakati wao wanaendelea kuchukua madiwani wetu,sisi kama wapinzani ni wakati wa kuhoji hatima ya mazunguzo ya makinikia,kutaka mikataba ya ununuzi wa bombedier na ujenzi wa reli ya kisada iwekwe wazi/iwasilishwe Bungeni..
Wakati wanajinadi kuwa hii ni serikali ya wanyonge, ni wakati wa upinzani kuisuta hadharani serikali hii kwa kushindwa kutimiza ahadi ya kutoa milioni 50 kwa kila kijiji.
Jamani hii ndio kazi ya upinzani na si kujadili Lowassa kaenda Ikulu au sijui nani kahamia CCM kutoka upinzani.
CHADEMA imefika hapa ilipo kwa kupigania matatizo ya wananchi agenda ambayo sasa tumewekwa mtegoni ili tuitelekeze na tubaki kujadili hamahama,fulani kaenda Ikulu au mheshimiwa leo kaibua ufisadi fulani bandarini, n.k
Ndungu zangu, tunapotea na sasa ni bora turudi kwenye mstari kwa kuongelea zaidi agenda zinazogusa maisha ya wananchi wengi moja kwa moja kama kilimo,ajira,n.k. na kuionyesha jamii ni kwa kiasi gani hii serikali imekuwa mzigo kwa wananchi.
Pia tumeweka mkazo zaidi katika kuongelea maswala ya demokarasia, utawala bora, utekaji,n.k huku tukisahau matatizo mengine kama shida ya maji,umeme,n.k mambo ambayo yanagusa wananchi moja kwa moja
Tushituke huu ni mtego kwetu.