CHADEMA NA TANU: Mfanano na Tofauti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA NA TANU: Mfanano na Tofauti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchambuzi, Sep 19, 2012.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Awali ya yote, naomba ieleweke kwamba shughuli ya kujadili Mfanano/Ulingano na Tofauti baina ya TANU na CHADEMA ni shughuli ngumu sana kwani hakuna any proven methodlogy au analytical framework yenye kuweza kusaidia katika reliability & validity for such an analysis; Lakini pamoja na hali hii, bado jitihada hii ni muhimu kwetu sote, hasa angalau kutupatia PAHALI PA KUANZIA. Tukifanikiwa katika hili, tutakuwa kwenye nafasi bora zaidi ya kuelewa Historia ya kisiasa ya nchi yetu kwa undani zaidi, na pia itatusaidia kuweka harakati za sasa za CHADEMA in the Right Context;

  Kauli ya hivi karibuni ya Mzee Pius Msekwa (Katibu Mkuu wa Kwanza wa TANU) iliyolinganisha Chadema na TANU ilikuwa sahihi lakini pungufu. Mzee Msekwa "SAID THE RIGHT THING, BUT HE DID NOT SAY IT RIGHT". Mzee Lusinde, ambae pia alikuwa mMoja wa viongozi wa mwanzo wa TANU nae alimfuatia Msekwa na kuja na kauli yake ambayo kidogo ilikuwa imeshiba kuliko ile ya Msekwa. Mzee Lusinde aliweka wazi kwamba Chadema ipo tayari kukamata dola 2015. Hii ni tofauti na kauli ya Mzee Sitta aliyoitoa hivi karibuni kwamba Chadema hakipo tayari kwa hilo.

  Ni dhahiri kwamba mjadala wangu utakuwa na mapungufu mengi, lakini AGAIN, nia yangu kuu ni kwamba: Angalau Tuwe na Sehemu ya Kuanzia; Ni matumaini yangu kuwa mjadala huu utafanikisha mambo makuu matatu yafuatayo:


  • Kwanza tutakuwa tumepata angalau sehemu ya kuanzia mjadala;
  • Pili, tutaiweka Chadema katika muktadha sahihi (right context) tofauti na sasa ambapo mjadala juu ya ulingano baina ya Chadema na TANU unapotoshwa, unakuwa ‘hijacked', na kupelekea suala hilo kuwa ‘A POLITICAL LIABILITY' badala ya ‘A POLITICAL ASSET', kwa Chadema; Ukweli ni kwamba, ulingano huu ni ‘A POLITICAL LIABILITY' kwa CCM, Sio ‘A POLITICAL ASSET'.
  • Tatu, ni matumaini yangu kwamba mjadala huu utatusaidia kuelewa kwa undani zaidi mapungufu na Changamoto zinazoikabili CCM, lakini vile vile Chadema.

  Mjadala wangu utakuwa na sehemu kuu nne kama ifuatavyo: Sehemu ya kwanza ni kuweka mjadala kwenye muktadha sahihi (right context); Sehemu ya Pili itajadili kwa kina ULINGANO [KIMSINGI], uliopo baina ya vyama hivi viwili; Sehemu ya tatu itajadili TOFAUTI [KIMSINGI], zilizopo baina ya vyama hivi viwili; na Sehemu ya nne itakuwa ni hitimisho. Reference zitakazotumika kwenye mjadala huu zipo UPON REQUEST!

  SEHEMU YA KWANZA: Kuweka Mjadala kwenye MUKTADHA SAHIHI (Right Context).

  Kwa muda mrefu sasa, mijadala inayohusisha ulingano na tofauti baina ya TANU na Chadema imekuwa inapokewa kwa hisia tofauti, lakini hasa, hisia za wengi ni kwamba mijadala hii inaipa CCM mtaji wa kisiasa kuliko Chadema. Tukifanikisha kuweka mjadala huu katika muktadha wake (right context), Wapenzi wa Chadema watafanikiwa kugundua kwamba ulingano wa chama chao na TANU unakipa Chadema ‘more political mileage' kuliko baadhi yao wanavyofikiri.

  Kabla ya kuendelea, ni muhimu nikatamka kwamba nia ya Nyerere kufuta mfumo wa vyama vingi mwaka 1965 haikuwa mbaya kwani ililenga kuongezea nguvu juhudi za kujenga umoja miongoni mwa watanganyika waliogawanywa vipande vipande na sera za ukoloni. Isitoshe, Chama cha Upinzani cha African National Congress (ANC) cha Zuberi Mtemvu ambae alijiondoa TANU, hakikufanikiwa kuungwa mkono na watanganyika wengi kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza kama ilivyokuwa kwa TANU; Lakini huu ni mjadala tofauti;

  Vinginevyo, matunda ya uamuzi wa Mwalimu tunayaona hadi leo ambapo Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika ambazo kwa kiasi kikubwa zilizofanikiwa kisiasa katika kipindi chote vurugu za COLD WAR ambazo zilishuhudia mapinduzi mengi, umwagaji damu n.k. Kati ya vipimo vya mafanikio ya kisiasa (relative na nchi nyingine nyingi Afrika) ni amani, utulivu, udugu, umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania, vitu ambavyo havitakiwi kubezwa. Lakini ni dhahiri kwamba mafanikio haya ya kisiasa yalikuja na Gharama zake, lakini hasa - Hali duni kiuchumi miongoni mwa watanzania wengi; Ni ndoto hizi za ukombozi wa kiuchumi miongoni mwa watanzania wengi leo, ndio zinachangia kwa kiasi kikubwa nguvu ya Chadema kwani watanzania wengi wanazidi kubaini kwamba katika hili, CCM imeishiwa ubunifu.

