CHADEMA shughulikieni Mwigulu Mchemba anawachafua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA shughulikieni Mwigulu Mchemba anawachafua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Kwetu, Mar 15, 2012.

 1. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 60
  Kwenye power breakfast kwenye dondoo za magazeti Mwigulu mchemba anasemekana amewaambia wakazi wa Mbuguni kwamba CHADEMA wamemwambia hawahitaji jimbo la Arumeru bali wanajenga Chama kitu ambacho kila mtu anajua ni uongo mtupu. amewadanganya wananchi hao kwamba CHADEMA hata ikishinda jimbo mbunge wake hataweza leta maendeleo yoyote kwani chama kilichoko madarakani ni CCM na hivyo mbunge wa CHADEMA akishinda ni sawa na kutokuwa na Mbunge.

  Hii hoja hata mimi binafsi nimemsikia Mchemba akiongea kwenye kampeni na ni hoja potofu na inabidi CHADEMA waivalie njuga kumkomesha huyu mpotoshaji mkubwa. Mbunge inajulikana ni mwakilishi wa wananchi awe CDM, CUF, TLP au CCM na wananchi wanamchagua kidemokrasia kwa kuona ni mbunge kutoka chama gani anayewafaa zaidi na kwamba vyama vinavyogombea ubunge vipo kisheria kwa maendeleo ya wananchi. Iweje mchemba avuruge wananchi kwa kauli za uongo halafu anaachwa. Mbona kuna maeneo mengi wabunge wanatoka vyama vya upinzani na shughuli za kimaendeleo zinafanyika.

  Basi mchemba aeleze ni kifungu gani katika katiba ya Jamhuri ya Tanzania kinachosema mbunge kutoka upinzani akiomba fungu la maendeleo la wilaya hatapewa mpaka atoke cham tawala. ijulikane na wanachi waambiwe kuwa fedha za shughuli za maendeleo ya majimbo na sehemu yoyote nchini hazitoki katika mfuko wa CCM bali serikalini zikiwa zinatokana na kodi za watanzania ambao ni kutoka vyama vyote. Mchemba atuambie ni CCm inatoa fedha za shughuli za maendeleo au serikali?. Ninavyojua CCM wana hali mbaya kifedha hata ya kujiendesha inapatikana kwa manati je iweje Mchemba adanganye wananchi kwa kauli za uongo tena majukwaani halafu anaachwa?

  Atuambie kama walipa kodi wamegawanywa kiitikadi ya vyama vingi hadi aseme CDM haitaleta maendeleo Arumeru kwa sababu walipa kodi wa CHADEMA ni wachache?

  Hizi kauli za kihuni, kejeli na kupotosha zinatakiwa zisisikike tena na CDM kama mlivyomjibu Mkapa kwa habari ya Vicent nyerere pambaneni na huu upotoshaji.

  Mchemba ni MHUNI NA ANATAKA KUFANYA KAMPENI ZA KIHUNI NA ASIVUMILIWE

  Kampeni zikifanyika kistaarabu CDM lazima waibuke washindi tu
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mwanasiasa lazima awe na ngozi ngumu-SAMWEL SITTA. Chadema waelezeni wananchi mtawafanyia nini badala ya kuhangaika na Mwigulu, Mkapa na wengine. Mnajulikana Sera yenu kuu ni kuuponda uongozi wa CCM sasa mambo kama hayo wananchi wameshayachoka. Tunataka sera kwa maendeleo ya wana-Arumeru na Watanzania kwa ujumla siyo majungu, kashfa na chuki binafsi. wewe kwa mawazo yako unafikiri njia nzuri ya kumdhibiti mwigulu ni nini kumtukana majukwaani? Kumpelekea Makamanda wamvae? Kumwagia tindikali? au kumwaga sera za nini mtawafanyia wana arumeru? CHADEMA angalieni sana.
   
 3. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 60
  Taratibu za kisheria zifuatwe kumshughulikia kwa sababu kuwadanganya wananchi kwa lengo la kupata kura huku ukiwachafua wenzako siyo sahii. aeleze jinsi CCM itakavyofanya na siyo kusema uongo kwamba amefanya mazungumzo na CHADEMA wakasema hawataki kushinda bali kujenga Chama. CHADEMA wamwulize hayo mazungumzo wamefanya naye wapi kama si upotoshaji?
   
 4. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huenda huna mda wa kuwasikiliza au uko kiitikadi zaidi!
  kupitia vyombo vya habari nimemsikia Nasari akiwaahidi wana Arumeru kupigania upatikanaji wa ardhi,kuboresha huduma za afya, kushughulikia tatizo kubwa la maji liliko Arumeru,kuboresha elimu kwani ufaulu uko chini, kuboresha taratibu za kulipia ushuru wa soko kwa biashara ndogo ndogo,ujenzi wa barabara zinapitika kwa taabu.
  hizi zote ni nini au aseme MKAPA ndo ziwe sera?
   
