Chadema ndiyo iliyoshinda Igunga

Manyema

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
540
1,156
Uchaguzi wa Jimbo la Igunga umemalizika J2 na mshindi kutangazwa jana 3 Oktoba,2011 na msimamizi wa Uchaguzi. Kwa kufanya tathmini ya haraka haraka tu baada ya Uchaguzi na matokeo kutangazwa CHADEMA kwa uhakika kabisa ndiyo Walioshinda Ubunge huko Igunga. Nitaeleza.
  • CHADEMA wamepata kura 23,260 dhidi ya kura 26,484 za CCM.Tofauti ya kura 3,224! Tukumbuke kuwa Uchaguzi Mkuu 2010 CDM hawakuwa wamesimamisha mgombea Ubunge jimbo la Igunga. Lakini mgombea Urais wa CDM Dr.Slaa alipata kura 8,000+. Hii inaashiria kuwa CDM inapendwa na ina uhakika wa kufanya vizuri zaidi 2015.
  • CHADEMA wametumia gharama ndogo ukilinganisha na CCM chama twawala. Gharama elekezi ya Uchaguzi toka msajili wa Vyamailikuwa Tshs.80m. CCM wametumia NGUVU na GHARAMA kubwa sana kulipata jimbo hili. Tunaambiwa CCM wametumia Tshs.10 Billion!Gharama hizi lazima ziwe juu kwa vile Serikali yote ilihamia Igunga.
  • CHADEMA wametumia HELIKOPTA MOJA tu wakti CCM wametumia HELIKOPTA MBILI.
  • CHADEMA hawakutumia SERA ya UDINI kama walivofanya CCM kwa kumgeuza DC wa Igunga kuwa mtaji wa siasa za UDINI. Pamoja na siasa CHAFU za udini za CCM bado hazikufaulu. Tumeona Masheikh wakihimiza Waislamu kutoipigia CDM kura kwasababu ya kumdhalilisha DC ambaye ni Muislamu fake!
  • CHADEMA kupata KURA 23,260 dhidi ya CUF iliyopata kura 2,104 ni ushindi tosha kabisa dhidi ya SIASA CHAFU ZA UDINI(Uislamu).
  • CHADEMA wamepata kura 23,260 kwa mjini tu yaani KATA 5! Huu ni wastani wa kura 4,652 kwa kata! CCM amepata kura 26,484 tokaKATA 17! Huu ni wastani wa wapiga kura 1,557 kwa kata.Kwa maana hiyo kama CDM kikianza kujiimarisha vijijini CCM wajue watakuwa na hali mbaya sana na hawatakuwa na kitu tena Igunga 2015! CDM lazima wajifunze toka hapo kwamba KUANZISHA MATAWI YA CHAMA VIJIJINI NI KITU CHA LAZIMA NA UTAKUWA MTAJI MZURI SANA KWA GE-2015.
  • CHADEMA hawajatumia DOLA(Serikali kwa maana ya Polisi,UWT na MAWAZIRI) kujinadi Igunga. CCM wametumia POLISI,UWT na RASLIMALI za SERIKALI.
  • Kwa CHADEMA hii ni INDICATOR kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2015 utakuwa ni UCHAGUZI MKUU WA KUIMALIZA NA KUINYAMAZISHA CCM KWENYE ULINGO WA SIASA ZA TANZANIA.
Kwa vipengele hivi inadhihirisha kabisa CHADEMA ndiyo washindi wa jimbo la Igunga na siyo CCM. Kwa mara nyingine CHADEMA wameithibitishia serikali ya CCM kuwa ndicho Chama pekee cha upinzani chenye nguvu Tanzania kwa sasa! Huo ndiyo ukweli wenyewe bila kujali CCM kama watakubali au la.

Nawasilisha.​--
[FONT='comic sans ms', sans-serif]
[/FONT]
 

WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
2,920
1,228
Habari nilizozinyaka mitaani sina detail nyingi sana ni kwamba CCM ilitumia 3biln, CHADEMA 400Mln na CUF 150Mln.

CCM wamepata kura 26,484, CHADEMA kura 23,286, CUF kura 2,104....


Kwa hesabu za shule ya msingi ni kuwa

CCM-3,000,000,000/26,484=113,275/=

CDM-400,000,000/23,286=17177/=

CUF-150,000,000/2,104=71,292/=

Hivyo basi
CCM imegharamikia kura moja kwa tsh 113,275/=

CDM imegharamikia kura moja kwa tsh 17,177/=

CUF imegharamikia kura
moja kwa tsh 71,292/=


CDM ndiyo washindi Igunga.
 

Escobar

JF-Expert Member
Sep 16, 2011
574
439
Habari nilizozinyaka mitaani sina detail nyingi sana ni kwamba CCM ilitumia 3biln, CHADEMA 400Mln na CUF 150Mln.

CCM wamepata kura 26,484, CHADEMA kura 23,286, CUF kura 2,104....


Kwa hesabu za shule ya msingi ni kuwa

CCM-3,000,000,000/26,484=113,275/=

CDM-400,000,000/23,286=17177/=

CUF-150,000,000/2,104=71,292/=

Hivyo basi
CCM imegharamikia kura moja kwa tsh 113,275/=

CDM imegharamikia kura moja kwa tsh 17,177/=

CUF imegharamikia kura
moja kwa tsh 71,292/=


CDM ndiyo washindi Igunga.

Fantastic break down, nimeipenda! Magamba wanatumia pesa vibaya mno, kuna mdau kanidokeza kuwa kuna fungu lingine lilitumika kulipia ugoni sasa sijui itapelekwa risiti gani kwenye kamati ya matumizi.
 

Mzee Wa Rubisi

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,758
437
Habari nilizozinyaka mitaani sina detail nyingi sana ni kwamba CCM ilitumia 3biln, CHADEMA 400Mln na CUF 150Mln.

CCM wamepata kura 26,484, CHADEMA kura 23,286, CUF kura 2,104....


Kwa hesabu za shule ya msingi ni kuwa

CCM-3,000,000,000/26,484=113,275/=

CDM-400,000,000/23,286=17177/=

CUF-150,000,000/2,104=71,292/=

Hivyo basi
CCM imegharamikia kura moja kwa tsh 113,275/=

CDM imegharamikia kura moja kwa tsh 17,177/=

CUF imegharamikia kura
moja kwa tsh 71,292/=


CDM ndiyo washindi Igunga.

Mkuu data ziko bomba,Simple research
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom