CHADEMA tishio

CHADEMA tishio

Django

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
354
Reaction score
147
KASI ya kuimarika na kushamiri kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kila kukicha kunakotokana na kukubalika kwake kwa wananchi, kumekuwa tishio kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hali ya mambo inaonesha kuwa, kitisho hicho ndicho kinainyima usingizi CCM na serikali yake, hivyo kupanga na kuibua vituko dhidi ya CHADEMA ili kukidhoofisha na kukipaka matope mbele ya wananchi.

Vituko na mikakati hiyo imezidi kushika kasi ambapo safari hii, makada watano wa chama hicho wameshtakiwa kwa kosa la ugaidi, ukiwa ni mwendelezo na sehemu ya mkakati huo kwa kutumia njia mbalimbali.

Kosa kama hilo pia alishtakiwa nalo Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare, hivi karibuni, lakini Mahakama Kuu ilimfutia shtaka hilo.

Wakati makada hao wameshtakiwa kwa ugaidi, kosa ambalo halina dhamana, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Tundu Lissu na Godbless Lema wamezuiwa kuingia bungeni.

Hata hivyo, matokeo ya kiwewe cha CCM dhidi ya CHADEMA, yamewahi kukipata Chama cha Wananchi CUF kuelekea uchaguzi wa mwaka 2005, baada ya kuonekana ni tishio dhidi ya CCM.

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Omari Mahita, aliibua tuhuma nzito dhidi ya CUF kuwa waliingiza nchini shehena ya majambia, hivyo ni chama hatari, doa ambalo kwa kiasi kikubwa lilikiathiri chama hicho.

Safari hii, hila hizo zinaelekezwa kwa CHADEMA kinachoonekana ni tishio kwa utawala wa CCM na serikali yake ambapo jana makada wake wameshtakiwa kwa ugaidi.

Mbowe, Lissu, wazuiwa

Licha ya kanuni za Bunge kuruhusu vazi la safari suti yenye mshono kama kombati zinazovaliwa na baadhi ya wabunge wa CHADEMA, kwa mara ya kwanza Kiongozi wa Upinzani, Freeman Mbowe na wenzake watatu jana walizuiwa kuingia bungeni.

Mbowe na Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini) na Ezekiel Wenje (Nyamagana) walizuiwa na askari kwa madai kuwa wamevalia sera za chama.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni katika viwanja vya Bunge, Lissu alisema walishangazwa na uamuzi huo wakati mavazi hayo wamekuwa wakiyavaa na kuingia nayo bungeni kwa miaka mingi sasa.

Lissu alisema kuzuiwa kwao wanakuchukulia kuwa ni mkakati maalumu wa serikali ya CCM kutaka kuwazima na kuhakikisha hawapati nafasi ya kuingia bungeni ili wasijibu mashambulizi ya tuhuma wazosingiziwa kuhusiana na mlipuko wa bomu jijini Arusha.

"Sisi hali hiyo tulianza kuishtukia tangu asubuhi tulipoingia kwenye eneo la Bunge, kama mligundua kulikuwa na askari wengi sana kila kona kuliko kawaida kana kwamba nchi imepinduliwa. Kinyume cha utaratibu na kanuni, askari wa kawaida wameingiza hadi bungeni.

"Tulipofika wakati wa kuingia ukumbini mimi, Mbowe, Lema na Wenje tuliambiwa haturuhusiwi kwa kuwa tumevaa sare za chama. Tulipouliza nani kawapa maagizo hayo walidai ni uongozi wa juu, yaani Spika wa Bunge," alisema Lissu.

Aliongeza kuwa kitendo hicho ni kichekesho kwani wakati wote tangu mwaka 2010 Mbowe amekuwa akivalia vazi hilo, achalia mbali wabunge wenzake baadhi ambao mara moja moja nao walikuwa wakivaa suti hizo lakini hawajawahi kuzuiwa.

Hata hivyo, pamoja na uamuzi huo, kanuni za Bunge hakuna mahali zinazuia mbunge kuvaa sare ya chama chake isipokuwa kanuni limeainisha aina za mavazi ya kuvaliwa na wabunge wanawake na wanaume.