 5. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante Tumain kwa ufafanuzi
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Narudia kwa msisitizo, HADI ASEME MKAPA NDIO ZIWE SERA?
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,562
  Trophy Points: 280
  Mwigulu ni vuvuzela! Hakuna mtu Chadema anayeweza kupoteza muda kujibizana na Vuvuzela!! Kazi ya vuvuzela unaijua? Baada ya mechi hutupwa hadi mechi nyingine!!! Mwigulu kiazi tu!
   
 8. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huyo Mwigillu kauli yake hiyo si ya kuwaponda cdm bali ni kuwadharau wana Arumeru kwa kua yeye amewaona uelewa wao ni mdogo!shame on him!kweli kua mwana c.c.m inabidi uwe mtu usiyeogopa mungu kwa kusema uongo na kuua,uwe mtu wa kujipendekeza,uwe mwizi na uwe muuaji!
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Aliwaambia wananchi wa Arumeru wasiweke gunzi katikati ya tochi ya Betri tatu.

  Yaani Betri (Rais toka CCM) + Gunzi (Kama watamchagua toka CHADEMA) + Betri (Madiwani toka CCM) maana wakifanya hivyo tochi haitawaka.
   
 10. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mwenye chuki binafsi ni huyo mmakonde aliyerusha mawe wakati yupo kwenye nyumba ya vioo.
  Ona sasa kavuliwa nguo mchana kweupe tena ukweni.
  Kwani sera ni kuwadanganya wananchi?
  Kweli mtaji wa ccm ni ujinga na upofu wa watanzania!!
   
 11. A

  ATA Member

  #11
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Lakini je sheria inaruhusu kusema uongo ukisimama kwenye majukwaa ya siasa?
   
 12. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kumsaidia cartons za condoms, maana hatofautishi wake za watu, wanafunzi, changudoa yeye mradi sketi tu.
   
 13. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Jana nimemsikia huyu Jamaa kwenye TZ akiongea siku ya uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Magamba, na leo asubuhi kupitia kipindi cha Power Break fast zimerushwa habari ya namna anavyoendesha Kampeni za CCM uko Arumeru.

  Huyu Jamaa ni mmoja kati ya vijana wanasiasa waongo, na wanaofanya siasa sizizo na tija ya namna yoyote ile kwa watanzania, ukimsikiliza kwa makini utagundua kwamba ni mtu ambaye bado anaamini kwamba mwanasiasa ni mtu ambaye anatakiwa kuwa na uwezo wa kuongea bila kuchoka, awe mpotoshaji, na awe na uwezo wa kudanganya bila uoga wala aibu.

  Hili la kuwa na ulinzi kutokana na nafasi yake CCM, ndilo linalompa kiburi na nguvu za kufanya siasa za maji taka kwa nguvu zaidi, hari zaidi, na kasi zaidi, na ndio kinachomfanya asiwe na hofu ya kutembea na wake za Masikini wa Tanzania.


  Nilipata kukutana na Jamaa ambao walitengeza timu yake ya Kampeni alipogombea Ubunge uko Iramba, Kuanzia mwenyekiti wa Kamati ile mpaka wajumbe wanajuta, labda awe amebadirika baada ya kuteuliwa kuwa mweka hazina wa CCM, Lakini ndugu hawa wanalalamika kwamba Jamaa ni Muongo kuliko Ibirisi Mwenyewe, Na mpaka sasa hajawahi kuivunja kamati hiyo sababu baada ya kupata ushindi alianzisha mkakati makini wa kuwakwepa wanakampeni wake.

  Hapa ninapoandika, wanairamba hawajawahi kukutana hata na mtoto mmoja Yatima ambaye Mwiguru alidai anawasomesha bure, wala iliko shule wanayosoma Yatima hao. Wakati wa Kampeni alizunguka Jimbo zima akisambaza uongo huo. kwamba anasomesha watoto Yatima wa Iramba zaidi ya hamsini, na kwamba akiwa Mbunge ataongeza idadi hiyo maradufu.
   
 14. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Siasa bana!!sijui haya maneno wanayatoaga wapi!
   
 15. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huyo Mwigulu dawa yake inaiva. Dk Kitila Mkumbo atamshughulikia Jimboni mwake 2015!
   
 16. s

  sawabho JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndio siasa, ni Uwongo uliokomaa.
   
 17. Fyengeresya

  Fyengeresya JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 702
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 60

  Mi nawashauri wawtahadharishe hao Wameru kwamba huyu jamaa ni mbaya sana kwa wake za watu, hivyo wasiwaruhusu wake zao kuhudhuria mikutano anayohutubia lasivyo atabaka mke wa mke halafu washili wazidi kulia kila siku kwa uharibu utakaotokea.
   
 18. s

  shykwanza Senior Member

  #18
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema mmefundwa kutukana tu na sio kujenga hoja
   
 19. s

  sirghanam JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kila siku ninaomba huyu jamaa asije akafanya yale mambo yake kwa wake za watu huko arumeru. Kwa sababu anaweza akatafuta nchi ya kukimbialia kujificha kwa aibu itakayompata
   
 20. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Lazima tujiulize kwanini Mwigulu alikimbia ualimu? CV yake akiwa mwalimu ipoje?Kama ukijua basi tambua kuna uwezekano alikua anawadanganya hata wanafunzi wake.
   
Loading...