CHADEMA na harakati za kupinga posho; msimamo wa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA na harakati za kupinga posho; msimamo wa wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Dec 11, 2011.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CDM) kimekuwa kikitoa kilio chake cha kupinga posho mbali mbali zinazolipwa na serikali au mashirika ya umma pamoja na wanasiasa kwa ajili ya vikao vya kikazi. CDM wanaona kuwa ni wajibu wa mfanyakazi kufanya kazi aliyoajiriwa nayo bila kulipwa posho ya kufanya kazi hiyo. CDM wamejikita kwenye hoja kwamba kama inaonekana kazi haendani na kipato ni wakati wa kuangalia mishahara ili iendane na kazi husika badala ya kakundi kadogo kujilipa fedha nyingi kwa kisingizio cha posho na kusahau kundi kubwa la wavuja jasho bila posho za kujikimu kama waalimu, madaktari, polisi, wanajeshi, manesi, wakulima, wafanyakazi nk.

  Je kilio hiki ni cha CDM pekee, je kilio hiki ni cha wanasiasa? yako wapi makundi yanayoathirika? wako wapi waalimu? wako wapi wanajeshi na polisi? wako wapi wakulima na wanafunzi?

  Wabunge wa CDM wakiwa wanauwezo wa kukaa kimya na kula posho zao ambazo zinapanda kila kukicha na vikao vingi vinavyopangwa na bunge kwa ajili ya kulipana posho, wao walau wameamua kutuonyesha jinsi watetezi wetu walivyoamua kutusahau na kugawana keki ya nchi wenyewe.

  Imefika wakati kwa kila mpiga kura kutathimini kama hii ndio kazi ya mbunge wake na bunge kwa ujumla. Kazi kubwa ya Mbunge ni kuonisha mahitaji ya wananchi wa sehemu husika na kuyapeleka bungeni na kutetea maslahi yakinifu kutokana na uchumi uliopo na vyanzo vyake. Je kujilipa miposho bila uwiano hilo ndilo lengo? kweli wanatukumbuka? Kwa nini hatusikii wakisema inabidi mwalimu alipwe posho ya kujikimu anapoingia darasani? Kwa nini daktari asilipwe posho ya kujikimu anapotibu mgonjwa. Kweli bado tunahitaji bunge na hawa wabunge tulionao??

  Hii vita isiwe ni vita ya wabunge 48 wa CDM na viongozi wao dhidi ya uongozi mbovu wa serikali na bunge isiwe vita ya wachahe ni vita yangu ni vita yako ni vita yetu. Tuamke tupiganie haki zetu, kodi zetu ni mali zetu sote tunawajibu nazo sio kajikundi ka wapumbavu wachache wanaofikiri wao ndio wanahitaji pumzi kuliko sisi.

  Watanzania hakuna mwanasiasa anayetupenda wala kutujali kama sisi wenyewe hatujijui, wakati umefika kujua majukumu ya serikali na bunge kwetu. Tunaweza kuwawajibisha tukiungana. Hakuna sababu ya kutengana kwa hili, tuache uvyama hautusadii wote tunaibiwa bila kujali itikadi zetu. Wote tunanyanyaswa na kadi za vyama vyetu mifukoni. Wote tunauwawa na umasikini wetu huku tukiwapeperushia bendera.

  Lets say No to POSHO.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni kwamba hata CDM wakipanga maandamano hao wahusika wanaotetewa hutowaona.
  Natamani wananchi wa Tanzania wangekua na sauti wakatae kutumika maana hii sasa imezidi. Watoto wanabanana madarasani, walimu wanafundisha bila malipo ya kuridhisha, madaktari wanafanya kazi katika mazingira yasiyoridhisha, wagonjwa wanabanana mahospitalini, watoto wamezagaa mitaani alafu wabunge wanaongezeana posho wakati hamna la maana wanalofanya zaidi ya kula pesa za wananchi tu.

  Alafu eti watu wanasherehekea miaka 50 ya uhuru. Uhuru gani walio nao wananchi? Uhuru wanao hao wakubwa maana ndio wanaogawana nchi bila kuulizwa.
   
 3. d

  dada jane JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Even me am saying no to POSHO.
   
