Wakati Chama chetu cha CHADEMA kitakaposhika dola 2015 kitaingia na sera mpya ya majimbo, na kimefafanua jinsi tawala hizo za majimbo zitakavyo kuwa kama ifuatavyo:
Nimeipenda sana sera hii kwani itakuwa ndio mwarobaini wa migogoro inayoendelea hasa ktk mikoa ya LINDI na MTWARA.
Lakini sasa baada ya kikao cha kamati kuu na baraza kilichokaa tar 26, 27 na 28 mwezi huu, kimekuja na mkakati mpya, kama Mwenyekiti wa chama anavyosema, "Tunataka tuishi vile tunavyosema kwa kuwa katika miaka mingi ya kuwa chini ya uongozi wa serikali ya CCM, wananchi wamekuwa wakiamriwa mambo yao na kundi dogo la watu wanaojikusanya sehemu moja ya nchi, hilo kwetu si mfano bora wa uongozi,"
Ukiusoma vizuri mkakati huu utagundua kuna mapungufu na pia unatofautiana kidogo na ule wa awali ambao chama kimeupendekeza uingizwe ktk Katiba mpya ya sasa na ndio sera itakayoingianayo mara kitakaposhika dola.
Kwanza wamesema kutakuwa na MAJIMBO / KANDA 10 ila zikiorodheshwa zinaonekana ziko 9 tu.
Pili, ktk mkakati huu mpya mkoa wa RUKWA umerukwa kwani hauonekani ktk orodha iliyotolewa, wakati ktk mkakati wa awali unaonesha mkoa wa RUKWA upo ktk Jimbo la Ziwa Tanganyika.
Pia mkoa wa Dar es Salaam ktk mkakati wa awali ulikuwa unajitegemea pekee kama Jimbo la Mji Mkuu ila sasa umechanganywa na PWANI na TANGA na kuitwa kanda ya MASHARIKI.
SASA SISI KAMA WANACHAMA WA CHADEMA NA WANANCHI, TUNATAKIWA TUSHIKE LIPI KAMA MSIMAMO WA MKAKATI MADHUBUTI WA CHAMA JUU YA SERA YA MAJIMBO NA KANDA?
TAWALA ZA MAJIMBO NA SERIKALI ZA MITAA
1. Nchi ya Tanganyika itagawanywa katika maeneo kumi ya kikanda yatakayojulikana kama Majimbo kama ifuatavyo:
(a) Jimbo la Nyanza Magharibi ambalo litaundwa na mikoa ya sasa ya Kagera, Geita na Shinyanga;
(b) Jimbo la Nyanza Mashariki litakaloundwa na mikoa ya sasa ya Mara, Mwanza na Simiyu;
(c) Jimbo la Ziwa Tanganyika litakalojumuisha mikoa ya sasa ya Kigoma, Katavi na Rukwa;
(d) Jimbo la Kati litakaloundwa na mikoa ya sasa ya Tabora, Singida, Dodoma na Iringa;
(e) Jimbo la Kaskazini litakaloundwa na mikoa ya sasa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara;
(f) Jimbo la Pwani ya Kaskazini litakaloundwa na mikoa ya sasa ya Tanga, Wilaya za Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Kisarawe na Mkuranga katika Mkoa wa sasa wa Pwani na Wilaya za Gairo, Kilosa, Mvomero, Morogoro na Kilombero katika Mkoa wa sasa wa Morogoro;
(g) Jimbo la Mji Mkuu wa Dar es Salaam;
(h) Jimbo la Pwani ya Kusini litakaloundwa na mikoa ya sasa Lindi, Mtwara na Wilaya za Rufiji na Mafia katika Mkoa wa sasa wa Pwani, na Wilaya ya Ulanga katika Mkoa wa sasa wa Morogoro;
(i) Jimbo la Nyanda za Juu Kusini litakaloundwa na mikoa ya sasa ya Mbeya, Njombe na Ruvuma;
2. Majimbo yataongozwa na Gavana atakayechaguliwa moja kwa moja na wananchi katika Jimbo husika.
3. Miji, manispaa na jiji ndani ya majimbo itaongozwa na Meya atakayechaguliwa moja kwa moja na Wananchi katika Mji husika;
Nimeipenda sana sera hii kwani itakuwa ndio mwarobaini wa migogoro inayoendelea hasa ktk mikoa ya LINDI na MTWARA.
Lakini sasa baada ya kikao cha kamati kuu na baraza kilichokaa tar 26, 27 na 28 mwezi huu, kimekuja na mkakati mpya, kama Mwenyekiti wa chama anavyosema, "Tunataka tuishi vile tunavyosema kwa kuwa katika miaka mingi ya kuwa chini ya uongozi wa serikali ya CCM, wananchi wamekuwa wakiamriwa mambo yao na kundi dogo la watu wanaojikusanya sehemu moja ya nchi, hilo kwetu si mfano bora wa uongozi,"
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepitisha mpango mkakati wake wa kuelekea kushika dola mwaka 2015 kwa kumega madaraka ya makao makuu katika kanda kumi. Maazimio hayo yalipitishwa na Kamati Kuu (CC) juzi kwa agenda moja kubwa ambayo ni kupitisha mpango mkakati wa mwaka 2013 ili kushinda chaguzi zote kuanzia serikali za vitongoji, vijiji na mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu 2015.
Akizungumza na wajumbe wa kikao cha dharura cha Baraza Kuu jana, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kuwa mpango mkakati huo umelenga kufanya mabadiliko ya uongozi kuanzia ngazi ya taifa kwenda katika majimbo na kukipanga upya chama hicho kwa mustakabali wa taifa. "Mtakumbuka kwamba wakati tunakianzisha chama chetu, tulizungumzia sera ya majimbo na kuainisha kazi zake…sasa tumeanza kupanga kazi zenyewe kwa kugawa majukumu katika kanda kumi. "Tunataka tuishi vile tunavyosema kwa kuwa katika miaka mingi ya kuwa chini ya uongozi wa serikali ya CCM, wananchi wamekuwa wakiamriwa mambo yao na kundi dogo la watu wanaojikusanya sehemu moja ya nchi, hilo kwetu si mfano bora wa uongozi," alisema.
Mbowe aliongeza kuwa katika miaka 20 ya kuhimili misukosuko ya kisiasa chama hicho kimejifunza mengi na sasa kiko tayari kushika dola ndio maana wameanza kugawa majukumu kwa wananchi kupitia uongozi wa kikanda. Alisema kuwa wamejiandaa kwa mashambulizi ya aina zote na sasa jukumu kubwa la kila kanda litakuwa ni kuhakikisha kila mwananchi anaiunga mkono CHADEMA katika eneo atakalokuwa.
Mwenyekiti huyo alitaja kanda hizo na mikoa husika kuwa ni
1. Kanda ya Ziwa Magaharibi (Mwanza, Geita, Kagera),
2. Ziwa Mashariki (Mara, Simiyu, Shinyanga),
3. Ziwa Magharibi (Kigoma, Tabora, Katavi)
4. Kati (Singida, Dodoma, Morogoro).
5. Nyanda za Juu Kusini (Mbeya, Ruvuma, Iringa),
6. Kusini (Lindi na Mtwara),
7. Mashariki (Pwani, Dar es Salaam na Tanga),
8. Kaskazini (Kilimanjaro, Manyara, Arusha),
9. Pemba na Kanda ya Unguja.