CHADEMA na Vyama visipofanya haya visahau kuhusu kuchukua nchi milele

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
2,829
3,824
Habari Wana jamvi la jf.

Moja kwa moja niende kwenye bandiko.nimetafakari Sana kuhusu vyama pinzani hapa nchini jinsi vinavyoendesha siasa zao na progress za vyama hivi miaka nenda ,miaka rudi bado patupu,hata wao wenyewe ukiwauliza hawatoi jibu ambalo ni touchable,watakuja na simple excuse, binafsi naona haya ndio yanayowaghalimu chadem na wengine,

1. hawana mipango endelevu- si chadema ,au wengine ,mipango yao huwa Niya msimu tu,hasa pindi za chaguzi ,ukiwasikiliza kipndi Cha harakati za uchaguzi huwa wanaonekana wanamipango kabambe ,lkn uchaguz ukiisha tu Basi wameshapoteana utaona kila siku wanakuja na Jambo geni,tofauti kabisa na sura waliyokuwa nayo kpnd Cha harakati za uchaguzi, ni Kama mtu aliekuwa usingzn alipoamka akaja na agenda aliyoiota usngzn!!
,niwashauli chadema na wengine muwe na long-term plans ,hata siku mbowe hayupo atakayekuja basi aanzie pale alipoishia mbowe, sio Mbowe asipokuwepo basi mnaanza upya tena
,mko serious kuchukua dola kweli!!?,mfano mdogo tu hv kweli kale kajumba Cha chumba sebule ndo Makao makuu ya chadema kweli,u guys mko serious kweli na plans zenu!!??,atleast basi muwe mnajifunza basi hata kutoka kwa wapinzani wenu ccm.

2. kwao viongoz ni Yule anayejua kupiga maneno ,na sio mtu creative!!, Hawa ndugu zangu hili ni tatzo kubwa ,jaribu kufuatilia viongoz wengi vyama pinzani ni mafundi wa kupiga maneno ,Ila creativity zero,mtu creative hujenga chama na kukifanya kiwe na nguvu na ushawishi kwa watu,kwa jinsi anavyopanga plan na namna ya kuwapanga watu wake,chadema walibahatika kuwa na mtu wa namna hii ,Dr.slaa na chacha wangwe Kama sijasahau,Dr.slaa alikuwa ni creative na good planner ,sote tuliona impact yake kpnd hicho.baada ya hawa watu kutoka chama kikapoteana.

3. Kwao chama pinzani , ideology ni kupinga anything kwa opposition wao!!,hili ni tatizo kubwa kwa vyama vyetu vya upinzani ,na hii inasababishwa na kuwa na viongoz ambao sio creative bali talkative,sijui ni kiingereza ndo shida
,huenda walielewa opposition parties =chama Cha kupinga/kutokukubaliana.kimsingi foundation ya chama pinzani ni ku challenge,na ku challenge ni kuja na wazo lenye mvuto zaidi ya mpinzani wako.kama ccm wamekuja na agenda ya bwawa la mwal.nyerere usipinge kwa kuleta hoja za mazingira n.k huku ukijua ,nchi ina uhitaji mkubwa wa umeme ,njoo na wazo jingine lenye mvuto ambalo halitoi uhalisia wa adha ya umeme ipo, Sasa mfano ukija na kisingizio Cha mazingira nn plan forward ambayo itatoa adha hiyo ya umeme na ambayo itakuwa affordable!!? chadema na wengine mjifunze ku appreciate & ku challenge!!!

4. Umoja wa kudumu -hapo juu nimesema mjifunze ku appreciate,hii itawafanya mje na wazo lenye kum challenge mpinzani wenu,chadema na wengine kwanza mkubali wote kwa moyo mmoja kwamba ccm ni chama kikubwa,kikongwe ,chenye nguvu kubwa,ushawishi wa kila style(whatever the style they use),na mikakati ya kudumu,kukubaliana na hayo kutawapa wazo la nn mfanye kuwa beat ccm!! the only option ni kuungana ,labda niwakumbushe vyama pinzani,hiyo ccm mnayoiona leo ,imeungana na vyama kadhaa miaka hiyo enz za mwal.mfano , Kama sijasahau TAA ,na ASP ,ikawa TANU,n.k hivyo ccm tu imepitia huko kwenye kutafuta nguvu kwa kuunganisha vivyama vidogo vidogo kadhaa hatimae ikawa ccm hii mnayoiona leo. ndio maana nikawaambia mjifunze ku appreciate & ku challenge!!!

kui beat ccm, sio Kazi rahisi,Kama mnavyochukulia, learn to appreciate & challenge!!
 
Habari Wana jamvi la jf.

Moja kwa moja niende kwenye bandiko.nimetafakari Sana kuhusu vyama pinzani hapa nchini jinsi vinavyoendesha siasa zao na progress za vyama hivi miaka nenda ,miaka rudi bado patupu...
Kwa miaka 60 ya uhuru bado WATANZANIA ni masikini wa kutupwa.

Kuna wananchi wanaishi kwa kupata mlo mmoja tu kwa siku.

Kuna watoto wanasomea chini ya miembe, wanakalia matofali na wanajisaidia vichakani.

Wananchi wanakosa maji masafi ya kunywa na kulazimika kutumia maji pamoja na mifugo.

Alafu anakuja mjinga mmoja kama wewe unaimba mapambio ya kuisifu ccm!
 
Mbona huwa wanashinda ila Kura zinaibwa ?!!!

Ccm hawajawahi kushinda nje ya kongwa au mkoa wa dodoma.
 
Hili swali liwe directed kwao. Kwanini wanaibiwa kura halafu no action?
 
Mods weka sawa heading ,chadema na vyama vingine ,visipofanya haya visahau kuhusu kuchukua nchi milele!!
 
Ccm hawajawahi kushinda nje ya kongwa au mkoa wa dodoma.
Hii inajenga taswira mbaya sana kwenu kama mnashinda kura nchini nzima halafu mnakuwa wadhaifu kutetea ushindi wenu. Na usiniambie vyombo vya dola ksb hata Zambia vipo lakini bado Lungu alitoka.
 
Habari Wana jamvi la jf.

Moja kwa moja niende kwenye bandiko.nimetafakari Sana kuhusu vyama pinzani hapa nchini jinsi vinavyoendesha siasa zao na progress za vyama hivi miaka nenda ,miaka rudi bado patupu...
Ndani ya Miaka 60 ya Uhuru kijana maoni kamaa huyu huenda ana Degree anaandika Hovyo namna hii, hajui kutofautisha R na L eti anaishauri CDM Ee Mwenyezi Mungu ponya taifa lako
 
Hii inajenga taswira mbaya sana kwenu kama mnashinda kura nchini nzima halafu mnakuwa wadhaifu kutetea ushindi wenu. Na usiniambie vyombo vya dola ksb hata Zambia vipo lakini bado Lungu alitoka.
Inawezekana unaishi north korea au south sudan
 
Ndani ya Miaka 60 ya Uhuru kijana maoni kamaa huyu huenda ana Degree anaandika Hovyo namna hii, hajui kutofautisha R na L eti anaishauri CDM Ee Mwenyezi Mungu ponya taifa lako
Hao vijana tayari walisha haribiwa na huyo huyo chakubanga
 
Inawezekana unaishi north korea au south sudan
Usikimbie mapungufu yenu. Mnashindwa kuingiza watu barabarani na wananchi hawana imani ya kupambana kwa ajili yenu toka ile incidence ya Lowassa. Mnahitaji new blood .
 
Lugha ya KUCHUKUA nchi ife mara mmoja, ni lugha ya hovyo, nchi inapaswa kuwa ya wananchi siku zote na hakuna anayepaswa kuichukua.
 
Usikimbie mapungufu yenu. Mnashindwa kuingiza watu barabarani na wananchi hawana imani ya kupambana kwa ajili yenu toka ile incidence ya Lowassa. Mnahitaji new blood .
Ingia wewe itasaidia
 
Wananchi hawapaswi kupambana kwa ajili ya watu wachache, wanapaswa kupambana kwa maslahi na mustakbali wao wenyewe na wa watoto wao.

Huo msemo alikuwa nao jiwe eti nchi yangu, wananchi wangu
 
Wananchi hawapaswi kupambana kwa ajili ya watu wachache, wanapaswa kupambana kwa maslahi na mustakbali wao wenyewe na wa watoto wao.
Kwa mantiki hiyo tusiwe na viongozi na wananchi wapambane kivyao.
 
Habari Wana jamvi la jf.

Moja kwa moja niende kwenye bandiko.nimetafakari Sana kuhusu vyama pinzani hapa nchini jinsi vinavyoendesha siasa zao na progress za vyama hivi miaka nenda ,miaka rudi bado patupu...
Ninakubaliana na baadhi ya hoja zako ila kwenye namba 1&4 kwenye kuwa na majengo ya kisasa kama ccm na kwamba ccm ni chama chenye maendeleo hapo ndipo kwenye point yangu; rudi nyuma wakati wa kuanzisha vyama vingi; early 1990s resources zilizokuwepo (majengo, viwanja, magari na fedha) za chama kimoja hazikutakiwa kubaki kwa chama kimoja pekee, kwa kufanya hivi kumekosekana usawa wa kupambana...ni kama anapambanishwa mike tyson (ccm) na akina twaha kiduku (chadema), dulla mbabe (act wazalendo).

Kama resources hizi zingegawanywa sawa hapo tungeweza kuwalaumu hawa vyama vingine. Yes wanapata ruzuku hata ccm nayo inapata ruzuku tena kubwa tu na wanatumia ruzuku hiyo kwenye mambo mengine kwa kuwa majengo tayari walikuwa nayo toka enzi na enzi ambayo mengi yalijengwa kwa fedha za walipa kodi.

Pili, kukosekana kwa Tume huru ya uchaguzi kunawanyima upinzani fursa ya kushinda. Polisi, NEC, Msajili wa vyama vya siasa, Mahakama and other state aparatus zipo upande wa ccm. Hata hivyo, bado kuna udhaifu upande wa viongozi wa upinzani na mikakati yao towards domination of state power.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…