CHADEMA si CHADEMA tena

Alichokiandika mtoa mada hakipo mbali na ukweli isipokuwa tu ameileta habari yake kwa mtindo wa KISHAMBENGA......

Lakini hata kwa kutazama tu ni wazi kuwa CHADEMA kuna tatizo la kiuongozi......
 
Usikonde hamia CCM/CUF Lipumba uwahi ruzuku.
 
Atuelewi yani ata ifanyanye tunaipenda tuuuh


iPhone 7 /A1786)
 
Ni kawaida ya Mwanamke kuongea saaaana! bila shaka uzi huu utakua umeandikwa na kina mama au mwana mama flani ivi. Kazi yao kupiga kelele bila hoja ya msingi.
Tena usirudie chadema si chama cha mashangingi sasa ilo neno la kindaki ndaki umelitoa wapi? we ni shangingi wa Nyinyiem Pandikizi la chama. stay tune mbwa wenye njaa 2020 wajiandae kula nyama ya sumu. Kuna usemi unaosema mwanaume lijali uumia kwaajili ya familia yake lakini mwanaume fala Ujitesa kwa furaha ya kahaba wake aliyekundini aepuke kutumika na ajali kujituma.
 
Duh! kumbe hali ni tete kiasi hiki.
 
Nilidhani ni mimi tu naluona hilo, watu wanafikiri Lissu ana baraka zote za Chadema. Jiulize mara ya mwisho umemuona Lissu na Lowassa meza moja ni lini? Na wasiwasi kabla ya 2020 Lissu anaweza kuwa na chama chake kama Chadema watamletea zengwe.
 
inafika wakati hata Lisu simwamini kama kweli ni mpinzani? huenda anaigiza tu. watu hawawezi kukubali kirahisi hali ilivyo hasa wenye chama lakini kuna kila dalili hizo ndio rangi za hicho chama kwa sasa.
lakini hii imetokana na ubinafsi na kufikiri kuwa demokrasia inaweza jengwa na fedha.
ok haijalishi tumeshakosea ila tukubali na kujipanga
 
Chadema zamani, siku hizi kila mtu Kambale ana ndevu.
 
Nianze kwa Kutoa pole kwa jumuiya nzima ya wanasheria nchini, pole yangu sio ya tukio la IMMA advocates, Bali pole yangu ni ya kuchagua Rais wa TLS Chama Chenu 'MAHIRI' cha wanasheria Tanganyika - TLS Ndugu Tundu Lissu ambae AMEDHIHIRISHA kuwa ameanza Rasmi Safari ya Kuizika TLS, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari kuhusiana na Tukio la IMMA advocates.
Nianze kwa kuweka msingi wa HOJA yangu kuwa sifurahishwi na kilichotokea kwenye IMMA advocates, ila pia SIFURAHISHWI zaidi na "AKILI NDOGO" za Rais wenu katika hatua za AWALI za kushughulikia suala hili.

Mimi ni Profesional communicator kama mwandishi wa Habari, na Nyinyi wanasheria ni Profesional kwenye Sheria, ukisoma na Kusikiliza kwa umakini TAARIFA ya Mhe Rais wa TLS utagundua makosa makubwa sana ya KIUFUNDI ambayo yanaifanya taarifa nzima kuwa kama taarifa ya Mfalme "****" na kwa sisi MAFUNDI wa taarifa tunasema taarifa ikikosewa katika UANDAAJI na UWASILISHWAJI inakuwa imekosa MASHIKO, na hivyo taarifa nzima kuwa BATILI.

KWANINI BATILI
1. Taarifa iliyowasilishwa na Rais wa TLS tayari kwa kiasi kikubwaa ilishatolewa na Chama cha wananchi CUF [HASHTAG]#teammaalim[/HASHTAG], ukisoma taarifa ya cuf ambayo ilitoka siku moja kabla ya hii ya Rais utaona nachosema, ila hii ya Rais imewaka mbwembwe ya Vifungu Vifungu vingi vya SHERIA tu, ila taarifa zote zimeonyesha kuwa IMMA advocate ni WABIA katika kazi mana cuf inatetewa na IMMA advocate na Rais Lissu anatetewa na IMMA advocate hivyo wote WANAOMBELEZA DHORUBA YA MMBIA WAO., japo TLS ni Chama na Lissu ni Rais, na ni mteja wa IMMA katika hoja hii ya kwanza nimalizie kwa kusema tu Hoi taarifa ni BATILI kwa kuwa Imekuwa taarifa ya KISIASA na Imetolewa na wanasiasa wa vyama viwili tofauti, japo Mmoja ni Rais wa TLS, hapa utaona sasa Hatari ya kuwa na Rais wa TLS ambae ni mwanasiasa.

2. Taarifa ni BATILI kwa kuwa imeanza kwanza kwa KUHUKUMU kuwa Ofisi za IMMA advocate zimepigwa BOMU na POLISI, japo hizi ni taarifa za AWALI lakini kwa maoni yangu TAARIFA haikupaswa kujielekeza kwenye kazi za mamlaka nyingine, mana kama mmeshajua waliolipua ni POLISI basi hamkuitaji kutoa taarifa Bali kufuata SHERIA kuwashtaki POLISI.
Katika hoja hii MWENDELEZO wake inasema wanavitaka vyombo husika wakiwemo "WATUHUMIWA" Polisi kufanya uchunguzi, mbele zaidi tena wanataka kukutana na "MTUHUMIWA" boss wao IGP, hivi hii ni SAWA WANASHERIA, mnataka kukutana kufanya nini tena na IGP au mkurugenzi wa usalama wa taifa ambae majuzi juzi hapa wakati wa Sakata la Bombadier Rais "WENU "alishema kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa" ANAMFUATILIA FUATILIA "sasa iweje Leo aombe mwenyewe kukutana na" MTESI " wake, NDIO MANA NASEMA HAPA KUNA TATIZO YA HIKI CHAMA KUONGOZWA NA MWANASIASA, labda niwakumbushe tu hawa wanasiasa enzi ya Lowassa Walisema" mwizi" alipokwenda kwao wakamuita mfalme wa AMANI hawa ndio wana SIASA.

3. Taarifa ni BATILI, kwa sababu taarifa inataka WANASHERIA kugoma jumanne na jumatano, huu ni MGOMO ambao katika taarifa yao wanaomba ufanywe UCHUNGUZI, lakini pia kwenye taarifa yao wanaomba kuonana na kaimu Jaji Mkuu ambae mmekuja kusema tena hapo Chini ASUSIWE hamtaki kwenda kwenye mahakama anazoziongoza, JAMANI mnajua mnachofanya? Hii ni sawa na KUJITEKENYA MWENYEWE KISHA UKACHEKA MWENYEWE. nadhani Wasomi wana Sheria tukubaliane katika jambo moja MGOMO au KUONANA na "WATESI "wenu huwezi kushika mambo mawili kwa wakati Mmoja lazima MOJA litaponyoka.

4. Hii taarifa ni BATILI, kwa sababu imemtangaza MGOMO pasipo kusema ADUI ni Nani, hivi Hebu tuambieni mnagoma mkilenga KUMUUMIZA Nani? Kuwaumiza wateja wenu walioko MAGEREZANI au? Hivi nyinyi hii kazi ya UANASHERIA ni ya kujitolea katika kazi zenu zote? Hivi hakuna pesa mmechukua za wateja wenu ambazo mnapaswa kuzifanyia kazi, au TUSEME na nyinyi "WEZI" mnachukua hela za wateja wenu kisha mnagoma?
Hebu mtuambie Nani ADUI YENU basi.

MASWALI MAGUMU ZAIDI TLS.

1. Hivi Mbona walipouwawa *WANASHERIA* na *MAWAKILI* nguli nchini, tena waliowasomesha na kuwafundisha *HAMKUGOMA KUSHINIKIZA HAKI ITENDEKE KAMA HIVI LEO,* au mmesahau Vifo vya *"UTATA"* vya Mawakili Marehemu Kapinga, Marehemu Mvungi, Marehemu Mwaikusa? Kwa kuwa mnasahau ngoja tuwakumbushe tu *HAKUNA NAMNA*, Leo hao wazee wamekuwa *"LIABILITY"* kwenu halafu cuf, Lissu, acaccia zimekuwa *"ASSET"*kwenu?