 4. Mashamba

  Mashamba JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  :A S embarassed: BIG NO TO POSHO .
   
 5. I

  Imurumunyungu Senior Member

  #5
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mnategemea mbunge kama shibuda atetee wananchi kweli jamani?.Yeye kaenda bungeni kuchuma through POSHO.Tujipange wananchi 2015 wabunge wa type ya SHIBUDA Tuwatupilie mbali wakatafute posho hata kwenye biashara ya matikiti maji na cyo kwenye kodi zetu.
   
 6. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tukumbuke kuwa vita dhidi ya posho siyo vita ya CDM bali ni vita inayofanywa ma mbunge mmoja tu wa CDM ambaye ni Mhm Zitto. Kama CDM wenyewe wameshindwa kuwa na msimamo mmoja kama chama, sisi wananchi wa kawaida tutaweza vipi?
   
 7. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  We makalio wacha umbea wako kenge usie na aibu!
   
 8. Bepari

  Bepari JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 814
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Well said mkuu, ni Zitto tu tuache unafiki. Chadema kama chama hawachukii hizo posho ndiyo maana hakuna vitendo.
  Wana kawaida ya kususa wakimaanisha kutokubaliana japo hawana nguvu kwa uchache wao. Wanasema "kufikisha ujumbe", ni dhahiri kuwa hili wamelibariki maana kama ni maneno mbona hata Ccm wanapinga!!
   
 9. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Kwanza tuwashukuru wabunge wote walioonyesha kukerwa na posho bila kujali vyama vyao. Pili tujiulize sisi wananchi tupo upande gani. Swala la hii vita ni ya Zito au la haisadii ila Tumshukuru Zito kwa kuonyesha msimamo wake na wale wote kwenye list ya kupokea hizo posho wanaoonyesha utetezi kutusaidia au kutuelimisha. Imebakia kwetu sisi ambao tunafanya kazi kwenye mazingira magumu bila posho, huduma za jamii zote ziko juu je spika hilo hajaliona bei za bidhaa Tanzania nzima zimepanda mno.

  Je mimi na wewe tupo kundi gani? Mimi nasema no to POSHO na nitamuunga mkono yeyote anayepinga hizi posho bila kujali itikadi je wewe mwenzangu, mwalimu, mwanajeshi, polisi, daktari, nesi, karani, nk upo upande gani????????
   
 10. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii vita ni yetu sote tuwaunge mkono wanaozikataa posho hizi kwani huu ni unyonyaji mkubwa.
   
 11. N

  N series Senior Member

  #11
  Dec 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  natamani pachafuke nimtwange hta she/vibuda na yai viza,jitu linawaza tumbo tu,kweli ndumi la kuwili . .
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Dec 11, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  aache umbea ili tusijue kuwa wabunge wa CDM wanapokea posho nene au aaache umbea kwa kusema ukweli??

  acha unafiki bro.
   
 13. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Umeongea vyema mkuu
   
 14. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ishu hapa sio nani kasema..posho ni mzigo kwa taifa letu..uzury wa tanzania hata wasio wenyeji wantoa maoni juu ya tanzania yetu....zitto ni ccm?
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wabunge wengi wa CDM wanajifanya kukerwa na posho lakini hawachukui hatua! Wanalia kilio cha mamba tu kutoa machozi huku wakimeza posho kama kawaida! Ni kweli kama alivyosema Rejao vita ya posho inaonekana kuwa ya mbunge mmoja mmoja na wala si CDM (matamko ya kichama bila vitendo) ama CCM ambao wamekaa kimya. CDM ni Zitto pekee aliyeonyesha kwa vitendo kwa kukerwa na posho baada ya kukataa kuzichukua na kwa CCM ni January pekee! Makamanda wa CDM wamekuwa wa matamko zaidi kuliko matendo hasa linapokuja suala la posho!
   
 16. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #16
  Dec 11, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kuchanganya hoja ya posho na itikadi za siasa<kwamba nani anachukua na nani hachukui,sijui mbona akina Mbowe na wenzake wanachukua nk>haiwezi kutusaidia.Hoja ni kwamba watanzania wote wenye mapenzi mema tukatae huu wizi.Hawa wapumbavu wachache hawawaonei huruma mama zetu wajawazito wanajifungulia sakafuni!Hawana huruma na wazee wetu wastaafu wanaolipwa chini ya laki moja kwa mwezi lakini wanalea watoto na wajukuu!Hawana huruma na wafanyakazi wanaoishi kwa mishahara mbuzi wakati huu wa mfumuko wa bei wa kihistoria!Wanachojali wao ni matumbo yao na ya mahawara zao tu.Mafirauni wakubwa hawa!Hivi tukiwaambia pumbavu zao tutakuwa tumekosea?
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  mkuu hapo juu upo sawa. katika suala la posho hakuna cha chama wala nini hapa ni wananchi kuinuka na kukemea na kuzikataa posho hizo. inaonekana wazi kwamba suluhu kisiasa haipo bali unafiki mtupu. katika posho wabunge wamesahau tofauti zao za kichama na kiitikadi na kuwa kitu kimoja. kinachonikera ni matamko yasiyo na tija ya wanasiasa wengi hasa wa CDM kuwa posho hatuziungi mkono lakini wanazimeza kama mamba. kwa nini wasizikatae kwa vitendo kama Zitto?
   
 18. m

  matawi JF-Expert Member

  #18
  Dec 11, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ningejua nisingesoma hii post maana imeamsha hasira zangu dhidi ya haya mazulumati hasa magamba wakiongozwa na magamba mkuu mkw€re
   
 19. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #19
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,612
  Likes Received: 2,993
  Trophy Points: 280
  Nadhani kumbukumbu yako ina matatizo. Mtu wa kwanza kupinga malipo makubwa ya wabunge yasiyofanana na ya Watanzania walio wengi alikuwa ni Dr. W. Slaa akiwa mbunge na Katibu Mkuu wa CHADEMA katika bunge lililopita. Dr. W. Slaa ni kiongozi na mtendaji mkuu wa Chama. Kauli ya kiongozi wa Chama ni kauli ya chama hata kama ndani yake kunaweza kuwa na wachache ambao wanaweza kuwa na mawazo tofauti. Ni kutokana na msimamo huo wa CHADEMA, ufutaji wa sitting allowance na posho nyingine tata likawekwa kuwa ni sehemu ya sera ya CHADEMA.

  Zito ni Naibu kiongozi wa upinzani bungeni, Mbowe ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Mnyika ni katibu wa wabunge wa CHADEMA bungeni - hawa wote wamesema kuwa CHADEMA haiungi mkono malipo ya posho na matumizi ya anasa yanayofanywa na serikali. Unataka aseme nani ndipo utaridhika kuwa CHADEMA kama taasisi haipingi posho tata kwa wabunge? Ni dhahiri CHADEMA kama taasisi ya kisiasa inapinga posho tata kwa wabunge na watumishi wote wa serikali. Mtu pekee ambaye tumesikia akipigania posho ni Shibuda, na hilo siyo jambo la ajabu. Chama kinaweza kuwa na msimamo fulani lakini baadhi wakawa na mawazo tofauti - na hao wanawajibishwa na chama chenyewe kama maamuzi yao hayo yanakiuka sera za chama, na ndiyo maana CHADEMA imeunda kamati ya kumhoji Shibuda kabla ya kuchukua uamuzi dhidi yake.
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena kweli hasa kuhusu historia ya kwamba dr slaa alipinga posho lakini kama kawaida ya utata wa CDM wakati anajitosa kugombea urais dr. akaingia MOU na CDM kwamba akikosa urais basi awe analipwa posho sawa na za wabunge (sina hakika kama naye amepandishiwa posho) ambazo.alikuwa akizipinga. Pia ni ukweli usiopingika kwamba CDM wanazipinga posho kwenye matamko lakini si kwa vitendo kama anavyofanya Zitto! Hivi kwa nimi wabunge wote wa CDM wasifanye kama Zitto wamuache Shibuda peke yake awe anapokea posho hizo ili tumzomee. manake kwa sasa ukitaka kuzomea ni Zitto tu hatazomewa lakini wengine wote watazomewa tu! Ningependa kama wabunge wa CDM wangekuwa wa matendo zaidi kuliko maneno na matamko ya hapa na pale kama utabiri wa hali ya hewa. Kataeni posho mbona mnamtosa Zitto?
   
Loading...