CHADEMA: Salute Kwa Ushindi Wa Kishindo!

inasemekana pesa ilitoka ccm - kwenda - kwa wananchi - halafu wananchi wakaipeleka cdm. hii nayo inahitaji kufikiriwa. unayetoa pesa umenyimwa kura na anayeomba pesa kapewa na kura kapata, hayo mapya.
hakika umenena vyema. kila neno ulilosema ni ukweli mtupu ila ukweli unaouma.
 
Lowassa anasemaje?
yuko happy na matokeo?
je kampeni ya kujivua gamba imekuwa ndo sababu ya CCM kushindwa?
au ni 'struggle for power within CCM' imerahisisha CCM kushindwa?
wewe kama insider unatuelezaje?


Mkuu hapo kwenye red ni matusi makubwa kwa watanzania, kama watanzania wanachagua viongozi kutoka kwenye vyama ambavyo havina migogoro basi leo SAU ndio ingekuwa the leading Political Party.

Ukweli ni kwamba CCM inakataliwa kwa sababu imejinyanganya uwezo wa kuongoza kwa kukumbatia Rushwa kitu ambacho kinawafanya washindindwe kusimamia maendeleo ya Taifa.
 
Bw. William nikiwa na hakika kwamba wewe ni mmoja wa wanufaika wa mfumo wa ccm wa kupokezana vijiti kifamilia una wajibu wa kuwahakikishia wtz kuwa nanyi watoto wa "wazito"mna uwezo pia. Kupitia michango yako hapa JF nilitegemea umekomaa na una reflect silika ya baba yako, kumbe ukishazoea kubebwa haukui! Nenda jimboni achana na vyeo vya kupewa maana mwisho wake umekaribia!!!!!!!!!!!
 
Kwa utamaduni wa CCM sikubaliani na pongezi zao, hasa kitendo cha Nape Nnauye kuwa wa kwanza kuita Press na kutoa msimamo wa CCM kukubali matokeo, mtazamo wangu ni huu:
1. Hii ni njia ambayao imetumika kumcofuse Edward Lowasa ili ajione hana ushawishi.
2. Kama CCM huwa inakubali matokeo hivi ni kwa nini jimbo kama la Ubungo, Singida na Arusha CCM haikukubali clear Defeated?

Mwigulu Nchemba alinukuliwa hapa JF akisema kukata rufaa matokeo ya uchaguzi ni kumnyima fursa Mbunge aliyechaguliwa kuwatumikia wananchi.....je hapa anamaanisha John Mnyika, Tundu Lisu na Godbless Lema wanawatumikia mashetani na sio wananchi?

Unafki utawapeleka pabaya sana wana CCM, na nina wasikitikia sana ninyi wana CCM na subirini muone hasira za Edward Lowasa kwenye uteuzi wa wabunge wa Afrika Mashariki na subiri uone JK atakavyoungana na Edward Lowasa kuhakikisha mama yako Anne Kilango anapigwa mweleka na Sophia Simba kwenye uchaguzi wa UWT. ukumbuke JK na Sofia Simba ni mtu na dada yake.
 
Yule Ndondocha tu! Elimu yake ni darasa la tatu na alikimbia umande na kukimbilia kutega ndege. Mshamba sana yule!

Wasira darasa la ngapi? Mimi huwa siamini sana elimu inaleta ustaarabu. Ukienda pale UDSM ,kuna vyoo karibu na Nkrumah humo ndani wameandika matusi ukutani. Wale nao ni wasomi
 
mimi nafikiri tusiuime ushindi wa kishindo,wala sunami, hizi ni lugha za washenzi CCM, HUU NI USHINDI WA MABADILIKO, THE POWER OF PEOPLE. Hebu tubadilike tuende na wakati, watanzania wanahitaji mabadiliko, kukombolewa, vitu hivi vinaenda sambamba na terminologies mpywa, na sio lugha na maneno ya hovyo kama hayo.
 
- Well, jana Demokrasia imechukua mkondo wake na Chadema wameibuka washindi katika mchuano mzito sana, binafsi ninawapa congratulitons straight form my heart kwamba ushindi wao ulikuwa ni wa kishindo na sasa ni wakati wa kusonga mbele na kujali TAIFA KWANZA!

- CCM pia wanahitaji heshima kubwa kwa kukubali matokeo bila vurugu wala ubishi wa kuibiwa kura, matokeo ya uchaguzi wa jana yawe ni changamoto kwa vyama vyote vya siasa nchini kwamba siasa sio uadui wala vita, na asiye kubali kushindwa sio mshindani!

- SALUTE CHADEMA NA MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William.

hivi wewe hujui tangia tupate uhuru kiongzi aliyejali taifa beside sokoine hayupo mwingine? Kikwete ba Mkapa wamejitahidi sana ktk elimu na kucut back unemployment. Sisi tangia enzi tunajali kusaidia wakimbizi na kuunga mkono wapalestina wakati nchi ina 98% unemployed people!
 
Hivi CDM wasingelinda kura, kweli CDM wangetoka kidedea? Wale waliokutwa na kura ktk maboksi hatua yao ikoje?
 
- Well, jana Demokrasia imechukua mkondo wake na Chadema wameibuka washindi katika mchuano mzito sana, binafsi ninawapa congratulitons straight form my heart kwamba ushindi wao ulikuwa ni wa kishindo na sasa ni wakati wa kusonga mbele na kujali TAIFA KWANZA!

- CCM pia wanahitaji heshima kubwa kwa kukubali matokeo bila vurugu wala ubishi wa kuibiwa kura, matokeo ya uchaguzi wa jana yawe ni changamoto kwa vyama vyote vya siasa nchini kwamba siasa sio uadui wala vita, na asiye kubali kushindwa sio mshindani!

- SALUTE CHADEMA NA MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William.

Thanks sana mkuu, Tunakutakia ushindi wa Kishindo na wewe maana vijana wanahitajika sana .
 
Back
Top Bottom