  Kushindwa kwa CCM kuinua hali za watanzania kuchumi maana yake ni kwamba watanganyika waliokiunga mkono TANU, kwa muda mrefu sasa wamebakia kuwa kama WAKIWA (they feel betrayed and abandoned by CCM). Swali linalofuatia ni JE: Wakimbilie wapi iwapo CCM imeisailiti historia yake yenyewe? Inazidi kujidhihirishwa kwamba majibu kwa wengi ni Chadema. Quote ifuatayo kutoka kwa Mwalimu Nyerere inazidi kuthibitisha hoja hii:

  ["In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU"].

  Source: Socialism & Participation: Tanzania's 1970s National Elections: The Election Study Committee, University of Dar-es-salaam, 1974):
  ****

  TANU ililenga kuwakomboa watanganyika na kuwapatia haki za kisiasa, kiuchumi na kijamii (Political, Economic and Social Justice). Katika hili, mikakati na sera za TANU kupitia kauli za viongozi wake ndio zilisaidia TANU kuungwa mkono kwa wingi sana kwani watanganyika wengi waliamini kwamba ndoto na matarajio yao yatafanikiwa kupitia TANU. Kwa mfano, Mwongozo wa TANU (1971) unatamka kwamba:

  ["We have been oppressed a great deal. We have been exploited a great deal. It is our weakness that has led to our being oppressed, exploited and disregarded. Now we want a revolution – a revolution which brings to an end our weaknesses so that we are never again exploited, oppressed or humiliated."]

  Bila ya kauli kama hizi, TANU isingeweza jipenyeza masikioni na mioyoni mwa watanganyika wengi. Na kwa vile hali za maisha ya watanzania wengi hazijabadilika kwa miaka 50 sasa, mtaji wa Chadema ni ule ule kama wa TANU – kutoa kauli kama hizi kwa watanzania, kwa matarajio kwamba wakipewa dhamana ya kuongoza taifa, watatekeleza kauli zao kwa vitendo. Bila ya Chadema kuja na kauli kama zila za TANU, haitakuwa rahisi kwa chama hiki kufanikisha azma yake ya 2015; Muhimu zaidi hapa ni kwamba, iwapo TANU ilitumia maneno kama haya ndani ya uhuru, Chadema ikitumia kauli za namna hii sio uchochezi bali ni kielelezo kwa wananchi juu ya uhalisia wa mambo. CCM kufikiria vinginevyo ni kusaliti historia yake yenyewe.

  TANU ilitumia mikakati mingi ambayo Chadema inajaribu kufanya sasa, hasa kupitia M4C. Kama vile TANU ilivyobaini nini wananchi wanataka kusikia, Chadema nayo ina haki hiyo hiyo. Kwa mfano, katika chapisho la TANU na RAIA (1962), Nyerere anasema hivi:

  ["Sisi hatuwezi kuacha watu wetu wazidi kuendelea kukaa katika hali ambazo tunajua kuwa hazifai. Hatuna budi tuwaamshe. Lakini katika kuwaamsha ni lazima tushirikiane nao. Ni lazima tukae nao pamoja tutaje ubovu huo tunaouona katika maisha yao, tuzungumze nao juu ya ubovu huo mpaka wautambue."]

  Nia ya M4C ya Chadema nayo ni amsha amsha kama ya TANU, na CCM kufikiria vinginevyo ni kusaliti historia yake yenyewe.

  Kuhusu PEOPLE's POWER au NGUVU YA UMMA, TANU iliheshimu dhana hii. Kwa mfano, Nyerere alielezea umuhimu wa kuheshimu Nguvu ya Umma wakati alipokuwa akifafanua juu ya sababu zilizopelekea CCM kufukuza baadhi ya wabunge wake mwaka 1968:

  [But there are also leaders, not MPs who by their conduct have assumed airs which once are anti-people and anti – party…Their common denominator is their usurpation of the power of the people. They have forgotten that power in our country derives from the people and therefore those entrusted with it, should respect the people. Such leaders are those who shout loudest about the rights of the UMMA (PEOPLE), but are themselves quick to trample these rights down and have the arrogance to so abuse their power ‘in the name of the PEOPLE'. These are the leaders who think that THE PEOPLE is an abstraction, and that to promote development they must substitute the PEOPLE's CONSENT with FORCE…; Disrespect for the PEOPLE and disrespect for their HUMANITY is dangerously anti – party action. Both groups must be disciplined so that there can be no doubt about the supremacy of the party, the source of POWER, the accountability of POWER and the purpose of POWER".] Source – The Nationalist, Editorial, ‘Party Discipline, October 16, 1968.

  Kwa maelezo haya, bila shaka mienendo ya baadhi ya viongozi wa CCM kubeza dhana ya NGUVU YA UMMA inayotumiwa na Chadema, pia ni CCM kusaliti historia yake yenyewe. Na kama TANU ilitekeleza vyema dhana hii, Chadema nayo wana haki ya kuitekeleza kwani hii ni nguzo muhimu pengine kuliko zote za demokrasia.

  Ni matumaini yangu kwamba mpaka sasa angalau tumejenga muktadha sahihi (right context) ya mjadala kama nilivyoahidi. Lakini tukielekea katika sehemu ya pili ya Mjadala huu, ni muhimu tukaingia huko tukitambua kwamba CCM SIO TANU, kwani TANU ilikufa na Tanganyika. Tutaliona hili zaidi baadae.

  SEHEMU YA PILI: Mfanano baina ya TANU NA CHADEMA

  Mfanano baina ya TANU & Chadema upo katika maeneo makuu nane (8) kama ifuatavyo:


  • Asili ya vyama hivi ni TANGANYIKA, SIO TANZANIA;
  • Aina ya harakati zinazoendeshwa;
  • Asili ya Upinzani dhidi ya TANU inafanna na ile dhidi ya Chadema;
  • Waasisi wake wanafanana;
  • Harakati zao zilianzia mijini kabla ya vijijini;
  • Matumizi ya sera ya kuajiri viongozi (recruitment of leaders) kuliko sera ya kurithisahana uongozi (leadership succession);
  • Chimbuko la vyama hivi ni SAUTI YA WANYONGE;
  • Vyama vyote vina Msimamo Mkali dhidi ya Ufisadi/Rushwa;


  1. Asili TANU & CHADEMA NI TANGANYIKA, SIO TANZANIA
  TANU
  haikuwa na mizizi Zanzibar kwa sababu za kihistoria na haikutarajiwa kuotesha mizizi Zanzibar; ni CCM ndio iliyofanikisha hilo lakini "ONLY BY MEANS OF POLITICAL PARTNERSHIP WITH Afro Shiraz Party". With all due respect to the UNION, The END was justified lakini tatizo lipo kwenye the MEANS towards that END, na hiki ndio chanzo cha kuyumba kwa Muungano wetu, kwani umejengwa kwa msingi dhaifu.

  Chadema kama ilivyokuwa TANU, nayo haina mizizi Zanzibar na haitarajiwi iwe na mizizi Zanzibar na haina haja ya kupoteza muda na rasilimali zake just to please msajili wa vyama vya siasa, hasa chini ya muundo mbovu wa muungano uliopo, na badala yake itumie muda mwingi na rasilimali zake kushinikiza muundo sahihi wa muungano (serikali TATU); lakini iwapo Chadema wameridhika na muundo wa sasa, na kama ina ina malengo ya kujijenga zanzibar chini ya mfumo mbovu wa sasa wa Muungano, ili kufanikiwa, basi ni lazima Chadema nayo iingie into ‘A POLITICAL PARTNERSHIP' na chama kingine cha Siasa chenye mizizi ZANZIBAR. Vinginevyo, mpaka kufikia hatua hiyo, Chadema itabakia kuwa Chama cha Tanganyika kama ilivyokuwa TANU, na shughuli za Chadema upande wa pili wa muungano zitaendelea kuwa zile tu za kutekeleza Sheria ya Vyama Vya Siasa ya 1992 na sio vinginevyo.

  2. Aina ya harakati zinazoendeshwa;
  Watanganyika walijiunga na TANU kwa wingi kwa imani kwamba TANU ndio MKOMBOZI wao – wa kufanikisha harakati zao dhidi ya utawala dhalimu wa kikoloni uliowanyima haki za kisiasa, kijamii na kiuchumi i.e. injustices in all spheres of life – Political injustice, Social Injustice & Economic Injustice; Ni kutokana na haya, TANU ikafanikiwa kuwa Chama kinachogusa maisha ya wananchi wengi kuliko chama kingine chochote, lakini muhimu zaidi, TANU ikawa chama kilichokuwepo midomoni, masikioni na moyoni mwa watu wengi kuliko chama kingine chochote cha Siasa Tanganyika.

  Chadema nayo inafanania na haya kwa kiasi kikubwa sana:
  Kwanza, wananchi wengi wa Tanganyika (BARA) wanaona hiki ni chama chao cha ukombozi katika nyakazi hizi na wanazidi kujiunga na harakati za Chadema kwa maelfu kila kukicha; Kikijipanga vizuri, Chadema kitakuwa ni chama cha kwanza chenye mafanikio TANGANYIKA (ndani ya serikali tatu ya muungano).

  Pili, baada ya kufa kwa Azimio la Arusha, CCM sio chama cha kuwajali tena wananchi walio wengi (hasa wakulima), lakini pia kwa kiasi kikubwa sana, kime abandon tabaka la wafanyakazi; tukumbuke kwamba ni matabaka haya mawili (wakulima na wafanyakazi) ndio yaliunda msingi mkuu wa itikadi, sera na dira ya TANU (baadae CCM); Hoja kwamba CCM imetelekeza wakulima sio ngeni kwani, baada ta ziara yake vijijini kuaga wananchi, Mwalimu mkoani Singida alitoa hotuba kuthibitisha hilo;

  Harakati za M4C za Chadema zinalenga kwenda kuwafariji WAKIWA hawa wa TANU ambao Nyerere aliwatembelea 1962 kuwajulia hali huku akimwachia nchi Kawawa, na baadae kurudi na uelewa zaidi juu ya jinsi gani ya kuwatumikia; na baadae alipoenda kuwaaga kabla ya kuachana na nyadhifa yake ya Uenyekiti wa CCM (1990), alikuwakuta tayari katika hali ya UKIWA;

  Na Tatu, Chadema kama ilivyokuwa TANU, ni taasisi ya kisiasa ambayo ipo midomoni, masikioni na mioyoni mwa watanzania wengi kuliko chama kingine chochote cha siasa ndani ya Tanzania ya leo; kama ilivyokuwa kwa TANU, shughuli na harakati za Chadema zinagusa maisha ya kila siku ya watanzania wengi kuliko chama kingine chochote, kwa mfano kupitia upinzani wake mahiri bungeni kwa hoja zenye maslahi kwa walio wengi; mchakato wa katiba mpya, vita dhidi ya ufisadi & ufujaji wa mali ya umma n.k.

