Chadema nafasi ni hiyo tumieni!!

Lilombe

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
242
39
Nikiwa mtanzania mwenye uchungu na adha waipatayo walalahoi katika hospitali za serikali, chonde chonde uongozi wa CHADEMA uwaangukie madaktari kokote walipo na wawaombe warudishe majeshi, kwani uongozi wa CCM unachojali ni maisha yao tu na pamoja na familia zao.

Dr. Slaa tumia fursa hiyo kukutana na madaktari, kwani madaktari wanachohitaji hivi sasa ni faraja ili warudi kuwatumikia watz wenzao. Hiyo fursa ni adimu sana, thubutuni kuitumia na kurejesha imani kwa watanzania kuwa mnaweza kumaliza migogoro hatimaye watz wakapata huduma bora.

Natumaini baadhi ya washauri wa Dr. Slaa na Mbowe mpo hewani JF, tafadhali pokeeni ushauri wangu, MTAFAIDIKA SANA KISIASA NCHINI TANZANIA!!
 
Huu ushauri mwingine!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!11yaani unamwambia kikwete aendelee kunywa chai ulaya ila unawashauri dr.slaa kutumia nafasi hiyo?tuandamane akina kikwete warudishe miposho wanayotapanya na maswahiba wao ktk ziara za kutafuta wawekezaji hewa wkt nchi haina umeme...........nchi haina dawa......nchi haina waalimu na madaktari na waliopo hawalipwi........hivi kwa nini wakati wote hamtaki kufikiria kumfukuza kazi kikwete?..........kwani anakazi gani tangu alilie urais na kupewa viatu ambavyo kamwe hawezi kuvivaa kwani pale ni mahali patakatifu lakini yeye kapafanya pango la walanguzi akina rostamu,lowasa na familia yake...................?????????????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!1111111
 
chonde chonde uongozi wa CHADEMA uwaangukie madaktari kokote walipo na wawaombe warudishe majeshi, kwani uongozi wa CCM unachojali ni maisha yao tu na pamoja na familia zao.

Dr. Slaa tumia fursa hiyo kukutana na madaktari, kwani madaktari wanachohitaji hivi sasa ni faraja ili warudi kuwatumikia watz wenzao. Hiyo fursa ni adimu sana, thubutuni kuitumia na kurejesha imani kwa watanzania kuwa mnaweza kumaliza migogoro hatimaye watz wakapata huduma bora.



Tatizo hawa viongozi wa CHADEMA wakiongea na Madaktari hawatawasaidia kwani CHADEMA haiwezi ktoa ahadi ya kuboresha maslahi na huduma za Hospitali kama ilivyo kwenye madai ya Madaktari.

Serikali inatakiwa kuwajibika kwa hili.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!!
 
Cdm wanaingiaje hapa plz msiingilie acheni wananchi wapambane na serikali yao teule!
 
Tatizo letu tunakunywa chai siasa, lunch siasa na Dinner pia Siasa...

Hapa tuangalie hoja na sio chama basi hata Chadema wakipata nchi si mtakuja kuwachosha hao wakina Slaa na chadema Kwani kuna vitu sio tu havitekelezeki Bali utekelezaji wake unahitaji Fedha na Kumbuka Drs ni sehemu tu ya watumishi katika Jamii..

Maana yangu hapa ni kua tusitegemee pepo toka kwa chadema Au chama chochote tunachopaswa kuangalia na kufuatilia ni jinsi gani system itatuongoza bila kujali ni chadema Au CUF Au CCM ili system nzuri iwe ndio Dira na Si Mtu Kwani hata huyo Mtu haishi milele Kama waliowahi kuwepo na wengi sasa hawapo, eg JK Nyerere,Nkrumah na wengine wengi.... Tunahitaji ni kubuni mifumo ambayo ndio iwe miongozo kila Mtu aifuate....


Tuache mtindo wa kupenda Mtu badala ya Mfumo... Na hili ndio mAana most of us we tend to follow individual at the office instead of services...
 
Hivi ni kweli wagonjwa ambao ni wanachama wa chadema wanaomba mgomo uendelee?
 
Nadhani tujiulize tu wagonjwa ambao ni wanachama wa chadema nao wanapenda mgomo uendelee ? Nyie msifanye mchezo na kuumwa Au kupata ajali ....

Watu wanateseka sana usiwe Kama mwenye shibe hamjui mwenye njaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom