Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Sijajua ni wapi UKAWA wameteleza mpaka wamepoteza mwelekeo kiasi hiki. Pamoja na mambo mengi waliyoandika kwenye taarifa yao juu ya maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kujaa uongo na upotoshaji, hakika mwanzo na mwisho wa Hotuba hiyo unajichanganya. Sijajua kama aliyeanza kuwasilisha alipatwa na ganzi kiasi ambacho akashindwa kumalizia na hivyo kumuomba mwingine amalizia ama la.
Mchezo umeanza hivi, ukisoma kichwa cha Maoni hayo ya Upinzani, Halima Mdee anatajwa kama ndiye anayewasilisha taarifa hiyo Bungeni. Ila kituko kinakuja walipomalizia. Taarifa inamalizia kwa kumtaja David Silinde kuwa ndiye aliyewasilisha taarifa hiyo. Hii ni aibu kubwa sana kwa upinzani. Kama hawajui hata protocali za kuandika hotuba, watawezaje kuongoza nchi?
By the way Mwakyembe alishasema kuwa Msomi na Muungwana huongea pale tu anapokuwa na cha kuongea ila mbumbumbu husema tu hata kama hana cha kusema. Ndio hali inayowatokea UKAWA sasa.