  3. Asili ya Upinzani dhidi ya TANU inafanana na ile dhidi ya CHADEMA
  Katika harakati za kufanikisha malengo yake ya kisiasa, TANU ilipitia changamoto nyingi zinazofanana na zile za Chadema katika Tanzania ya leo hii. Kwa mfano:


  • Aina ya Kwanza ya Upinzani - TANU ilipata upinzani mkali kutoka serikali iliyokuwa madarakani, hasa kupitia chama cha siasa cha wakoloni - United Tanganyika Party (UTP), kilichoundwa mwaka 1956, miaka miwili tu baada kuzaliwa kwa TANU (1954), kwa lengo la kuidhibiti TANU. UTP ilikuwa inaeneza propaganda kwamba TANU ni chama cha KIBAGUZI kwa vile kilikuwa kinajijenga miongoni mwa watu weusi pekee yake, huku chama cha UTP kikijinadi kama chama cha kitaifa kwani tofauti na TANU, uanachama wake ulikuwa wazi kwa watu Weusi, Wahindi na Wazungu; Chadema pia inakabiliwa na changamoto inayofanana na haya;


  • Aina ya Pili ya Upinzani kwa TANU - Serikali (mkoloni) na chama tawala (UTP) vilitumia makundi mbalimbali ndani ya jamii pamoja na influential leaders kukata makali ya TANU; Kwa mfano, serikali ilimtumia vyema Chifu Marealle na wengine kadhaa kukihujumu TANU; vile vile serikali ilijaribu kutumia vyama vingine vya siasa kuidhibiti TANU; Leo hii, Chadema pia inakabiliwa na changamoto zinazofanana na hizi;


  • Aina ya Tatu ya Upinzani - Upinzani dhidi ya TANU mara nyingi ulitokana na ‘PURE IGNORANCE' miongoni mwa watanganyika wengi; Lakini upinzani uliokuwa more effective ulikuwa ule FROM WELL INFORMED QUARTERS zilizokuwa na ‘genuine fears' of loosing privileged positions katika siasa na ndani jamii kwa ujumla; Hili pia linajitokeza nyakati hizi ambapo wapo watanzania wengi ambao wanakipinga Chadema out of ‘pure ignorance'; vile vile, upinzani mkubwa zaidi wa Chadema unatoka from well informed quarters – Baadhi ya viongozi wa CCM wasioheshimu demokrasia, na political allies wao katika dola, lakini pia wafanyabiashara, wote wakiwa na ‘genuine fears' of loosing privileged positions walizonazo sasa;


  • Aina ya Nne ya Upinzani - Serikali ya mkoloni ilipitisha sheria maalum ‘to govern' general societies ndani ya Tanganyika i.e. "The General Societies ACT", ambapo Msajili wake alitumiwa kikamilifu na Serikali ya Mkoloni kuikandamiza TANU, na pia kuchelewesha usajili wa TANU kwenye majimbo mbali mbali kwani Sheria ya Msajili ilikuja na mbinu ya kuvitaka vyama vya siasa kujisajili kwa hatua na sio mkupuo, kwa mfano chama cha siasa kusajiliwa Dodoma haikuwa na maana kwamba chama hicho kilikuwa na ruksa ya kuendesha shughuli zake kwa mfano Morogoro;mMchakato wa applications za usajili zilikuwa tofauti kimajimbo; Mkakati huu wa msajili wa Vyama ilipelekea TANU kupata tabu sana kuendesha shughuli zake za kisiasa kwa mfano Sukumaland, Dar-es-salaam, Tarime, North Mara, Singida, Rungwe, Musoma, Bagamoyo, Kilosa, Kisarawe, Kondoa – irangi na Lindi; Chadema pia inakabiliwa na changamoto nyingi zenye sura hii;


  • Aina ya Tano ya Upinzani - MATUMIZI YA WAKUU WA WILAYA (DCs) Kudhibiti Mienendo ya Vyama Vya siasa. Hili linaelezwa bayana ndani ya Kitabu cha Towards Ujamaa: Twenty Years of TANU. Serikali ya mkoloni ilitumia sana government machinery, hasa wakuu wa wilaya kuidhibiti TANU. Wakati wa ukoloni (na hadi sasa to a large extent), kazi kubwa ya Wakuu wa Wilaya ilikuwa ni kusimamia LAW & ORDER. Wakuu wa Wilaya waliongoza Mikakati ya ‘Ulinzi na Usalama' katika maeneo yao. Kwa mfano, katika mikoa ya Singida, Musoma, na Mwanza, Ma-DC walikuwa wakiendesha operesheni za kamata kamata viongozi na wanachama wa TANU, walikuwa wakiwaweka vizuizini, wakiwafunga jela, wakitoa amri ya kuvunja mikutano ya hadhara ya TANU, n.k. Justification ya Serikali kufanya hivyo according to Ruhumbika (1974) zilikuwa mbili:


  1. Viongozi wa TANU walikuwa wanaendesha Siasa za UCHOCHEZI;
  2. Viongozi wa TANU walikuwa WANATUMIA LUGHA YA KASHFA NA MATUSI kwa viongozi wa serikali.

  In the process, matawi mengi ya TANU yakafungwa kwa muda mrefu (mengine hadi miaka mitatu) na mikutano ya hadhara ikapigwa marufuku kwa muda mrefu sana maeneo kama vile Shinyanga, Tabora, Dodoma, Iringa, Kondoa – Irangi n.k. Chadema pia inakabiliwa na changamoto zinazofanana na hizi;


  • Nyerere's Millitancy
  Baada ya mkutano mkuu wa TANU Taifa uliofanyika Tabora mwaka 1958 na kuhudhuriwa na wajumbe 152 kutoka nchi nzima, na kuja na maazimio mengi ya kuendeleza vita dhidi ya utawala dhalimu, hapa ndipo hali ya kujiamini na ari ya upambanaji ikashika kasi miongoni mwa viongozi wa TANU. Kwa mfano, ni baada ya mkutano huu Serikali ya Kikoloni ikaona Nyerere amegeuka kuwa ‘a millitant', hivyo kumfanya kuwa enemy number one of the state, na kuja na azimio la kumuondoa Nyerere from circulation; Nyerere akakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kutumia lugha chafu na ya uchochezi dhidi ya viongozi wa serikali, na pia kutumia lugha ya uchochezi kwenye mikutano ya hadhara, na kuhukumiwa kwenda Jela miezi sita au kulipa faini ya shillingi elfu tatu.