Kwa mujibu wa kanuni ya 149 (3)(a) Kwa wanawake na (b) Kwa wanaume inasema: (a) Kwa wanawake;- (i) Vazi lolote la heshima yaani ambalo si la kubana mwili, lisiloonesha maungo ambayo kwa mila na desturi za Kitanzania hayapaswi kuoneshwa na ni refu kuvuka magoti.

(ii) Gauni la kitenge au blauzi inayovaliwa na kitenge au sketi ya rangi yoyote (iii) Kilemba cha kadiri au mtandio (iv) Suti ya kike; au (v) Vazi linalovaliwa wakati wa eda.

(b) Kwa wabunge wanaume;-(i) Suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baragashia; (ii) Vazi la kimwambao yaani ka nzu rasmi na nadhifu, koti, baraghashia na makubadhi au viatu; (iii) Suti kamili ya Kimagharibi ya rangi kadiri isiyomeremeta; (iv) Koti aina ya blazer na tai, pamoja na suruali yoyote ya heshima; au (v) Tarbushi na kilemba cha Singasinga, au kilemba chochote kinachovaliwa kwa mujibu wa masharti ya imani au mila.

Wasusia kupitisha bajeti

Akizungumzia kuhusu uamuzi wa wabunge wao kutoingia bungeni kupitisha bajeti ya serikali kwa mwaka 2013/14, Lissu alisema baada ya kukutana na kujadiliana kwa kirefu hawakuona sababu ya kuingia.

"Tukio la bomu kwa wafuasi wetu jijini Arusha halikuwa la bahati mbaya lakini tumejiuliza ni kwanini Bunge halikuahirishwa walau kwa siku moja kama ilivyo utamaduni ili kushiriki kuomboleza msiba huo," alisema.

Alisema kuwa pamoja na kwamba kiongozi wao wa kambi, Mbowe na Lema ndio walikuwa wamelengwa kulipuliwa lakini wakarusurika, Spika wa Bunge na Waziri Mkuu hakuna hata mmoja aliyetuma salamu za pole kwa viongozi hao.

"Waliolengwa kulipuliwa ni Mbowe, Lema na James ole Millya, lakini hata risasi zilizowaua wale wafuasi wetu wanne zilikuwa zikielekezwa kwa viongozi wetu.

"Sasa tunajiuliza, Bunge limeona waliokufa Arusha ni Watanzania lakini kwa vile walikuwa kwenye mkutano wa CHADEMA haiwahusu, hivyo kama wanajifanya kama hakuna kilichotokea sisi tunaingia ndani kufanya nini?" alihoji.

Lissu alitaja sababu nyigine kuona siku zote kila unapotokea msiba mkubwa wa wananchi wakati Bunge likiendelea, wamekuwa wakitumwa wawakilishi lakini kwa tukio la Soweto, Arusha Bunge halikutuma mwakilishi.

Alifafanua kuwa sababu kubwa iliyowafanya wafikie uamuzi huo ni kutokana na hatua ya Spika wa Bunge kupindisha ratiba ya Bunge ili kuwanyima nafasi wasijadili bajeti hiyo, hivyo kuhoji wanakwenda kupitisha kitu gani ambacho hawakushiriki.

"Hatukuweza kuwasilisha maoni ya kambi kutokana na tukio la Arusha lakini kulingana na ratiba tulimaliza mazishi Ijumaa tukijua kabisa Jumatatu tungepewa muda wetu wa nusu saa kuwasilisha maoni ya kambi.

"Si hivyo tu, bali hata wale walioomba kuchangia wangepata nafasi ya kuchangia halafu Jumanne bajeti hiyo ingepitishwa kwa mujibu wa ratiba. Lakini kutokana na hofu kuwa tungejibu mapigo kuhusu madai ya Arusha waliamua kufanya mbinu za kutunyima nafasi," alisema.
Source; Tanzania Daima
 
Back
Top Bottom