Moderators at JamiiForums..naomba mnapobadili au kuondoa topic,muwe reasonable...hii ni mara ya tatu.
Naweka mnahamisha ..naweka mnafuta...why?
Kuweni fair na sio biased otherwise toweni "Ban" ili mtu anaachana nanyi na kuendelea na mambo Mengine kwingineko!
Mnaacha topic nyingi sana humu, tena zenye kutukana hadi Marehemu kinyume na maadili ya kitanzania!
Lakini mnaondoa baadhi ya topic zenye kuwahusu baadhi ya wale tunaoona kama mnawakingia ngao....kwa mfumo huu mtaiuwa hii platform yenu taratibu....
#Maxencemello na mwenzako lifanyieni kazi hili jambo..
Sisi ni watu wazima hivyo hatuko humu kama burudani.
" Lema Toa Elimu Badala ya kutukana!"
Ndugu Godbless Lema ambae ni Muishiwa Mbunge wa Arusha zamani.
(sio mheshimiwa)maana hana huo ubunge kwa sasa.
Anaendelea kuzunguka nchini akitukana makundi mbalimbali ya kijamii hususan Bodaboda!..kama kawaida yake.
Na sasa ameirudia tena kauli yake safari hii akiwa Mwanza!
Mwanza!
Ambako ni kitovu cha wavuvi katika ziwa Victoria.
Nimetafakari maneno yake kwamba ..
"Bodaboda walioko kazini sasa,na wanaoongezeka ni dalili ya umaskini nchini."
Kwamba watakufa kwa "Neumonia" ndani ya miaka ishirini ijayo...(kwa utabiri wake wa vifo vya wenzake).
Baada ya hapo nikatafari pia mazingira ya wavuvi wadogo wadogo wa nchi mbalimbali Duniani.
Ambao huingia ziwani na Bahari kuu zote usiku kucha na kurejea nchi kavu asubuhi.
Na hii ni Lifestyle yao ya kila siku miaka nenda miaka rudi.
Na Mazingira ya kukesha majini kila usiku,wakinyeshewa na mvua kubwa na tufani za upepo.ni magumu kuliko Bodaboda ambao wanaendesha pikipiki zao nchi kavu.
Tena wakiwa wamevaa vifaa kinga kama Helmet,Jackets na hata Gloves kwa wale waelewa zaidi.
Sasa kwa uelewa wa Lema kuhusu vifaa kinga ....ingawa hawezi kuwa na takwimu zitokanazo na vifo vya Neumonia kwa Bodaboda Duniani.
Pia atueleze wavuvi wangapi wanakufa kwa :Neumonia" Tanzania na Duniani,kwa uelewa wake.
Aje atuambie ni kundi gani liko hatarini zaidi kati ya haya mawili.
Badala ya kutembea akibwabwaja bila kuwa na maelezo ya kitaalamu!
Badala ya Lema kubwabwaja bila kutoa njia mpya za kuikomboa kiuchumi hiyo jamii anayoibeza!
Ili kwamba labda Chadema wanayo njia tofauti ya kuwapanulia ajira...na aiseme ili tuichambue na kuielewa.
Anawatukana Bodaboda huku akiendelea kuwatumia kwenye misafara ya chama chake,huku akiwafitinisha na serikali iliyoko madarakani.
Anawatumia Bodaboda kama sera!
Lema anapaswa kuambiwa na aelewe kwamba...
Kila kazi ni hatarishi endapo haitakuwa na vifaa kinga kwa mtu anayetoa huduma husika.
Ndio maana hata madaktari wanakuwa na "PPE."
Wavuvi wanakuwa na "life Jackets" pamoja na vifaa vinginevyo ili kujikinga na baridi kali majini.
Ndio maana ya Bodaboda pia kutakiwa kuvaa "Helmet" imara na bora zenye kuwa pia na matundu ya kuchujia hewa.
Pamoja na "Jackets" imara ili kuwakinga na Upepo na Baridi.
Ndio maana wafanyakazi migodini wanapaswa kuvaa "Helmets","Safety boots" na "Safety Glasses."
Ndio maana hata Malaya na wazinzi wote wanapaswa kuvaa "kondomu" nk.
Kila kazi inaweza kupelekea ajali ambayo itasababisha kifo, pale ambapo vifaa kinga na vigezo sheria havitatimizwa au kutumika.
Kwa hiyo Lema anaporopoka maneno yake labda tuseme anawaongelea Bodaboda wake wa Arusha.
Ambao kwa ujumla ni watovu wa nidhamu ikiwemo kutotii sheria za usalama Barabarani zinazowapasa kuvaa vifaa kinga.
Badala ya kuvaa

Helmet.. wao huvaa kofia maarufa Arusha kama "Boshore"
Badala ya kuvaa ma Jackets wao wengi huvaa sweta na kisha kutoboa "Exhaust" za Pikipiki zao na kugeuka kero kwa jamii Barabarani kutokana na kelele mbaya za pikipiki zao.
Lema wakanye wanao kabla ya kuwatukana!