  Shillingi ELFU TATU zilikuwa ni nyinga sana kwa wakati ule. Kwa mfano, mshahara wa waziri wa serikali (mzungu) ulikuwa ni shillingi 5,000/= Kwa mwezi; mtumishi wa ngazi ya juu mweusi shillingi 107/= kwa mwezi, mtumishi wa ngazi ya chini mweusi shillingi 45.50/= kwa mwezi; now given the taxation system ya kikoloni ambayo literary ilikuwa inachukua sehemu kubwa sana ya mshahara kwa makusudi, Serikali ya kikoloni haikutegemea kama TANU ingeweza ku ‘raise' 3,000/= ndani ya kipindi kifupi; lakini hilo lilifanikiwa na Nyerere akaachiwa huru, na Chadema pia inakabiliwa na changamoto zinazofanana na hizi – hasa, tendency inayoanza kujitokeza miongoni mwa baadhi ya viongozi wa CCM kwamba viongozi kama Lissu, Mnyika, Dr. Slaa na wengine wanaonyesha ‘millitancy' dhidi ya serikali, hivyo kuwa maadui wakubwa wa CCM na serikali yake.

  Tunaendelea na mjadala wa Mfanano baina ya TANU na Chadema. Ufuatao ni Mfanano wa NNE hadi NANE.

  4. Waasisi wao TANU na CHADEMA wanafanana
  TANU ilitokana na chama cha TAA. Chama cha TAA kilianzishwa na kundi la Watumishi WEUSI wa serikali pamoja na wafanyabiashara weusi wachache waliokuwepo ambao kwa pamoja na kwa kuanzia, walikuwa concerned zaidi na hali duni za maisha ya watanganyika – kijamii na kiuchumi. TAA hakikuundwa kwa madhumuni ya kisiasa; Siasa zilikuja baadae sana; Chadema pia mwasisi wake Edwin Mtei alikuwa ni mtumishi wa serikali ambae alianza kupingana na sera za Ujamaa kwa imani kwamba sera hizi hazikuwa na majibu kwa hali duni za maisha ya watanzania – kiuchumi na kijamii. Mzee Mtei hakupingana na Mwalimu kisiasa bali kisera, hasa kiuchumi; upinzani wa Mtei dhidi ya CCM Kisiasa ulikuja baadae. Vile vile, kama ilivyokuwa kwa TANU, Chadema kilijizatiti zaidi baada ya kufanikiwa kushawishi baadhi ya watumishi wa serikali (retired/resigned) na wafanyabiashara weusi kujiunga na Chadema.

  5. Harakati za TANU na CHADEMA Zilianzia mijini kabla ya vijijini
  Chama cha TAA (mzazi wa TANU) kilianza harakati zake mijini chini ya watumishi wa serikali weusi na wafanyabiashara weusi. TAA (na baadae TANU) haikuanza na ujenzi wa ‘base' miongoni mwa wakulima vijijini, kazi hii ilikuja baadae baada ya Nyerere kugundua mapungufu yaliyojitokeza, na hatimaye kugeuza TANU kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi, lakini hasa wakulima ambao ndio walikuwa ni wengi. Ilichukua muda mrefu kwa TANU kuweza jenga ‘base' yake miongoni mwa wakulima na wafanyakazi, na kazi hii haikumalizika. Chadema pia kilianza kama chama cha mijini kilichoongozwa na wafanyabiashara na watumishi wa serikali (retired/resigned); Kusambaa kwa Chadema vijijini kunakuja taratibu, lakini wengi wanatarajia penetration vijijini itashika kasi zaidi kupitia M4C;

  6. TANU na CHADEMA Wanatumia zaidi Sera ya Kuajiri Viongozi (recruitment of leaders) kuliko Sera ya Kurithishana Uongozi (Leadership Succession)
  Ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa, TANU ilihitaji kuwa na ‘enlightened people' na iliajiri na ku-groom watu wengi katika nafasi za uongozi; TANU ilijitahidi sana (sio wakati wote) kuzuia sera za kurithishana madaraka kwani ilipotokea hivyo, ilikuwa ni mara chache sana (mifano ipo); Vinginevyo TANU iliajiri na ku-groom watu mbalimbali ili waje kuwa viongozi wake kwa mfano: Bomani (Sukuma Land), George Kahama (Kagera), Eliufoo (Chagga land), Mwanjisi (Nyakyusa land) n.k; Chadema pia, jinsi kinavyozidi kukomaa kisiasa,kinaonyesha jitihada za kujaribu kuajiri viongozi (recruit) kuliko kurithishana uongozi (succession); Ni kutokana na hili, ndio maana Chadema inazidi kuwa kimbilio la vijana wengi; hadi sasa, Chadema imefanikiwa kupata viongozi kama Mnyika, Lissu, Mdee, Zitto, Sugu n.k ambao wameajiriwa na kuwa groomed na chama. Faida kubwa iliyonayo Chadema pia ni kwamba, wananchi pia wamejenga imani miongoni mwa watu hawa na kuwapa dhamana ya kuwa wawakilishi wao bungeni kupitia chaguzi kuu zenye ushindani mkubwa wa kisiasa;

  7. Chimbuko TANU na CHADEMA ni SAUTI YA WANYONGE
  Chimbuko la TANU lilikuwa ni wananchi wanyonge; Hali hii inajitokeza pia kwa Chadema na ni jambo lililo dhahiri hivyo sina haja ya kulijadili kwa kina.

  8. Vyama Vyote vina msimamo mkali dhidi ya Ufisadi.
  TANU ilikuja na msimamo mkali dhidi ya Ufisadi; Chama kiliweka kanuni ya wazi kabisa kwamba: RUSHWA NI ADUI WA HAKI, SITATOA WALA KUPOKEA RUSHWA. Nyerere aliamini kwamba rushwa iliwanyima haki maskini,. Kutokana na msimamo huu mkali na pia sere za vitendo, TANU ilijinyakulia mtaji mkubwa wa kisiasa miongoni mwa wananchi.

