CHADEMA tumbo joto, ni kuhusu uhusika wao kwenye mlipuko!

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,818
WanaJF!

Mpaka sasa CHADEMA hawajatoa ushahidi wowote ule kuhusiana na tukio la Soweto, Arusha lililo husisha mlipuko wa bomu ambao umepelekea vifo kwa wahanga hao wa bomu na ulemavu wa kudumu kwa watanzania wasio na hatia.

Jambo ambalo CHADEMA wamelifanya ni kutoa tuhuma tu kwa askari wa jeshi la polisi kuwa askari huyo ndiye alie husika na kurusha bomu hilo, lakini HAWATAKI kuthibitisha tuhuma zao kwa kuwasilisha USHAHIDI wao usio na shaka kwa mamlaka zinazo husika.

Kwa mantiki hiyo; jeshi letu la polisi limeundiwa picha mbaya kwenye jamii pasipo kuwepo na USHAHIDI wowote kuhusu ushirika wake kwenye mlipuko, zaidi ya kuleta HADITHI za matumizi ya DVR na CCTV Camera kwenye mikutano ya CHADEMA kuwa imemnasa askari huyo akirusha bomu.

Aidha, kwenye jamii bado suala hili linazungumzwa, na sio watu wote kwenye jamii walio na imani juu ya tuhuma za MBOWE kwa jeshi letu, hivyo hata baadhi ya watu wamekuja na hisia zao kuwa wenda ni CHADEMA yenyewe ndio imefanya tukio hilo la mlipuko kwa 'SABABU' zifuatazo;

i)Ni mkakati wa viongozi wa CHADEMA kuhakikisha wanaunda tukio ambalo lingeweza kufanya uchaguzi uliopaswa kufanyika ndani ya CHADEMA hivi karibuni una hairishwa.

ii)Ni katika kuhakikisha uchaguzi una chelewa kwa kujua kabisa kama ukifanyika LAZIMA watashindwa, kwani wananchi wengi wa Arusha wamechukizwa na maamuzi ya viongozi wa CHADEMA ya kuwatimua MADIWANI ambao wananchi wanawapenda.

iii)Ni katika kutafuta huruma ya wananchi kwa CHADEMA ili basi itengenezwe picha kuwa CHADEMA ni chama TISHIO, hivyo maadui zake CHADEMA hasa CCM imeshindwa hoja imeamua kurusha mabomu.

iv)Ni mkakati wa CHADEMA kujitangaza kimataifa hasa kwenye zile nchi ambazo zina fadhili chama hicho ikiwemo GERMANY, ili wafadhili hao wazidi kutoa misaada kwa CHADEMA kwa huruma waliyo ijenga kwa chama hicho kufuatia mlipuko huo.

Ndugu wanaJF, hizi hisia si zangu, ila ni minong'ono ya wananchi kuhusu namna ambavyo wao wametafsiri tukio zima, kwa hali hii basi, ni vyema MBOWE akapeleka USHAHIDI kwenye mamlaka zinazo husika kwani hii mitazamo ina pelekea CHADEMA kuonekana kimeratibu tukio la MLIPUKO kwenye mkutano wake Soweto, Arusha.
 
Umekariri Mkuu,huu ni wakati wa DIGITALI!
Pamoja na hayo yote, bado wale ambao Hamy-D kasema tunanong'ona na katusikia, tunasubiri mwisho wa sarakasi hizi, tuone nani karuka sarakasi na taulo na ndani hajavaa ch.upi mbele ya wakwe na wanae.
 
Hivi tangu lini CHADEMA wamekuwa waoga kiasi hiki? Yaani CHADEMA wawe na ushahidi waa video halafu wasiiweke hewani!

Siamini!
 
hui ni upumbavu

Mkuu, upumbavu uko wapi hapo? Mbowe ashinikizwe awasilishe ushahidi ili taswira ya chama na jeshi letu la polisi ieleweke ipi ina staili kuchafuka. Kwa sasa sio jeshi wala sio CHADEMA ni wasafi kwenye jamii.
 
Haya si maoni yangu ni watu baki, wao hawana shida na ushahidi wowote, wanacholalamika ni kwanini serikali imeamua kuwamaliza, wanajuta sana CCM kuwa madarakani, kwani sanasema damu ya ndugu zao inathamani kuliko CCM.
Bwana mwingi akauliza hivi lile bomu lingemtungua rais, wangeshindwa kumkamata mtuhumiwa kwa sababu ya mawe ya wananchi?
 
Haya si maoni yangu ni watu baki, wao hawana shida na ushahidi wowote

Wananchi hawataki sarakasi wanachotaka ni kuuona huo ushahidi ambao Mh. Mbowe anadai anao. CHADEMA msitake kucheza na maisha ya watu wasio na hatia.

Kama Mh. Mbowe hatatoa huo ushahidi atatuambia alilisingizia Jeshi la Polisi kwa madhumuni gani.
 
WanaJF!

Mpaka sasa CHADEMA hawajatoa ushahidi wowote ule kuhusiana na tukio la Soweto, Arusha lililo husisha mlipuko wa bomu ambao umepelekea vifo kwa wahanga hao wa bomu na ulemavu wa kudumu kwa watanzania wasio na hatia.

.
waambie wenzako CCM mbona mnaogopa kuundwa kwa tume ya kijaji? ili mbivu na mbichi zijulikane?
 
Haya si maoni yangu ni watu baki, wao hawana shida na ushahidi wowote, wanacholalamika ni kwanini serikali imeamua kuwamaliza, wanajuta sana CCM kuwa madarakani, kwani sanasema damu ya ndugu zao inathamani kuliko CCM.
Bwana mwingi akauliza hivi lile bomu lingemtungua rais, wangeshindwa kumkamata mtuhumiwa kwa sababu ya mawe ya wananchi?
kama mbowe amekalia ushahidi jamii imueleweje? inamuona kuwa ni GAIDI TU. NA ATAPIGWA TU
 
Wananchi hawataki sarakasi wanachotaka ni kuuona huo ushahidi ambao Mh. Mbowe anadai anao. CHADEMA msitake kucheza na maisha ya watu wasio na hatia.

Kama Mh. Mbowe hatatoa huo ushahidi atatuambia alilisingizia Jeshi la Polisi kwa madhumuni gani.
mtaa wananchi wana panga jinsi ya kuwatoa madarakani, uongozi wa kipropaganda ni uongozi muflisi,
swala la kukamata watuhumiwa si la chadema ni swala la polic
 
Mkuu HAMY-D, Nakupongeza sana kwa uchambuzi wako. chadema walijua nini wanakifanya na hata Mheshimiwa Mwigullu Nchemba alibainisha kuwa kwa jinsi mazingira ya tukio lile ilivyokuwa chadema hawana pa kuchomoka
 
Mkuu hamy hawa jamaa hawana jipya na hawana la maana wanajitekenya na kucheka wenyewe.

Ngoma ya soweto wameipiga wenyewe na lazima waichezezi wao hawatafanya watanzania wajinga siku zote.

Siku zote huwezi kuwa mchafu halafu watu unawambia msafi na ile hali watu wanakuona wewe u mchafu kwa hiyo wafanye wafanyavyo lakini hawatoki.
 
Haya si maoni yangu ni watu baki, wao hawana shida na ushahidi wowote, wanacholalamika ni kwanini serikali imeamua kuwamaliza, wanajuta sana CCM kuwa madarakani, kwani sanasema damu ya ndugu zao inathamani kuliko CCM.
Bwana mwingi akauliza hivi lile bomu lingemtungua rais, wangeshindwa kumkamata mtuhumiwa kwa sababu ya mawe ya wananchi?

Tuwe wa kweli mkuu, uwezi kulinganisha ulinzi wa rais na raia wa kawaida, ndio maana umeona mwenyewe ulinzi ulivyo imarishwa kabla hata ya Obama kuwasili nchini. Hivyo, ingekuwa ni busara kwa wananchi wa Arusha badala ya kupiga polisi mawe, wao wangempiga huyo wanae dai amerusha bomu.
 
Back
Top Bottom