CHADEMA ni ''Sugu'' badala ya kuibomoa utabomoka wewe

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,902
106,933
CHADEMA sio Freeman Mbowe au Tundu Lissu, sio kijikundi cha watu wawili watatu mkadhani mkiwabana basi siasa zake zitaishia hapo. SAHAU

CHADEMA ni imani na hisia za watu. CHADEMA ni zaidi ya chama cha siasa. Huwezi kupambana na mtu mmoja au wawili ukafanikiwa. Unakuwa unaumwa akili ukiaamini kwamba mikwara na vitisho vinaweza kuiua CHADEMA. CHADEMA sio James Lembeli ukadhani ukihamia CCM ndio CHADEMA imekufa. UNAJISUMBUA

Tumia akili ndogo tu kwamba wale watu milioni 6 walitoka wapi pamoja na kuchakachua kote?

CHADEMA ipo maofisini, kilabuni, vijiweni, ipo Ikulu, ipo kwenye baraza la mawaziri, ipo CCM ipo kitandani, ipo jikoni, ipo club ipo msibani, ipo kwenye birthday ipo deathday. …………………………………….CHADEMA ni love and affiliation.

Nipe mfano mmoja tu wa hujuma zenu dhidi ya CHADEMA ambazo zimewahi kufanikiwa. Alikuwepo Dr.Slaa na Zitto Kabwe CHADEMA, we still moving to the top. Walikwepo watu wa hujuma kali kama Steven Wasira na Jakaya Kikwete wako wapi mwisho wa siku wameaibika wao. Kikwete kila Magufuli akipanda jukwaani anamsema yeye. Wasira sitaki hata kujua alipo, ajihukumu mwenyewe (in Lowasa’s Voice)

Tena kwa bahati mbaya hawa wa leo wanatumia nguvu na mishipa, hawatafanikiwa kamwe, heri yule aliyekuwa anatumia system, fitna na ununuaji wa wanachama.

Tumieni maono ya CHADEMA kujenga nchi kama mlivyopata kukopi ilani zake japo mnashindwa kuzitekeleza.

Mungu mbariki Freeman Mbowe, mpe maisha marefu hapa na Mbinguni. Anakutumikia na anatumikia watu wako.
 
We huoni kwanini Pombe amekimbilia home? UKUTA usikukute utakuaibisha kama wewe ni mwanademokrasia uchwara.
 
Si hekima kudhoofisha upinzani, labda kama hawajui umuhimu wa vyama vingi vya siasa nchini. Badala yake wachukue Yale mawazo mbadala na kuyafanyia kazi
 
hapa mwisho mi sijapasoma nimeogopa kuwaombea wasiowaadilifu sina duwa yakuwaombe hata kina ngosha
 
We huoni kwanini Pombe amekimbilia home? UKUTA usikukute utakuaibisha kama wewe ni mwanademokrasia uchwara.
Mkuu, kwani mtu kwenda kwake ni vibaya? Kwani Tundu Lissu alimtukana Rais si akiwa kwao? Kipi cha ajabu kwa Mkuu wa nchi? By the way Rais ameenda Chato hata kabla hajatukanwa na Lissu
 
Magufuli ameshapoteza dira yake baada ya kuanza kucheza mchezo wa Chadema. Wana-mprovoke kidogo yeye anajaa mazima.
Lissu mmoja anawasumbua na wanamshindwa. Je, hao milioni 6 wakiamua kuisumbua serikali wataiwezea wapi Chadema?
Serikali ya CCM ikubali kuwa wanachadema ni waungwana sana.
 
Kuna watu wanasema wanaipenda CDM ila hawampendi Mbowe.Ukweli ni kuwa hauwezi kutenganisha mafanikio ya CDM na uwepo wake kama mwenyekiti.Mbowe anabaki kuwa mpinzani anayeitia homa ccm na serikali yake kuliko wote
 
Magufuli ameshapoteza dira yake baada ya kuanza kucheza mchezo wa Chadema. Wana-mprovoke kidogo yeye anajaa mazima.
Lissu mmoja anawasumbua na wanamshindwa. Je, hao milioni 6 wakiamua kuisumbua serikali wataiwezea wapi Chadema?
Serikali ya CCM ikubali kuwa wanachadema ni waungwana sana.
Milioni sita watoke wapi ? Ni JPM FOR EVER
 
Back
Top Bottom