CHADEMA ni chama cha Waoga Wapenda Magwanda!?

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,285
Ni mwezi wa nane Mwenyekiti ndugu Mbowe anautangazia Umma kuhusu operation UKUTA, akisema una lengo la kuondoa Udikteta nchini, mara kwa mara anaendelea kusema kuwa hakuna choice isipokuwa kufanya maandamano makubwa tarehe mosi mwezi September. umma unapokea tangazo lake, vijiweni, kwenye vibaraza vya kahawa kwenye mikisanyiko nchi nzima ni mazungumzo juu ya Maandamano ya UKUTA.

Nchi inajawa na tension, kundi kubwa la watu linaunga mkono, na kundi kubwa linapinga, Nguvu kubwa za kipolisi zinatumika kuwatia watu hofu.

Tahamaki, Mwenyekiti katika Kombati zake anagwaya, anarudi nyuma, anasurrender!. Na ili aonekane bado yumo anawahadaa Wafuasi wake kuwa UKUTA sasa ni mwezi October!, lakini wajuzi walishaona kwamba hapa Kamanda mkuu keshamwaga Manyanga.

Ni kweli October inafika Mwenyekiti badala ya kwenda mtaani kupinga Udikteta, akaenda Uwanja wa Taifa kuangalia mpira wa Simba na Yanga!. Huyu ndo kamanda katika Kombati, Kamanda Muoga!.

Miezi Miwili baadae, Kamanda huyu ndani ya Kombati, aliyeitangazia dunia kuwa Tanzania sasa ina Udikteta na inabidi tuuondoe, anakwenda kufanya uchaguzi wa Kidikteta na kimagumashi kuwahi kutokea ndani ya chama chake mwenyewe!, anakwenda kumkata kijana Sosopi na kumuweka Msigwa bila ya kufuata msingi wowote wa kidemokrasia. This is cowardice, Kamanda wa Kombati hana tena moral authority ya kupigania demokrasia!

Ni nini Athari za Uoga huu wa Kuacha kusimamia Operation UKUTA?

1. Watawala sasa wanajua, UKAWA siyo credible threat tena kwao, Wanajua wakitumia nguvu kidogo za kuwasumbuasumbua watanywea kama kuku walioshikwa mdondo!

2. Watawala wanajua, Hakuna Uongozi ndani ya Chadema wenye guts wala moral authority ya kuwaambia stop!

3. Consequence za Kusitisha Operation UKUTA sasa zimefanya watu wakamatwe hovyo kwa makosa madogomadogo na kuwekwa ndani bila hata kupewa dhamana, Kwa sababu wenye kufanya hivyo wanajua Mtawafanya nini?.

Sasa hivi Chadema imekosa dira, haijui isimamie nini na ifanye nini. Ni dhahiri kuna hofu ya kushughulikiwa Kwa Biashara za Makamanda ndani ya Kombati kutiwa kashkash, kusumbuliwa submbuliwa kiuchumi, Lakini kama ni makamanda kweli, then that is the price to pay! La sivyo wakae pembeni, waje watu wanaoweza kusukuma gurudumu hili la kudai mabadiriko ya kweli lishike usukani!.

Nasema Chadema haipaswi kuwa chama cha Waoga chenye kuendeshwa na Jemedari Muoga!
Tunataka Upinzani wa kweli utakaosimama kidete bila kutetereka katika awamu hii ya tano na tunautaka NOW, kamanda ndugu Mbowe kama umeshindwa kuprovide leadership katika hili kaa pembeni mjomba!
 
Siyo wapinzani tu, watanzania wote ni waoga. Malalamiko yote haya ya maisha magumu ingekuwa nchi nyingine pangechimbika
 
Siyo wapinzani tu, watanzania wote ni waoga. Malalamiko yote haya ya maisha magumu ingekuwa nchi nyingine pangechimbika

Nchi zote huhitajika platform ya kuongoza movement fulani ya kusimamia madai yao, Hapa Tanzania Wananchi waliweka tumaini lao katika Chadema kupigania haki yao!.

Watu waliichukulia Operesheni UKUTA kama ukuta kweli wa kuwakinga dhidi ya uminywaji wa demokrasia nchini, Cha kusikitisha Mwenyekiti Mbowe akagwaya, akaogopa akasurrender!.

Kitendo cha kusurrender kimekiondolea chama turufu yoyote ya nguvu ya umma katika kuishinikiza serikali!. Chadema nacho sasa kimegeuka Chui wa Karatasi haking'ati, kimekuwa chama cha kusubiria ruzuku ya kila mwezi!
 
Huwa nashindwa kuelewa kwamba hata kama ni kulipwa MTU unaanzaje kuamka tu asubuhi hii na kuanzisha thread ya kushambulia chama ambacho hakina Dola??

How come?? Mimi Yale niliyoyawaza na kuyapanga usiku ndio nayafanyia kazi SAA hizi, kwahio Wewe mwenzetu umelala unawaza kuhusu Chadema??? Seriously?? Unawaza kukulemaza Chadema??? Kwa Makala za dizaini hii?? Aisee jipange upya yaani hata kama ni propaganda ndio umeajiriwa kwa ajili hio ujue bado saaaana.

Nitakuja niwafundishe jinsi ya kufanya propaganda ambayo ni endelevu na inavutia kusoma na kushawishi
 
Kutokuwa chama dola siyo hoja ya kukifanya chama kiwe na uzembe wa kutopigania maslahi na haki za kikatiba za wananchi, maana kimsingi hiyo ni kazi ya chama kinachojiita cha kidemokrasia.

Lakini wananchi tuna haki ya kuhoji utendaji wa hivi vyama kwa sababu tunachangia uwepo wao na utendaji wao kupitia ruzuku ambayo ni kodi zetu. Kwa hiyo tunataka vyama vyote kikiwemo Chadema vitutetee kwa nguvu zote, na viwe na zero tolerance katika usiginaji wa katiba ya nchi na haki za raia.
 
kuna jemadari mmoja wa vita aliwahi kutokea!
walienda kupigana vita katika kisiwa baada ya meli zao zote kutia nanga jemadari akaamrisha zichomwe meli zote moto isibaki hata 1zilivyoteketea zote akawaita watu wake akawaambia hapa leo kuna mawili kufa au kushinda!!jamaa kuona hakuna namna tena walipambana ile vita na walikuwa wachache mara 10 ya maadui zao na walishinda kwa kishindo kikubwa sana!sio mbowe anatangaza ukuta yeye yuko zake sauzi anakula bata!kila siku naongea hapa mbowe anaburuza na kutumia akili za raia vibaya!bora akatangaze tu chama chake kimefilisika kiakili
 
mkuu uko sahihi sana....CHADEMA ndio inapaswa kuiongoza nchi na kukibana chama tawala
tuna bahati mbaya ya kuwa na mwenyekiti dhaifu na opportunist
kumbe alikuwa anakingiwa udhaifu wake na slaa
katibu mkuu wa CHADEMA naye ni bomu kabisa...alipewa ukatibu kwa sababu ni mtu wa lowasa...lowasa alimtumia katika kuendesha mgomo wa madaktari
mkimfahamu lowasa...he is a seriously bad person . ...a mafioso...he doesn't deserve the highest office of our country
 
Ni dhahiri Zitto na Dr Slaa walikuwa wana shield mapungufu mengi ya Mbowe!

Bunge la Tisa, na Operesheni za kikakamavu ziliifanya Chadema kuwa Chadema.

Sasa hivi EL ni pacifist, hataki kuipoke system to the limit, kwa sababu anajua wanajua yake mengi, anakuwa compromiser sana kwa sababu anajua wakimdeal kwenye biashara zake, wakianika mafaili yake he has more to lose!.

EL anasema eti alishinda, halafu eti akakaa kimya tu!. Sasa cha kujiuliza kama ulishinda na ukafanyiwa mchezo mchafu, ni nini basi kitawazuia wasikufanyie mchezo mchafu katika uchaguzi ujao?, na Je usiposimama kidete sasa then utajikomboaje?
 
mkuu uko sahihi sana....CHADEMA ndio inapaswa kuiongoza nchi na kukibana chama tawala
tuna bahati mbaya ya kuwa na mwenyekiti dhaifu na opportunist
kumbe alikuwa anakingiwa udhaifu wake na slaa
katibu mkuu wa CHADEMA naye ni bomu kabisa...alipewa ukatibu kwa sababu ni mtu wa lowasa...lowasa alimtumia katika kuendesha mgomo wa madaktari
mkimfahamu lowasa...he is a seriously bad person . ...a mafioso...he doesn't deserve the highest office of our country

Sasa hivi tunashuhudia the lowest moment ya Chadema tangu mwaka 2005, Issue hapa ni uongozi uliochoka, usio na ubunifu na ambao ajenda yao.namba moja ni kustrategise kwa ajili ya maslahi yao zaidi kuliko maslahi mapana ya umma!
 
cha kujiuliza zaidi tunao asilimia 90 ya watu waliokuwepo tangu kipindi hicho..lakini this time around Wapo tu wakiwa wamekata tamaa.

kiongozi dhaifu mbowe yeye hana hata muda na chama ila anao muda na lowasa

na je zile milioni 200 ambazo chama changu mnamlipa lowasa kila mwezi ni za nini?

cc technically MTAZAMO
 
It seems Mbowe keshagive up mabadiriko kwa ajili ya umma, bali yupo kipersonal zaidi mathalan yaani maadam ruzuku inaingia baaaasi, kwa nini nisumbuke na sera na falsafa za chama.
 
Huwa nashindwa kuelewa kwamba hata kama ni kulipwa MTU unaanzaje kuamka tu asubuhi hii na kuanzisha thread ya kushambulia chama ambacho hakina Dola??

How come?? Mimi Yale niliyoyawaza na kuyapanga usiku ndio nayafanyia kazi SAA hizi, kwahio Wewe mwenzetu umelala unawaza kuhusu Chadema??? Seriously?? Unawaza kukulemaza Chadema??? Kwa Makala za dizaini hii?? Aisee jipange upya yaani hata kama ni propaganda ndio umeajiriwa kwa ajili hio ujue bado saaaana.

Nitakuja niwafundishe jinsi ya kufanya propaganda ambayo ni endelevu na inavutia kusoma na kushawishi
Mpwa wakati mwingine ni mateso tuu kuwafikiria watu kama hawa kuwa huwa wanafikiri nini. Baada ya kutangazwa Ukuta sijui hajaona dola ilivyo haha kujiandaa kijeshi utadhani ile vita tunayoambiwa yakugombania ziwa Nyasa imewadia.
Ule ulikuwa ni ushindi kwa chama kilichoandaa ushindi kwani inaonyesha salamu zao serikali imezisikia na ndio maana kila mtu alikuwa anatoa matamko na mpaka Bwana kubwa alitoa matamshi yenye utata na kujipunguzia points nyingi kwani watu wakamtambua yukoje na ana moyo wa aina gani.
Kuwasukuma tuu wanachama na wapenzi wako kuingia barabarani huku unajua kuwa kuna vichaa wamekabidhiwa silaha za moto kuwauwa hiyo sio busara, unafuta maandamano hayo kwani kama hayo ya kidemokrasia yaliyo andaliwa na yenye usimamizi hawayataki basi wasubiri kwani kuna siku watu watakasirika na wataingia barabarani bila uratibu na ndio watajua maana ya maandamano
 
Back
Top Bottom