VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Sakata a Zitto Z.Kabwe lina sura nyingi. Zipo zinazoonekana mbaya na zile nzuri. Mimi nimechagua sura hii.Sura ya ukomavu wa kisiasa na kitasnia ndani ya chama hicho. Sijui kama ni sura mbaya au nzuri. Najikita katika mapambano ya kisheria yalliyotukia Mahakama Kuu ya Tanzania,Kanda ya Dar es Salaam ambapo Zitto 'anatafuta' haki yake.
Tuanze na Mawakili. Zitto ana Wakili Albert Msando.CHADEMA wana Mawakili Tundu Lissu na Peter Kibatala. Ndani ya chama,Mawakili hawa wote wana nafasi za kiuongozi. Wakili Msando ni Diwani wa CHADEMA katika Kata ya Mabogini,Moshi. Wakili Lissu ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA,Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki.Wakili Kibatala ni Mkurugenzi wa Sheria wa CHADEMA. Wote wa pale pale CHADEMA.
Mawakili hawa juzi na jana, wamepambana kwa hoja wakisahau pande zao wanazoziwakilisha katika shauri husika. Pande ni Zitto Kabwe dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA pamoja na Katibu Mkuu wa CHADEMA. Wamoja wanapigania kitu kimoja:haki. Wanaamini kuwa siasa ni kitu kimoja na tasnia yao ya Sheria ni kitu kingine. Hakuna hata mmoja aliyehama kwenye hoja na kujikita kwenye mashambulizi ya nafsi. Ukomavu wa kitasnia usioelezeka.
Pande za kesi husika kama nilivyozitaja hapo juu nazo ni kutoka sehemu moja: CHADEMA. Yaani CHADEMA inapambana na CHADEMA kusaka haki. Ni ukomavu wa ajabu kabisa.Sijapata kuuona popote katika siasa za Tanzania.Hongereni sana CHADEMA!
Kimsingi, kila upande kupitia Mawakili wake una imani na Mahakama.Kwamba Jumatatu, watasikiliza na kukubaliana na uamuzi wa Mahakama katika kilichowapeleka pale. Watakwenda kutekeleza uamuzi husika.Hakuna haja ya tashwishwi na mihemuko isiyo na maana. CHADEMA ni ya wana-CHADEMA. Watarudi chamani mwao na kumalizia kiporo cha mambo yao.
Kila la kheri!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam