CHADEMA na ACT-Wazalendo wote simamisheni wagombea wa Urais, Ubunge na Udiwani kimkakati

Kasegela

Senior Member
Mar 24, 2019
127
261
Salam wana JamiiJorums,

Napenda kutoa maoni yangu juu ya CHADEMA na ACT-Wazalendo Kusimamisha wagombea wa Urais ,ubunge na Udiwani kabla ya kuungamisha nguvu.

Wapo wasioelewa kwanini Membe kachukua fomu wakati toka awali wapinzani wammeshaonesha kuwa watamuumga mkono. Hesabu zipo hivi.

Lissu achukue fomu tume ya taifa ya uchaguzi, Membe kadhalika achukue fomu

Pia, Maalim achukue fomu kwa upande wa Zanzibar na Mgombea wa CHADEMA mwenye nguvu achukue fomu.

Hii ni kanuni ya kutoweka mayai yote kwenye kapu moja hasa kwa kipindi hiki ambacho CCM inabuni kila mbinu ya kuharibu uchaguzi.

Malengo ya CCM kumkamata Lisu na kumpa kesi zisizokuwa na dhamana,yapo na endapo watafanya hivyo Membe aungwe mkono na Uponzani wote huku wakiendelea kumpigania Tundu Lissu.

Wakiona hiyo mbinu haiwalipi na kuamua kuacha Lissu, basi Membe amsaidoe Lissu kukusanya kura.Membe amuunge mkono Tundu Lissu.

Yaani hapo CCM watakosa pakukimbilia,huku kifo kule kuolewa

Zanzibar pia fanyeni hivyohivyo, Wakomfanyia zengwe lolote Maalim Seif (Japo haiwezekani) basi Mgombea wa CHADEMA apeperushe bendera ya upinzani na CCM wafurushwe madarakani kwa njia ya sanduku la kura.

Kadhalika kwenye Ubunge, wakiweka pingamizi kwa mgombe wa CHADEMA, wananchi waelekezwe waunge mkono mgombea wa ACT-Wazalendo. Na kinyumbe chake iwe hivyohivyo.

Hii ndio njia pekee ya kushindana na CCM yenye mbinu nyingi
 
Lissu anatoa taarifa za kufuatiliwa na gari isiyojulikana 2017


"hatufanyii kazi taarifa za kishabiki za mitandaoni sisi"

Lissu anatangaza kurejea 2020


"hata Hivyo tumeona katika mitandao ya kijamii baadhi ya viongozi wa Chadema wakihamasisha wananchi kukusanyika.

Kuna watumishi wana akili mbovu sana
 
Back
Top Bottom