2. Hivi tangu lini mmeanza kushirikiana press releases na vyama vya siasa mfano cuf?

3. Hivi TLS kimekuwa Chama cha Siasa, au kwakuwa Rais wenu ni mwanasiasa?

4. Mnawezaje kuitenganisha TLS na siasa?

5. Katika Sheria kuna neno linaitwa *"INNUENDO"*hivi mnajua maana ya hilo neno katika Sakata hili la IMMA advocate?

6. Hivi mnajua IMMA advocate ni kampuni "inayotajwa" KUCHOTA mabilioni ya fedha za EPA kupitia kampuni ya DEEP GREEN kiasi cha *BIlioni 8* zilichotwa, mnajua hilo? kama hamjui nendeni Brella kisha mkasome anuani za Kampuni ya *DEEP GREEN,* kisha mtangaze *MGOMO.*

7. Hivi mnajua huyu Rais wenu Lissu akiwa Bungeni mwaka 2012 Aliitaja kampuni ya IMMA advocate kuwa ilizitetea kampuni za TanGold na Deep green microfinances *KUCHOTA* pesa za EPA, halafu Leo HAWAHAWA imma advocate ndio wanaomtetea Lissu katika kesi zake?

Hivi mnajua maana ya vita ya *KIUCHUMI,* adui yako anaweza kutumia *MKEO, WATOTO* na hata Ndugu zako ili mradi *APATE USHINDI.*

Mwisho, Nawapenda sana *WANASHERIA,* mana najua mchango wao katika taifa la Tanzania, nawathamini sana Wanasheria wamaotanguliza *UZALENDO* kwa taifa Lao pamoja na changamoto tunazopitia kama taifa Changa, Nawapenda Wanasheria wanaosem *KWELI* kwa maslahi ya taifa Lao na Sio *MATUMBO* yao.

Sasa Sikilizeni, *AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO.LEO TUNDU, TUNDUNI.*

Wasalamu
*Jerry C. Muro*
*28/08 /2017*
 
Wenye akili hawawezi furahi pale chama cha upinzani kinapoanza kurumbana.

Lakini wenye busara hawawezi vumilia kuona chama cha siasa kinafanya mambo ya ovyo kama CCM YA KIKWETE.
 
JERRY MURO ha ha ha ha
 
Mimi kama mkereketwa wa sera za upinzani leo najitokeza hadharani kuhoji hiki kinachoendelea ndani ya CHADEMA.

Kabla ya ujio wa Edward Lowassa, CHADEMA tulitamba sana kwa kutetea wananchi masikini, siku zote tulitetea wamachinga, mama ntilie, wakulima, na wafugaji. Mitaani CHADEMA tulikuwa na mvuto wa kipekee kwa sababu ya hoja na sera zetu za kuifikirisha serikali.Tulikuwa ukivaa magwanda na kupita nayo mtaani unashangiliwa kila kona.

Mara baada ya Edward Lowasa kujiunga chadema, mambo mengi yamebadilika ndani ya chama. CHADEMA ya leo haina mvuto kwa wananchi kabisa, hata ukivaa magwanda na kupita nayo mtaani unaonekana kama lofa fulani tu.
Kwa nini imekuwa hivi?

1.Ni kwa sababu CHADEMA ya leo si mtetezi wa wanyonge tena. Watu maskini wanabomolewa nyumba zao lakini hutasikia wakiwatetea .
CHADEMA ya leo ni rafiki na mtetezi wa wakwepa kodi, wauza madawa, wala rushwa, majangili na wachawi.

2. Imezuka falsafa mpya ndani ya CHADEMA kuwa chama ni watu, kwa hiyo ili mradi tu wewe ni mtu hata kama ni fisadi, mchawi, mkwepa kodi, muuza madawa ya kulevya na mchawi njoo CHADEMA utapokewa.

Je maadili na miiko ya CHADEMA imeenda wapi?

Kutokana na sababu hizo hapo juu nimeamua kutema nyongo kwa Edward Lowassa aturudishie chama chetu, hii siyo CHADEMA tuliyoizoea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu si lowasa tatizo ni yule mkulu kuzuia kila kitu kama mikutano ambayo ndio kero za wananchi walikuwa wanatoa duku duku zao.

Leo wanataka kuwa na gap kubwa katikati hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…