CHADEMA, NCCR-MAGEUZI NA CUF someni hapa

CHADEMA, NCCR-MAGEUZI NA CUF someni hapa

Baba Clara

Member
Joined
May 10, 2011
Posts
94
Reaction score
27
NASHUKRU CHADEMA,NCCR-MAGEUZI na CUF MMEFATA MAONI YANGU KUTOKA KWENYE MAKALA YANGU ILIYOTOKA GAZETI LA FAHAMA LA FEBRUARY 2013,Nimechukua swali moja tu kati ya maswali 15 niliyojibu siku hiyo;

1.Unaelezeaje siasa za vyama vya upinzani nchini kwa ujumla, unadhani vinalenga ukombozi wa kweli kwa wananachi ama ni maslahi binafsi?


Kisandu; Siasa ya vyama vya upinzani nchini ni siasa isiyo kuwa na mshikamano, historia inajionesha kuwa kipindi cha Mh.Mrema NCCR-mageuzi ilipokuwa na nguvu vyama vingine havikuwa tayari kukiunga mkono ili chama hicho kishinde, na kipindi chama cha TLP kilipokuwa na nguvu pia vyama vya upinzani havikuwa tayari kusapoti chama hicho ili kishinde, vilevile kipindi chama cha CUF kilipokuwa na nguvu vyama vya upinzani bado havikutaka kuonesha ushirikiano wa kutaka ushindi na kipindi chama cha CHADEMA kilipokuwa na nguvu vyama havikutaka kuisapoti. Nahii yote inasababishwa na maslahi binafsi, moja chama kimoja kikiungwa mkono na kikashinda hicho ndicho kitakuwa chama tawala na jina la chama hicho litakuwa kubwa na vyama vingine vitamezwa kabisa hata kama viongozi wake watakuwa na nafasi katika serikali na hii ndio inayosababisha vyama vya upinzani kushindwa kuungana.Pia kila chama kinajiona kina nguvu kuliko chenzake hasa kutokana na maslahi binafsi, kwa mfano CHADEMA wamekuwa natabia ya kuviambia vyama vingine vinatumika na CCM na kuviita CCM B wakati haohao ndio wanaongoza kwa kutumika na CCM, mfano mzuri mwenyekiti wa kambi ya upinzani alikataa gari la serikali na nyuma ya pazia akalifata.

Mh. James Mbatia alipo ibuka na hoja yake ya mitaala ya elimu na kuamua kutoka nje kwa kutorizishwa na Spika, hapo ndipo unafiki wa vyama vya siasa ulipooneka baada ya CHADEMA, CUF,TLP na UDP kuungana na Mbatia kutoka nje wakijiadai wanasapoti wakati haohao wanapenda kuwaita wenzao CCM B na walifanya hivyo si kwa nia njema bali kwa kuogopa kumezwa kisiasa, pamoja na yote CHADEMA walitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa kutakuwa na mkutano wa hadhara na maandamano ya vyama vya upinzani TEMEKE kupokea wabunge wa upinzani lakini kinyume chake chama cha CHADEMA kilitumia mgongo wa vyama vya upinzani hasa hoja ya mbatia ili kupata watu wengi kwenye mkutano tena hata vyama vya upinzani havikupewa taarifa yoyote kuhusu mkutano huo. kwa hali hii vyama vya siasa havina nia ya dhati ya Ukombozi wa watanzania bali vinalenga maslahi binafsi na sio kuiondoa CCM madarakani. Ushauri wangu katika hili kama serikali ikibadilisha mfumo, sheria itakuwa nzuri ili vyama vikiungana vyote vinatumia jina moja na hii ikifanikiwa itakuwa ni rahisi kuiondoa CCM.Na kama hii haitawezekana basi vyama vikubaliane kuachiana majimbo na kusapotiana pamoja na kupendekeza mgombea urais anayekubalika, tukifika hapa tutashinda na ukombozi wa kweli utapatikana.( kutoka wall ya FB ya Deo Kisandu)
 
Huyo bwana Kisandu ni mpotoshaji mkubwa, CDM mara zote imekua ikiunga mkono vyama vingine vya upinzani mfano ni uchaguzi mkuu wa kwanza CDM waliiunga mkono NCCR kwenye uraisi, Pia walishawahi kuwapigia kampeni ya uraisi CUF, lakini vyama vingine havijawahi kuwapigia kampeni CDM hata siku moja. Chama cha upinzani cha ukweli ni CDM pekee wengine ni CCM B na vipo kwenye siasa kwa nia ya kuvuruga watanzania.
 
Wapinzani watakuwa wamefanya kosa kubwa kama wakiamini kila chama cha upinzani ni wapinzani kweli, wengine hutumiwa na ccm ili kuvuruga upinzani!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom