CHADEMA na maandamano

Khaa hapo unaona unaijua history ile mbaya eeh? Mtanzania wa leo hakosi chochote??? Anapata vyote mkuu hadi mabomu ya mbagala na Goms.... Tangu nchi hii ipate uhuru watanzania wamekufa tu kwa kuliwa na wanyama?!
 
mtoa mada, ni mchanga sana kifikra na pia anahitaji kusaidiwa kwa kupewa taarifa za kutosha, natamani Nchi nzima ifanye maandamano ndani ya siku moja na yaendelee siku zote mpaka tumtoe mkwere ikulu.


Kama ni ya nchi nzima itaandamana its ok. lakini ukisoma vizuri concern ya mtoa maada (ambaye anaweza pia kuwa mwana CDM!) ni kwamba CDM ina ji associate mno na maandamano kiasi kwamba itakuwa ndiyo trade mark ya CDM ukiacha ile ya PIPOOOOZ PAWAAAA!!! yaani badala ya kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, kina kuwa Chama cha Demokrasia na Maandamano!! (what a name!)
 
Emma 26 nadhani ufikirie kwanza kabla ya kuleta madhaifu yako hapa JF. Unaishi ulimwengu gani? Jaribu kutafakari hali za wananchi na angalau kutafuta namna ya kushinikiza mambo au hatua za dhati zichukuliwe. Kwa mfano hizo hela za Dowans wange- subsidise kwenye gharama ya sukari ili bei iweze kuwa kawaida na mwananchi aweze kuimudu. Hali ya maisha kwa mtu wa kawaida hapa Tanzania imwekuwa unbearable. Pse tubu haraka!!!!!!
 

Ukimuamsha aliyelala..........!
Ila kama mtanzania unajua hali halisi ya taifa letu kama kiongozi wa nchi anaamua kulidanganya taifa mchana kweupe unategemea nini? NIWAKATI UMEFIKA KUWAELIMISHA JAMII KUTOKA KWENYE MAWAZO MGANDO NA KULITETEA TAIFA. Kuwa mwanaharakati mezani panapo shindikana kinachofuata ni kupaza sauti.
PEOPLE'sss power
 

Huo ndo uwezo wako kifikra, waache wenye fikra pevu wakuletee mabadiliko
 

Kwanza kajifunze kiswahili fasaha ndio urushe upuuzi wajo humu.

Maanadamano ni haki ya kikatiba na ni njia mojawapo ya kufikisha ujumbe kwa wahusika

Inaonekana wewe unaishi sayari ya PLUTO:A S 13:
 

Mimi nafikiri ndugu yangu bado hujafahamu kinachoendelea katika taifa hili au unafahamu lakini una ushabiki na CCM sasa basi hata kama ni mwana CCM hilo sio tatizo, tatizo ni kuangalia wapi tulikuwa kama taifa na sasa tupo wapi na tuchukue uamuzi gani ili tuelekee kwenye njia sahihi.

Maandamano ni haki na ni haki kwa kila raia, Chama au hata kikundi cha watu ili mradi wanafuata taratibu na hawavunji sheria za nchi, kwa hivyo huwezi kutuzuia tusiandamane.

Ugumu wa maisha umesababishwa na serikali isiyo makini na isiyo na "Vision" and "Mission" walichukua uongozi sawa, sasa what next! hawajui zaidi ya kuiangamiza nchi.

nchi ya Tanzania na Visiwa vya japan nani anastahili kumsaidia mwezie Chakula!?ajabu Japan ndio anasaisia mwenzie, pamoja na mambo mengi tuyajuayo miundo mbinu mibovu nayo imechangia kusababisha njaa, kuna sehemu vyakula, matunda na malighafi nyingine vinaoza na kuharipika ilhali kuna sehemu nyingine za nchi wanakufa njaa na kukosa malighafi za viwandani.

Tunataka Rais atakayeweza kuona vipaumbele, yaani kipi kifanyike kwanza na kwa manufaa gani, na ambaye atasimamia uwajibikaji wa kila idara na kila mtumishi na mwenye kuona Taifa letu litakuwa wapi baada ya miaka kadhaa, na huyo si mwingine ni Dr, Phd. Slaa.

Mungu Ibariki Tanzania, Tubariki Wananchi wenye nia safi, Ibariki Chadema na Viongozi wake wenye nia njema.
 

hivi hii 26 in represent umri wako au, hata kama ni hivyo bado hii siyo excuse, sasa nakushauri ukajifunze kwanza kiswahili, lugha ambayo hai hitaji kusoma academia wala intaneshino skuli, sina haja ya ku highlight yale ma broken uliyoweka. hapa tunazungumza mambo ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu, usituletee lugha zako za 'mimi kama mimi' hapa eeeboh!!! nimekasrika sana mtanisamehe wajameni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…