Chadema sawa na ANC, Dr Slaa sawa na Mandela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema sawa na ANC, Dr Slaa sawa na Mandela

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Mar 25, 2011.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama umesoma historia, hakuna kazi ngumu duniani kama kuleta mabadiliko. Tatizo ni kwamba wale walioshika madaraka wananufaika hivyo hawataki hali ibadilike. Ili kujilinda wanawatumia watumwa wachache wakiwadanganya kuwa wao ndio watakuwa watumwa bora kuliko wengine ili watumike kupigana na watumwa wenzao. Ukisoma kitabu cha Mandela "Long Walk to Freedom" utagundua kwamba upinzani mkubwa zaidi wa kuleta mabadiliko South Africa ulitoka kwa PAC na IFP ya Chief Butelezi na weusi wengine. Kazi ilikuwa ngumu sana maana PAC na IFP walikuwa kikwazo kikubwa na kama walivyo CUF, NCCR, TLP na UDP, walikuwa wanawaipiga vita zaidi ANC kuliko makaburu. PAC walikuwa na wivu wa kisiasa walivyoona ANC inaungwaji mkono zaidi.

  Ndio maana mimi naona Chadema ni sawa na ANC kwa maana ya kupigwa vita na CCM wanaotaka ku maintain status quo na vyama uchwara vya CUF et al vinavyodanganywa na CCM na pia vikisukumwa na wivu. Nawaomba Chadema wasikate tamaa maana katika kuleta mabadiliko vikwazo ni vingi na hakuna njia ya mkato. Hata Arafat alipingwa sana na Hamas waliokuwa wanafadhiliwa na mkoloni Israel na kweli walifanya haki iwe ngumu kupatikana.

  Kama ilivyo ANC, Mandela alipigwa vita na utawala wa mkaburu pamoja na vyama pinzani vya ANC. Sababu ni kwamba alikuwa anapendwa na watu wake na alikuwa na msimamo na hata alitangaza kuwa alikuwa tayari kufa kwa "cause " aliyokuwa anaipigania. Hana tofauti na Dr Slaa anayepigwa vita kuanzia CCM, vyama uchwara vyaa upinzani hadi Mufti. Namwomba pia awe mvumilivu maana hii ni vita na akumbuke Mandela alikaa gerezani miaka 27 kabla hajauona mwanga wa mabadiliko. Kama Dr Slaa na wanachadema wengine wameamua kwa dhati kuwatumikia Wa Tz, basi kuna gharama au sadaka na ndio wanayolipa na wataendelea kulipa zaidi hadi mabadiliko yaje. Na tatizo la kukatisha tamaa ni pale unapotaka kumkomboa mtu asiyejua kuwa yeye ni mtumwa. Kwanza unapaswa kumfanya ajue yeye ni mtumwa na pia ajue anaweza kufanywa huru. Ukienda mbali zaidi hata Yesu na Mtume Muhamad (SAW) walitaka kuleta mabadiliko ila vikwazo vilikuwa vingi sana hata Yesu akauawa. Mtume hakuuawa ila alipingwa sana. Hii inadhihirisha hakuna mabadiliko yanayoweza kupatikana mezani.
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,237
  Trophy Points: 280
  It is true, long leave and keep the motion until we eliminate these tellorist and black colonialists.
   
 3. J

  Joblube JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nakubali yote uliyosema kwa haja makini
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kapate kikombe haraka kwa babu kule Loliondo.

  Huwezi hata siku moja kufananisha Sukari na Chumvi. Huko ni kuchanganyikiwa. Wahi kikombe kabla hali haijawa mbaya
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Wewe ndio unatakiwa upate kikombe haraka sana kabla hali haijawa mbaya!
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Mandela hakuwa kuwa mwanachama wa chama cha makaburu halafu ndiyo akaenda CDM!

  Slaa alikuwa CCM na baada ya kufukuzwa ndio akaenda Chadema!

  Slaa is very good leader, he is special one, ila kwa Tanzania hakufaa kugombea urais, na hatakuwa rais nchi hii, Though rais anaweza kutoka chadema, lakini siyo Slaa. Sometime life is like this we dont get what we want when we want!
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  WEB wengi wetu tunajua kabisa unachuki binafsi na Dr Slaa hata wakati wa uchaguzi ulijionyesha wazi,Umeweka maandiko yako hapo kama vile Dr.Slaa alin'gang'ania kutaka uraisi,alishasema mwenyewe mara nyingi kwamba Chadema walimwomba sana asimame kugombea uraisi na kwa mapenzi ya chama chake alikubaliana na uamuzi wa kamati kuu na akafanya atekeleze waliyoamua sasa la hatakuja kuwa raisi linatoka wapi mmh ,jaribu kupunguza chuki kiliba cha moyo kimekujaa we msomi bwana acha hivyo
   
 8. d

  dotto JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama wewe ni Mungu!! Pia Uraisi wa nchi hii sio mali ya mtu au kikundi cha watu bali ni jukumu la Watanzania wote kumuchangua mtu mmoja kuwa kiongozi wao. Sidhani kama wewe ni muakilishi wa Watanzania wote. Labda waweza kuwa mmoja wapo wa Vibaka wa demokrasia katika nchi hii. Na uovu huwa una mwisho wake. Waweza kuwa mzuri au mbaya- Refer: Kukuwa zabanga.
   
Loading...