Baada ya Chadema kupoteza Igunga nimeanza kujiuliza maswali kama chadema wana institutional framework za kuweza kuendesha nchi kubwa kama Tanzania?
Wana watu makini lakini je ni watu makini kiasi gani wa kuweza kuendesha nchi kubwa kama Tanzania?
Wanaweza kuwafikia bibi na babu waliopo huko majita,matombo na kwingineko?
Muhimu kwao sasa ni kutengeneza chama, kuwa na mikono ya chama kama baraza la wazee, wanawake kamati kuu,halmashauri kuu,baraza la vijana ambozo zina nguvu na ushawishi wa kutosha kuanzia vijijini,watu wa mjini tushaelimika,sasa waanze kuelimisha na kusambaa mijini, angalia bavicha,haionekani kuwa na watu ambao wana ushawishi,uelewa pamoja na uzoefu katika siasa.
Slaa ni mtu anayeweza kuitoa Tanzania shimoni lakini chama chake kinaweza kumbeba kama yeye alivokibeba mwaka 2010?

Kuna vitu viwili hapa. CHAMA na SERIKALI. Serikali ndiyo inatawala nchi sio CHAMA. Hivyo usiwe na wasiwasi. Chama chochote kishinda uchaguzi wa urais kinaweza kusimamia nchi vizuri tu. Kuna watanzania wengi tu wanafanyakazi serikali kama wataalum na sio wanasiasa. Hawa ndio wanaendesha nchi. Rais kazi yake ni kutoa tu malekezo ni sera gani itekelezwe. kama sera ni nzuri kama maana ya kutekelezeka basi wataalum watafanya hivyo.
Hata ndani ya CCM kuna watu wengi tu wana nia njema na nchi yetu hao wanafahamika na wanaweza kutumikia serikali isiyotokana na CCM. Kwa mfano Rais wa Marekani Barack Obama alimpa kazi ya waziri wa ulinzi mtu ambaye alikuwa anashikilia nafasi hiyo hiyo wakati wa rais Bush. Ina maana kwamba mtu huyo ni wa chama tofauti na cha Obama. Pia hivi karibuni rais wa Zambia Michael Sata amewateua badhii ya mawaziri wake (4) kutoka chama kilichoshindwa uchaguzi wa rais. Muhimu hapa ni kuangalia watu wachapakazi na wenye nia njema na nchi. Hawa watu watakuwa wanatekeleza sera kama jinsi watakavyoelekezwa na rais mwenyewe. Na rais akiona hawafanyi hivyo anakuwa na mamlaka ya kuwaondoa na kuweka wengine mara moja.
Kimsingi nchi inatakiwa kuwa na rais aliye makini na mahiri katika kazi zake. Na hili ndio tunakosa hapa Tanzania. Ndio maana kila siku Prof. Lipumba anasema nchi ina obwe ya uongozi (Leadership vaccum).

good comments..!watu wako wengi sana hata wakitaka kuoverhaul kuanzia mtendaji wa kijiji.
Ebu tafuta waliogombea ubunge kwa tiketi ya cdm ni wangapi; wengi wao ni watu makini sana mfano deusdedith jovin kahangwa wa karagwe. Huyu ni mjenga hoja kama akina zitto, halima mdee, mnyika nk.
Kuna hao wasomi walio kwenye mawizara wasioridhika na ccm - hivi unafikiri siri za serikali cdm wanazipata vipi? (kuna watu).
Kuna vijana wanaomaliza vyuo vikuu, kuna wanaomaliza kidato cha sita na nne. Ni wengi, kama hao wa formiv ni kuwapa kozi ya mwaka mmoja halafu wanakuwa watendaji wa vijiji na kata nk.
Kama wengi walivyosema. Kinachohitajika ni uongozi wa juu.