  Chadema nayo katika nyakati hizi, hasa kuanzia mwaka 2005 imekuwa na Msimamo mkali sana dhidi ya Ufisadi, na imefanikiwa kujinyakulia mtaji mkubwa wa kisiasa kutokana na msimamo huu.

  SEHEMU YA TATU: Tofauti Baina ya TANU na CHADEMA

  Baada ya kujadili ulingano baina ya TANU na Chadema, zifuatazo ni tofauti nane baina ya vyama hivi viwili:

  1. TANU kilikuwa ni chama cha Kijamaa (mrengo wa kushoto) kilichosimamia sera za Ujamaa na State – led development na kupinga sera za soko huria; Chadema ni Chama cha mrengo wa kati na kinasimamia itikadi ya uliberali (ya mrengo wa kati), na kinaunga mkono sera za soko huria;
  2. TANU kilikuwa na Dira; Taifa lilikuwa na DIRA iliyokuwa wazi kwa kila mwananchi ya WAPI taifa linataka kwenda na NINI kifanyike kufika huko, na dira yake ilikubalika na watanzania walio wengi; Chadema HAINA DIRA rasmi inayoeleweka kwa wananchi zaidi ya sera mbalimbali zinazohimiza masualaa kama vile Utawala Bora; kubana matumizi ya fedha za umma; vita dhidi ya ufisadi; uboreshwaji wa huduma za kijamii; usimamizi wa rasilimali za taifa; uwajibikaji; na utawala wa sheria – hasa kupitia katiba mpya;

  3. TANU
  ilijijenga miongoni mwa Wakulima na Wafanyakazi, lakini hasa wakulima ambao ndio walikuwa wananchi wengi (kama ilivyo hata sasa); Chadema bado haijafanikisha hili;

  4. TANU (na baadae CCM), imepitia mabadiliko makubwa manne nchini: Uhuru (1961); Ujamaa (1967); Mageuzi ya Kiuchumi (1985/6); na Mageuzi ya Kisiasa (1992); Chadema imepitia badiliko moja tu: Mageuzi ya Kisiasa (1992);

  5. Mafanikio ya TANU
  yalijitokeza ndani ya mfumo wa chama kimoja ambao ulikuwa hauna ushindani, wakati mafanikio ya Chadema yanajitokeza ndani ya mfumo wa vyama vingi wenye kila aina ya ushindani wa kisiasa;

  6. Iliichukua miaka saba tu
  tangu kuanzishwa kwa TANU (1954) kabla chama hiki kukamata dola ya nchi (1961) tofauti na Chadema ambapo sasa ipo katika mwaka wa kumi na sita kwenye ulingo wa kisiasa za ushindani; suala hili linadhihirisha udhaifu wa hoja ya Mzee Sitta kwamba Chadema haipo tayari kuongoza nchi kwa vile haina hazina ya kutosha ya viongozi kwani TANU iliweza ndani ya miaka saba tu.

  7. Ushiriki wa TANU
  katika siasa za Muungano (shughuli za kisiasa Zanzibar) ini kwa kupitia ubia TANU na ASP (1977), na hivyo kufanya shughuli zake TANU (sasa Zanzibar kuwa rahisi zaidi kuliko ilivyo kwa Chadema; Mafanikio ya Kisiasa ya Chadema Zanzibar yanakwazwa na mfumo mbovu wa muungano; Chadema ikipata mbia wa kisiasa kama ASP kwa TANU, chini ya mfumo mbovu wa sasa wa muungano, pengine mambo yatabadilika; nilishalijadili hili kwa undani katika sehemu ya PILI ya mjadala huu;

  8. Tofauti na Chadema
  , harakati za kisiasa za TANU hazikushamiri sana ndani ya Bunge wakati wa mkoloni, kwani pamoja na Nyerere kuteuliwa kuwa Mbunge na Gavana wa kikoloni, Nyerere alichukua uamuzi wa kujiuzulu muda mfupi baadae kwa maelezo yafuatayo: Source (Towards Ujamaa: Twenty Years of TANU Leadership (1974):

  "[I have given everything that it was in my power to give and what I have given has been rejected. I came to the council expecting a little of the spirit of give and take. That spirit is not there. I would feel that I am cheating the people and cheating my own organization if I remained on the council, receiving allowances and attending sundowners as an Honorable Member, giving the impression that I was still of some service on that council, when in fact I know that I am useless. I had therefore no alternative but to tender my resignation and to ask that my resignation take effect from Friday, 14[SUP]th[/SUP] December, 1957, the day my last compromises were rejected by the government"].

  Tofauti na TANU, Chadema ina nafasi ya kuendesha harakati zake za kisiasa kote – Nje na ndani ya BUNGE; Pia kuna suala hapa worth mentioning: Hoja ya Halima Mdee kuhusu James Mbatia (Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa) kwamba ana mahusiano na CCM ilijadiliwa na wengi humu kwamba ni hoja sahihi pale Mbatia alipoteuliwa na Mwenyekiti wa CCM kuwa Mbunge; Hoja ya Mdee kwa kiasi fulani ina mahusiano na hoja ya Mwalimu Nyerere hapo juu; JE:

  James Mbatia alifanya uamuzi sahihi kukubaliwa uteuzi au ilitakiwa afanye uamuzi kama wa Nyerere? Nia ya mjadala wangu sio kubaini hilo, lakini niseme tu kwamba ni matukio kama haya ndio yanazidi kuing'arisha Chadema mbele ya umma unaojihisi kusalitiwa na CCM na kuachwa YATIMA, kwani Chadema imekuwa inajenga hoja kwamba HAINA UBIA wa aina yoyote na CCM, tofauti na mtazamo wa watu wengi juu ya uwepo wa mahusiano baina ya CCM na vya vyama vingine vya siasa .

  SEHEMU YA NNE - Hitimisho:

  Ni matumaini yangu kwamba kufikia hapa, tumeweza kutengeneza angalau mazingira ya kujenga mjadala juu ya ulingano na utofauti baina ya TANU na Chadema; Vile vile ni matumaini yangu kwamba nimejaribu kuweka mjadala huu katika muktadha ulio sahihi (the right context), kwa nia ya kukabiliana na upotoshaji unaojitokeza kwenye mijadala mingi ya namna hii kwamba ulingano baina ya TANU & Chadema ni more of a POLITICAL ASSET TO CCM as it is more of a POLITICAL LIABILITY TO CHADEMA. Mtazamo wangu binafsi ni the other way round Yani - kufananisha TANU na CHadema is more of a ‘POLITICAL ASSET' TO CHADEMA THAN A POLITICAL LIABILITY and it is more of a ‘POLITICAL LIABILITY' TO CCM THAN A POLITICAL ASSET. Mtazamo huu matokeo ya hoja niliyojaribu kuijenga awali kuhusu jinsi gani TANU/CCM imesaliti historia yake yenyewe and its repercussions, kwahiyo mjadala wowote unaolenga kufananisha TANu na CHADEMA offers more political mileage for CHADEMA kuliko CCM.

  Kama nipo sahihi katika hili, basi nina amini kwamba tupo katika nafasi nzuri zaidi ya kubaini changamoto zinazoikabili Chadema, lakini vile vile CCM. Vinginevyo nasimama kupingwa, na naomba kuwakilisha.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Naam...
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ni uchambuzi mzuri Mchambuzi...I salute you! From now on I will pay more attention to what you say, you have earned my respect. Nitaanza kupitia tena michango yako kwa umakini zaidi kuliko hapo nyuma...for the first time I am seeing you in a completely new light kwa sababu tofauti na wana CCM wengi, I think you are real!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi nimependa sana hii. Niliwahi kuandika pia kidogo kuhusu ulinganifu wa aina yake kati ya CDM na TANU. Kwa upande wangu hata hivyo niliangalia ulinganifu huo kama harakati dhidi ya mifumo miwili inayofanana sana. TANU iliongoza harakati za uhuru ili kuondokana na utawala wa kigeni (ukoloni) na kuwapa wananchi nguvu ya kuendesha taifa lao. Ilikuwa ni harakati iliyotaka kuhakikisha kuwa wananchi wa iliyokuwa Tanganyika wanaamua mambo yao wenyewe, wakitumia uwezo na raslimali zao wenyewe kwa faida yao na ya watoto wao. Zilikuwa ni harakati za kuamua siasa za Tanganyika zinaendeshwa na Watanganyika (bila kujali rangi japo kulikuwa na elements za kudai haki ya 'weusi' kujiamulia mambo yao).

  Mfumo wa ukoloni ulidhalilisha utu wa Mtanganyika. Kwani ukoloni kwa asili yake ni utawala uliojipachika juu ya wananchi, ukisimikwa na kulindwa kwa kutumia sheria na taratibu mbalimbali. Ni mfumo ambao kwa asili ni kandamizi (oppresive system). Hata unapofanya mazuri - kujenga mashule, barabara, elimu, n.k - unafanya hivyo kwa ajili ya kuutumikia mfumo huo (wale walionufaika zaidi na mfumo walitarajiwa kuingia ndani ya mfumo kuutumikia). Lakini matokeo yake kwa kiasi kikubwa yalitengeneza kikundi cha watu wachache ambao walikuwa ni 'watawala' huku wengi wakiwa ni 'watawaliwa'. Watawaliwa hawakuwa na sauti dhidi ya watawala.

  Hivyo, TANU inapokuja inakuja kuupa changamoto mfumo huu kandamizi.

  Kwa maoni yangu Ufisadi una athari zile zile za ukoloni. Umetengeneza kikundi cha watu wachache kuwa ni watawala, unatumia nguvu kubwa kujilinda na unanufaisha wageni kwa namna ambayo ili wenyeji wafanikiwe ni lazima wajihusishwe na wageni hawa! NI mfumo ambao kwa asili yake nao ni kandamizi. Hata pale unapofanya mambo - kujenga madaraja, shule, barabara n.k - unafanya hivyo kama namna ya kunyamazisha manung'uniko siyo kwa ajili ya kupanua wigo wa nafasi za kufanikiwa. Nafasi za kufanikiwa zinazidi kuwa chini ya kikundi kidogo cha jamii.

  CDM inapokuja inakuja ikitoa changamoto kwa mfumo huu kandamizi (CDM comes posing a clear challenge to this oppresive regime). Tofauti kubwa ambayo ninaiona kati ya TANU na CDM kwenye kupambana na mifumo hii na kwa kiasi pia umeonesha hapo juu ni kuwa uongozi wa TANU ulielewa kabisa unachotaka kufanya na ulianza kukifanya mapema ukijitegemea wenyewe nje ya serikali ya mkoloni. CDM inategemea sana CCM ili iweze kufanikiwa. TANU haikupewa ruzuku ili kufanya harakati zake wakati CDM bila ruzuku ni kama kitu ambacho hakifikiriki. Ni ruzuku hii ndio ambayo kwa maoni yangu imedumaza sana harakati za kisiasa nchini.
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mchambuzi nimeanza kusoma nikagundua kuna kakosa kadogo. Nitai print nisome. Ila rekebisha Msekwa si Katibu Mkuu wa kwanza wa TANU bali CCM.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Hongera na asante sana kwa kututoa porini na kutuleta barabarani.
   
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  uko right but all in all jamaa kafanya kazi nzuri sana,ngoja tusome sasa kwa umakini kabla ya kuingia kichwa kichwa kwenye hii kitu yake
   
 8. Mhamiaji Haramu

  Mhamiaji Haramu Member

  #8
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukweli mtupu..
   
 9. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kweli wewe ni Mchambuzi,mengi uliyoyanena huo ndio ukweli wenyewe,good analysis.
   
 10. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  In most times, if not always, I salute and appreciate your analysis Mchambuzi; you have always deserved my respect!Btw, tofauti nyingine kubwa (bila shaka umeigusia katika maeneo baadhi) ni tofauti ya nyakati tulizopo, tuko katika kipindi ambacho asilimia kubwa ya watu at least 'wana uelewa' wa mambo, iwe kwa kupitia madarasani au kwa kusikia na kuona kwenye vyombo vya habari na kwingineko duniani, juu ya nini kinaendelea.
   
 11. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji,

  Nashukuru sana kwa mchango wako. Nakubaliana na wewe kwamba ulinganifu baina ya vyama hivi viwili unatazamika pia kama harakati dhidi ya mifumo kama ulivyoainisha; Ni kweli kwamba taifa linapitia mfumo kandamizi usioweza vumiliwa na walio wengi, kwa mtindo ule ule wa ukoloni; Tofauti kubwa baina ya mfumo wa kikoloni na huu wa leo ambao ni ukoloni mamboleo ni kwamba watanganyika tumepewa KWA KIASA TU, Uhuru wa kisiasa ili tuhisi kwamba tunajitawala wenyewe huku maamuzi makubwa ya kisiasa na ya iuchumi yakiendelea kufanywa na wakoloni wale wale indirectly kupitia World Bank na IMF; Wakoloni wale wale wanaendelea kutufanyia maamuzi ya kisera (hasa katika nyanja ya uchumi), na pia wanaendelea kushikilia njia kuu za uchumi, wanahodhi mitaji na faida (profit) kwa manufaa yao, sio kwa manufaa ya Wananchi, na kwa kiasi fulani, watawala wetu wanawasaidia Wakoloni hawa kufanikisha hili; Nyerere alijitahidi sana kupingana na mfumo huu, hasa enzi za TANU, kwani baada ya TANU kufariki na Tanganyika, Taifa lilianza kuyumba kidogo in terms of prioritization and execution ya mambo muhimu ya taifa;

  Vile vile upo sahihi juu ya Ufisadi na athari zake zinazofanania na Ukoloni. Sikutazama hili kwa jicho hilo, hivyo asante kwa kunifungua zaidi; Tunazidi kushuhudia jinsi gani HAKI YA MUNGU (Rasilimali) tuliopewa watanzania zikigeuzwa kuwa HAKI YA MZUNGU kwa hoja kwamba wazungu ndio wenye uwezo wa kuendeleza rasilimali hizo kwa faida yetu; Lakini inapotokea Watanzania wenye weusi wenye uwezo huo, zinajengwa hoja nyingine kuwanyima fursa hizi – kwa mfano, rejea sakata la Reginald Mengi wakati wa mchakato wa ubinaifishaji; Watawala wetu ndio mabingwa wa kutunyan'ganya HAKI YA MUNGU na kuigeuza kuwa HAKI YA MZUNGU, na ni Rushwa ndio hutawala mchakato huu – rejea sakata la mamilioni ya dollar za watawala wetu kwenye mabenki kadhaa huko Uswisi na kwingineko.

  Pia nimependa sana hoja yako kuhusu harakati za TANU kutotegemea ruzuku, tofauti na harakati za Chadema nyakati hizi; Huu ni utofauti mwingine baina ya vyama hivi ambao sikukumbuka kuujadili; Tofauti na Vyama vingine, CCK kina sera Rasmi ya kupinga Ruzuku hizi, lakini binafsi naona hili suala ni kama ‘a double edged sword' kwani, kuchukua ruzuku kunapelekea madhara uliyoainisha, lakini vile vile kuikacha ruzuku kunapelekea kudumaa kwa demokrasia kwani vyama hivi vishindwa kujiendesha kwa ufanisi; Hii ni changamoto kubwa sana ambayo hata wahisani wanapata shida sana kuipatia ufumbuzi wa kudumu hasa ikizingatiwa kwamba kitendo cha kusaidia vyama vya siasa kifedha ni kinyume cha utaratibu lakini vile vile, kitendo cha kuliacha tatizo hili bila ufumbuzi wa uhakika, na kinadumaza demokrasia;
   
 12. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi asante sana.

  Ni uchambuzi uliofanywa kwa umakini mkubwa. Kwa kifupi uchambuzi wako huu maridhawa umeingia moja kwa moja kwenye archive yangu.

  Wakati huo huo umeamsha ghafla hamasa ya mimi kuyatafuta ili nipekue baadhi ya makbrasha ya zamani kulingana na reference ulizoweka humu; kwa maana umekwenda deep & wide sana!

  Very well done. BIG LIKE too
   
 13. H

  HByabatto jr Senior Member

  #13
  Sep 19, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa mchango wako.
   
 14. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  A merit Phd! Ukiitwa Dr ni halali yako mkuu wangu Mchambuzi. A complete 5 star master piece of Analysis . I like it bro.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  A merit Phd! Ukiitwa Dr ni halali yako mkuu wangu Mchambuzi. A complete 5 star master piece of Analysis . I like it bro.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Umasikini tulionao ni matokeo ya TANU. maisha ya mtanzania wa kipindi cha mkoloni mweupe hayana tofauti sana na mkoloni mweusi (ambaye mwaasisi wake ni nyerere). kwa hiyo kama na chadema ndo lengo lenu basi ni wakuepukia mbali kama ukoma.
   
 17. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mchambuzi, hii analysis imetulia. I like it!
   
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi umegusa penyewe! Huu ni ukweli mtupu!
   
 19. n

  nsanu Member

  #19
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  very interesting analysis
   
 20. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Umasikini tulionao kwa sehemu pia ni matokeo ya kuongezeka kwa idadi ya mijitu mivivu ya kujisomea na kujielimisha na kubakia kulaumu waasisi wa taifa. Mijitu ya namna hii hupendelea kukaa vijiweni na kusimuliwa hadithi yanayopenda kuzisikia.
   
Loading...