Chadema ruvuma kufanya mkutano mkubwa wa hadhara leo mchana viwanja vya soko la samaki la zamani

Mar 23, 2012
64
13
Na Mwandishi Wetu, Songea

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Ruvuma leo tarehe 4/7/2012 majira ya saa nane kinatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Viwanja vya Soko la Samaki la zamani (Shule ya Msingi Mfaranyaki).

Taarifa zilizopatikana mjini hapa jana na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mjini Joseph Fuime zimeeleza kuwa mkutano huo utahutubiwa na viongozi wa ngazimbalimbali wa Chadema kutoka ndani ya mkoa wa Ruvuma
.

Fuime alisema lengo kuu ni kuimarisha chama na kukemea mamboambayo yanaashiria ukandamizaji wa haki za wanyonge kunakofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Alisema kuwa hoja mbalimbali zitawasilishwa kwenye mkutano huo zenye lengo la kutuma salamukwa viongozi wa Serikali kutokana na mambo yahovyo wanayoyafanya ambayo yanaathiri ustawi wa maisha ya watanzania wengi.

Hata hivyo, alitoa wito kwa wanachama na wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo ili kuweza kusikia sera za Chadema na maovu yanayofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi
.
 
Chadema again, kwa nini hii mikutano ya CHADEMA inaruhusiwa wakati Bunge linaendelea?
 
M4C swafi sana viva chadema, waambieni waende na jimbo la Peramiho huyu Jenister hajafanya lolote la maana, lazima 2015 atolewe
 
safi sana, hata mimi nitakuwepo!
pipoooooooooooooooooozi, pawaaaaaaaaaaaaaa......................
 
Chadema again, kwa nini hii mikutano ya CHADEMA inaruhusiwa wakati Bunge linaendelea?

Na bado mwaka huu mtakosa pa kupumulia, kila mtu CDM ni kamanda so sidhani km wabunge watakuwepo (rejea habari km ilivyoandikwa mwanzo)
 
Back
Top Bottom