CHADEMA ni chama kinachoendeshwa kwa majungu, ushakubimbi na umbea

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

1. Walisema Zitto Kabwe ni msaliti na hawatashirikiana naye kwa namna yoyote ile. Leo hii wanakula sahani moja.

2. Walituaminisha kuwa Jakaya Kikwete ni Rais dhaifu kuweza kutokea Tanzania. Leo wanamkumbuka na kujipendekeza kwake.

3. Walisema Lowasa ni fisadi Papa. Leo hii wamemsafisha na kashfa hizo na ndiye tegemeo lao pekee uchaguzi mkuu wa 2020.

4. Walitaja hadharani kuwa Ridhiwani Kikwete anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, leo hii wametajwa wao tena kwa ushahidi wanasema wameharibiwa utu wao.

5. Walitaja majina ya Mafisadi Papa wakiwemo Lowasa na Kikwete leo hii hawataki kuhusishwa Lowasa na kashfa ya Richmond.

6. Wanasema wanapambana na biashara ya madawa ya kulevya kwa dhati lakini watuhumiwa wanaoikimbia CCM kwa uchafu wao wanawaona lulu kwao

Kwa tabia hizi na nyingine ambazo sijazitaja kwa hakika CHADEMA hawastahili kuongoza hata kitongoji.
 
Umeorodhesha mambo lukuki yaliyojaa kichwani mwako na moyoni mwako kuhusu Chadema.
Na bado unajitia moyo kuwa huna mahaba na Chadema.
We Chadema unaipenda sema hujajigundua tu. Usingeipenda isingeutesa moyo wako hivyo.
Tumia malimao, huwa yanasaidia !
 
Siasa sio uadui na panapo hitaji ushirokiano Nivyema kushiirikiana hio ndio siasa mambo Leo na uzalendo usiwagawe watanzania

Hata ccm wakifanya jambo lenye tija tutawapongeza coz hakuna mwenye hatimiliki ya Tanzania tanzania niyako niyangu niyetu sote
 
Ni uhalisia Mkuu

Unadhani Upumbavu mnaofanya CCM basi vyama vyote wanafanya,maana mwenyekiti wenu alilalama wanaccm wanafikiri.Na yule jamaa yake aliyetoroka naye alilalama.wanaccm wanafikiri.Hahahahahaha mtajibeba
 
hauna jipya mkuu, utaongea sana hakuna kitakachobadilika, chadema inazidi kuchanja mbuga.
Propaganda zako ni nyepesi sana halafu tushakuzoea huna madhara. Poleee
 
Walisema hawachukui makapi toka ccm Matokeo yake limekuwa ni Lango la kila mharifu kuingia
 
Narudia tu ushauri wangu kwako.. Tafuta kazi achana na kutumika na umbea
 
Unadhani Upumbavu mnaofanya CCM basi vyama vyote wanafanya,maana mwenyekiti wenu alilalama wanaccm wanafikiri.Na yule jamaa yake aliyetoroka naye alilalama.wanaccm wanafikiri.Hahahahahaha mtajibeba

Hapo umeongea nini?
 
Wadau, amani iwe kwenu.

1. Walisema Zitto Kabwe ni msaliti na hawatashirikiana naye kwa namna yoyote ile. Leo hii wanakula sahani moja.

2. Walituaminisha kuwa Jakaya Kikwete ni Rais dhaifu kuweza kutokea Tanzania. Leo wanamkumbuka na kujipendekeza kwake.

3. Walisema Lowasa ni fisadi Papa. Leo hii wamemsafisha na kashfa hizo na ndiye tegemeo lao pekee uchaguzi mkuu wa 2020.

4. Walitaja hadharani kuwa Ridhiwani Kikwete anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, leo hii wametajwa wao tena kwa ushahidi wanasema wameharibiwa utu wao.

5. Walitaja majina ya Mafisadi Papa wakiwemo Lowasa na Kikwete leo hii hawataki kuhusishwa Lowasa na kashfa ya Richmond.

6. Wanasema wanapambana na biashara ya madawa ya kulevya kwa dhati lakini watuhumiwa wanaoikimbia CCM kwa uchafu wao wanawaona lulu kwao

Kwa tabia hizi na nyingine ambazo sijazitaja kwa hakika CHADEMA hawastahili kuongoza hata kitongoji.
Wewe leo umesema kada wenu wa CCM na waziri Nape Nnauye anajihusisha na biashara ya unga/madawa ya kulevya kwa kushirikiana na Majizo na ukafika mbali kuweka maazimio ya kikao chao walichokaa jana.

Sasa kuhusu majujungu, umbea nk tuanzie hapa kwenye hii mada.
 
Back
Top Bottom