PreGE2025 CHADEMA nendeni kwenye Uchaguzi! Polepole ndio mwendo!

PreGE2025 CHADEMA nendeni kwenye Uchaguzi! Polepole ndio mwendo!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Chadema haitashiriki uchaguzi bila Reforms bali itauzuia
Kwa vile Chadema hamtaki kusema mtazuia vipi uchaguzi basi inabidi tukisi. Njia za kuzuia uchaguzi ni kwa mojawapo ya njia zifuatazo:
1. Kwenda Mahakamani na kuomba waweke zuio kwa sababu hautakuwa wa haki. Sioni hakimu au jaji mwenye ubavu huo. Sana watasema hawawezi kuingilia mhimili mwengine. Au mtashauriwa mshiriki halafu kama hautakuwa wa haki mfungue kesi za kupinga matokeo. Lakini ikumbukwe kuwa matokeo ya kura za urais hayapingwi.
2.Kuomba taasisi za kimataifa na nchi rafiki waweke zuio. Hapo suala la sovereignity litatumika kuwakatalia.
3. Kufanya civil disobedience ili watu wasipige kura. Kwa chama ambacho hakitaki wanachama wake waumizwe, hili litakuwa gumu kutekeleza. Civil disobedience zinaweza kuwa kwa njia ya maandamano, sit ins, migomo n.k.
4 Kuwahimiza wafuasi wafanye fujo ili wale wenye nia ya kupiga kura waogope kujitokeza. Mkifanya hivi ni kufuta vifungo.

Mimi sioni lolote katika haya ambalo CDM wanaweza kufanikisha. Lakini labda wana strategy ambayo ukifika wakati muafaka ukifika wataifungulia jamii.

Amandla...
 
Back
Top Bottom