CHADEMA shughulikieni Mwigulu Mchemba anawachafua

CHADEMA shughulikieni Mwigulu Mchemba anawachafua

Mi nawashauri wawtahadharishe hao Wameru kwamba huyu jamaa ni mbaya sana kwa wake za watu, hivyo wasiwaruhusu wake zao kuhudhuria mikutano anayohutubia lasivyo atabaka mke wa mke halafu washili wazidi kulia kila siku kwa uharibu utakaotokea.

Je unafahamu CV yake akiwa kule chuo cha Ualimu? kama kapitia ualimu na aliiva basi anene siasa za kweli na si udanganyifu wa namna ile.Alikera wengi sana hususani kwenye mf wa manati na nembo ya CDM
 
Kwenye power breakfast kwenye dondoo za magazeti Mwigulu mchemba anasemekana amewaambia wakazi wa Mbuguni kwamba CHADEMA wamemwambia hawahitaji jimbo la Arumeru bali wanajenga Chama kitu ambacho kila mtu anajua ni uongo mtupu. amewadanganya wananchi hao kwamba CHADEMA hata ikishinda jimbo mbunge wake hataweza leta maendeleo yoyote kwani chama kilichoko madarakani ni CCM na hivyo mbunge wa CHADEMA akishinda ni sawa na kutokuwa na Mbunge.

Hii hoja hata mimi binafsi nimemsikia Mchemba akiongea kwenye kampeni na ni hoja potofu na inabidi CHADEMA waivalie njuga kumkomesha huyu mpotoshaji mkubwa. Mbunge inajulikana ni mwakilishi wa wananchi awe CDM, CUF, TLP au CCM na wananchi wanamchagua kidemokrasia kwa kuona ni mbunge kutoka chama gani anayewafaa zaidi na kwamba vyama vinavyogombea ubunge vipo kisheria kwa maendeleo ya wananchi. Iweje mchemba avuruge wananchi kwa kauli za uongo halafu anaachwa. Mbona kuna maeneo mengi wabunge wanatoka vyama vya upinzani na shughuli za kimaendeleo zinafanyika.

Basi mchemba aeleze ni kifungu gani katika katiba ya Jamhuri ya Tanzania kinachosema mbunge kutoka upinzani akiomba fungu la maendeleo la wilaya hatapewa mpaka atoke cham tawala. ijulikane na wanachi waambiwe kuwa fedha za shughuli za maendeleo ya majimbo na sehemu yoyote nchini hazitoki katika mfuko wa CCM bali serikalini zikiwa zinatokana na kodi za watanzania ambao ni kutoka vyama vyote. Mchemba atuambie ni CCm inatoa fedha za shughuli za maendeleo au serikali?. Ninavyojua CCM wana hali mbaya kifedha hata ya kujiendesha inapatikana kwa manati je iweje Mchemba adanganye wananchi kwa kauli za uongo tena majukwaani halafu anaachwa?

Atuambie kama walipa kodi wamegawanywa kiitikadi ya vyama vingi hadi aseme CDM haitaleta maendeleo Arumeru kwa sababu walipa kodi wa CHADEMA ni wachache?

Hizi kauli za kihuni, kejeli na kupotosha zinatakiwa zisisikike tena na CDM kama mlivyomjibu Mkapa kwa habari ya Vicent nyerere pambaneni na huu upotoshaji.

Mchemba ni MHUNI NA ANATAKA KUFANYA KAMPENI ZA KIHUNI NA ASIVUMILIWE

Kampeni zikifanyika kistaarabu CDM lazima waibuke washindi tu

Kauli za Mwigulu zinatia shaka uwezo wake wa kufikiri na kujenga hoja...kama tuna ziongozi aina ya Mwigulu bungeni tutegemee ujinga na upumbavu ndio vitajaa bungeni...
 
hao ndo magambaz,

kumbuka hata kamanda Mbowe

aliwaomba wanaarumeru mashariki

wampe Nassari jimbo sababu mbunge mmoja

wa Chadema ni sawa na wabunge 30 wa magamba

ndo dizaini ya mwigulu,lusinde,maji marefu.........

endeleza idadi
 
DUH, HII IMENIKUMBUSHA MWAKA 2005, NILIKUWA SAME KULE KWA MAMA KILANGO, NIKAMKUTA MGOMBEA UDIWANI WA CCM AMBAYE KAISHIA FORM 2 ANAWATISHIA WATU KUWA WAKICHAGUA UPINZANI HAWATALETEWA MAENDELEO. NIKAAMUA KUMTOLEA UVIVU LIVE BILA CHENGA KWA HOJA MPAKA AKASHINDWA KUSIMAMA.
Akanong'onezwa kuwa yule jamaa yuko chuo kikuu, ndo akasimama babu mmoja akaanza kujidai alisoma na yeye middle school.
Jamani hawa jamaa dawa yao wasomi tuu. Ndo maana CCM wanaringa na ujinga wa waTZ kule vijijini
 
Kwenye power breakfast kwenye dondoo za magazeti Mwigulu mchemba anasemekana amewaambia wakazi wa Mbuguni kwamba CHADEMA wamemwambia hawahitaji jimbo la Arumeru bali wanajenga Chama kitu ambacho kila mtu anajua ni uongo mtupu. amewadanganya wananchi hao kwamba CHADEMA hata ikishinda jimbo mbunge wake hataweza leta maendeleo yoyote kwani chama kilichoko madarakani ni CCM na hivyo mbunge wa CHADEMA akishinda ni sawa na kutokuwa na Mbunge.
Kuna msemo unasema usihangaike na mbwa ongea na mwenye mbwa, kwa hiyo CDM imeanza kumshughulikia Mkapa hao wengine ni wadogo sana.
 
Mwigulu ni vuvuzela! Hakuna mtu Chadema anayeweza kupoteza muda kujibizana na Vuvuzela!! Kazi ya vuvuzela unaijua? Baada ya mechi hutupwa hadi mechi nyingine!!! Mwigulu kiazi tu!

Huyu namfananisha na mtu anayemshikia mwenzake pembe na wengine wanakamua maziwa naye kuambulia michubuko kutokana na kujeruhiwa na Pembe.

Huyu anatumika na akishawatengenezea wenzake njia anatupwa nje kama naniii.............
 
Back
Top Bottom