Head teacher
JF-Expert Member
- Mar 10, 2012
- 1,796
- 413
Kwa nchi za kiafrika chama tawala kamwe hakiko tayari kuachia madaraka kirahisi rahisi. Ni lazima wapinzani wapitie katika hatua za kuuwawa, kushtakiwa,kubambikwa kesi, kulipuliwa mabomu, na kadhalika. Kwa hiyo nawakumbusha wapigania uhuru na wananchi kwa ujumla msidhani wakoloni wa CCM wapo tayari kupoteza maslahi yao na usalama wa mali zao kirahis rahisi tu. Nawaapia chadema hata kama mtashinda kwenye kura za urais hawa wanaojiita green bregade wataingia msituni ili kuipindua serikali ya chadema. Kumbukeni idadi wa wanyonyaji waliopo CCM na ambao wana nguvu ya kifedha za kifisadi na ushawishi pamoja na marafiki zao wa kiasia na wazungu,na wachina walioingia nao mikataba hawapungui laki moja. Hivyo chadema mnatakiwa mjipange hasa hasa si lele mama.Kukata mirija ya kifisadi ya CCM ni sawa na kumnyang'anya kitoweo simba nchi kavu au mamba mtoni. Hivi ndivyo nionavyo mimi.