Hakikwanza
JF-Expert Member
- Dec 11, 2010
- 4,043
- 1,012
Chadema inawanyima usingizi ccm kila wakilala na kuamka wanaiwaza chadema kuliko chama chao.
Kwa miaka kadhaa sasa, nimezidi kuamini zaidi kwamba CHADEMA ni chama ambacho kimelenga kuleta mabadiliko katika nyanja ya kiutawala, kijamii, kiuchumi na kisiasa. Kifupi kimedhamiria kwa dhati bila shaka kukiangusha chama tawala cha CCM.
CCM ambayo ilizaliwa mwaka 1977, ilirithi utawala kutoka kwa kilichokuwa Chama cha TANU. Uhuru wa nchi yetu tuliupata wakati TANU kikiwa ni chama cha siasa kilichokuwa kikiongozwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Alipokuwa akitangaza dhamira yake ya kutaka kujiuzulu wadhifa wa urais, Nyerere ambaye ndiye Waziri Mkuu wa kwanza wa nchi yetu hii, aliwahi kusema: "Mimi nang'atuka, lakini bila CCM madhubuti nchi itayumba."
Usemi na utabiri huu wa Baba wa Taifa umeanza kujionyesha dhahiri sasa. Sote tunashuhudia jinsi nchi inavyoyumba kwa utawala tulionao huu wa CCM. Hili halina kificho wala hapaswi mtu kuvimbisha mishipa ya shingo yake kubisha ukweli wa jambo hili.
Enzi za Mwalimu hakukuwepo na utitiri wa viongozi kujilimbikiza mali. Enzi hizo ulikuwepo uwajibikaji wa dhati baina ya viongozi kwa wananchi wake. Dhuluma na uporaji wa haki za wanyonge ulikuwa mwiko. Lakini leo hii tunashuhudia maajabu.
CCM ya Mwalimu Nyerere si sawa na hii ya leo ya akina Rais Jakaya Kikwete, Nape Nnauye, Abdulrahman Kinana, Philip Mangula, Mwigulu Nchemba, Juma Nkamia anayetukana wabunge wenzake bungeni, imekosa mwelekeo. Ndivyo ilivyo.
Ndani ya CCM kumeibuka mambo mazito ya kudharauliana na kupuuziana wao kwa wao. Imeonekana hawaaminiani tena. Huyu akisema hiki, mwingine anasema hivi. Yaani ni vurugu tupu.
Chadema mwendo mdundo .