CHADEMA, serikali tatu na serikali ya majimbo

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,347
CHADEMA wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?
 
Kitendawili: Ili upate wachangiaji wengi kwenye uzi wako hapa JF ni lazima ukitaje Chama Gani????
 
Kinachouliziwa ni gharama au ufanisi kiutawala?
Jibu kwa yote ni majanga ... more like trading flu for a septic shock!
 
Chadema ni bendela fuata upepo wao siku zote hawana hoja wanafuata yale yanayotokea kwenye jamii ndiyo wanaruka nayo.
 
Chadema wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?
Mkuu wewe unahangaika na chadema huku unafahamu kuwa chadema hawako sawa vichwani mwao zao ni kukurupuka tu hata hoja hakuna.
 
CHADEMA walipendekeza kuwa na mfumo wa majimbo ikakataliwa na wananchi, wakauweka pending. Mfumo wa serikali tatu ndo ukakubaliwa. Shida iko wapi?
 
Chadema wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?

Hapo sasa, SLAA atakuja kufafanua labda itakavyokuwa ila naamini hapa watajikanyaga sana.
 
CHADEMA walipendekeza kuwa na mfumo wa majimbo ikakataliwa na wananchi, wakauweka pending. Mfumo wa serikali tatu ndo ukakubaliwa. Shida iko wapi?

Wewe ni msemaji wa CHADEMA au unataka kuchafua hali ya hewa ndani ya CHAMA? mimi naamini wamejikanyaga,
 
Chadema wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?

Mkuu,
Ninavyofahamu mimi ni kwamba serikali yetu hivi sasa ina gharama kubwa za kiutendaji bila hata ya kuwa na serikali za majimbo. Nimepoteza hata idadi ya mikoa kutokana na kuongezeka kila kukicha, na kila mkoa una Mkuu wa Mkoa, Katibu Mtendaji (?) a.k.a. RAS na mlolongo mkubwa wa watendaji mkoani kuanzia Elimu, Afya, Mhandisi, Maji n.k. Hawa wote wapo, ila hawawajibiki kwa wananchi mkoani wala hawana maamuzi binafsi. Kazi yao kubwa ni kutekeleza 'amri' kutoka Dar ama Dodoma. Pia ufanisi wao utategemea pesa zitoke Makao Makuu pamoja na maelekezo ya shughuli za kufanya.

Kukiwa na serikali za majimbo ni kwamba hatutakuwa na RC 'mteuliwa' na Rais aliyeko Dar. Badala yake wananchi wa mkoa husika watapata nafasi ya kumchagua 'gavana' wao atakayesimamia matakwa yao na maendeleo yao. Watendaji wote watakaokuwa mkoani watawajibika kwa gavana ambaye atawajibishwa na wananchi waliomweka madarakani. Kwa maana hiyo shughuli za maendeleo zitasimamiwa kwa ukaribu zaidi kwani hakuna tena kusubiri 'amri' kutoka kwa mkuu wa kaya. Maana ingine ni kuwa ufisadi uliopamba moto na ubadhirifu vitaweza kudhibitiwa kirahisi zaidi iwapo watendaji wanajua ya kuwa uwepo wao unategemea ridhaa ya wananchi. Mathalani endapo wananchi wa mkoa fulani wana tatizo la Maji, Afisa wa Maji atapaswa kutoa majibu kwa wananchi na kueleza mikakati gani atakayochukua kuwapatia ufumbuzi. Serikali Kuu itakuwa msimamizi mkuu, itapanga sera za kitaifa kulingana na mipango mbalimbali itakayofikishwa huko kutoka kwenye majimbo badala ya kutoa amri na kutangaza sera majukwaani kama ifanyavyo sasa. Mfano mzuri ni huu mpango wa 'Big Results Now' ambao serikali imeutangaza, 'wateuliwa' Mawaziri wameupitisha, na pia mikoani maafisa elimu wameupitisha, walimu ambao ndio 'watekelezaji' hawakushirikishwa na sasa wanalazimishwa waukubali.

Laiti tungekuwa na serikali za majimbo serikali kuu isingewaburuza watendaji kutii amri kutoka juu. Badala yake mpango mzima ungeanzia kwa watendaji. Kila jimbo lingekuja na mawazo yake yanayoweza kutekelezeka kabla serikali kuu haijapayuka na kutangaza hadharani. Kwa mtazamo wangu hata gharama za kiutendaji zitapungua kwani mipango mibovu isiyo na tija haitapata nafasi. Wafanyakazi wazembe mikoani hawataweza kujificha na ufanisi utaongezeka. Hizo gharama nyingine za sasa zinazosababishwa na uangalizi mbovu wa miradi ya maendeleo zitakwisha chini ya mfumo wa majimbo.
 
Jaji Warioba alitoa ufafanuzi mzuri kuwa, 'wananchi hawataki majimbo, mkataba wala serikali mbili! Wanataka tatu'. Vyama vyote hapa vikubwa vilipoteza. Ni mbumbumbu ndo hawakuelewa
 
acha tu kuyaambia
 
chadema ni chama cha mashetani mkuu.

hivi unajua kweli kama kuna ahadi zaidi ya 70 zilizotolewa na mwenyekiti wa ccm ambazo mpaka sasa hazijatekelezwa???kweli wewe ni mwanachama dhaifu,,,,mimi nilizani utatumia uwepo wa jf kuwaeleimisha members ahadi chache mlizozitekeleza,,unakalia cdm cdm,,,
 
chadema wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na rais wa muungano na wakuu wawili wa serikali za bara na zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za bara na zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?

huu ni mtizamo wako na wala si msimamo wa chama ,,,

chadema ni chama makini na kinaongozwa na viongozi makini,,,,tumalize kwanza mchakato wakatiba unaohusu taifa kwa ujumla,,,,ilo ndilo la msingi kwanza,,,
 
Chadema wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao. Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini. Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?
wamevurugwa, hilo ni kosa la kuongozwa na akili ndogo wanafikilia leo bila kujali siku zijazo.
 
umeuliza maswali ya msingi sana kwenye hoja yako hii EMT. lakini kwanza hebu tujaribu kutafakari kwa undani ni kitu gani ambacho wanachi wanataka wka sasa??

wananchi wanataka serikali 3 wao hawataki moja wala mbili wala serikali za majimbo, kama ndivyo wananchi wanavyotaka ni wazi kwamba matakwa yao ndio yatimie.

lakini kwa upande mwngine CDM walilenga gavana wa jimbo ndiye atakaye mreplace mbunge by so doing wabunge wapewe meno ya kuwawajaibisha watendaji wa serikali. to me hii ilikuwa inaniwia ngumu sana sana kuipatia picha itakavyokaa manake niliwaza kiutendaji wabunge wetu kwanza sio wachapa kazi ni watu wa maneno mengi pasipo utekelezaji na hapo hapo pia wabunge wetu zaid ya kujineemesha kwa kutaka maposho makubwa hawana jingine wanalo tusaidia sisi kama wananchi sasa leo hii wakipewa hayo mamlaka ya kiutedaji si ndio watatumaliza??
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Chadema wanataka kuwe na serikali tatu. Wakati huo huo wanataka kuwe serikali ya majimbo. Kwa maana hiyo, kutakuwa na Rais wa Muungano na wakuu wawili wa serikali za Bara na Zanzibar. Pia kutakuwepo na gavana katika kila jimbo ambao watakuwa na mamlaka kamili kwenye majimbo yao.

Ukiondoa suala la gharama ambalo kwa demokrasia ni vyema kuzipitia kiutawala hii imekaa sawa? Utawala wa majimbo chini ya serikali tatu unawezekana? Dhana kuu ya sera ya serikali ya majimbo ni kuhamisha madaraka ya maamuzi kutoka kwa watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi vijijini.

Kama ni hivyo, hizo serikali mbili za Bara na Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na wakuu wawili zitakuwa zinafanya nini? Madaraka ya wakuu wa serikali hizo mbili hayatagongana na madaraka ya magavana wa majimbo? Kama serikali moja chini ya utawala wa majimbo haiwezekani, solution ni kuwa na utawala wa majimbo chini ya serikali tatu?

Single ya gharama haiuziki kwa maudhui ya kuhamisha madaraka ya mwisho kwa wananchi. Umesema vizuri hapo pekundu maana gharama ya hilo ni sifuri.

Hayo maswali uliyouliza yametolewa majibu mara nyingi, lakini kama ujuavyo bongo ni masuala ya maslahi yanapofusha ufahamu.

Nina hakika Serikali tatu inawezekana bila gharama za maslahi, na majinbo ndiyo hasa muondo wa msingi wa kujitawala toka iwepo dunia ya kidemokrasia.

Ni muhimu kujiuliza maswali hayo hayo kinyume; hasa pale pekundu hawa watawala wachache wamefanikisha nini kwa wananchi zaidi ya sintofahamu ya afadhali jana kuliko leo na afadhali leo kuliko kesho.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom